Ajira hazilipi

Ndio maana wengine wanafidia kwenye posho.
 
Jambo la muhimu hapo ni kujitahidi kubuni miradi mingine ya kukuongeza kipato ili kukidhi mahitaji!.
 
Hivi hakuna kuvaa, kujirusha (kurelax), sahani vikombe vilivyovunjika... au ndo dharura yenyewe?
 
Tena uanaambiwa huyo ni meneja. Je akina sisi wa kima cha chini vp? Mshahara unatoka unaishia kulipa madeni tu
 
Jambo la muhimu hapo ni kujitahidi kubuni miradi mingine ya kukuongeza kipato ili kukidhi mahitaji!.

Hiyo miradi utafanyia ktk ofisi hiyo hiyo ulimoajiriwa? Au unataka uweke mtu asimamie, baada ya week unakuja jf kulalamika tena kuwa nduguyo kakuchakachua? Pagumu kidogo, kuwa na kazi ya ajira na kuwa na mradi mbali na ofisi yako. Ni mchango tu, yaweza isiwe kweli kwa wengine.
 
ukiweka na takrima hautoshi mkuu

Mkuu takrima si mpaka mwaka wa uchaguzi kama mwaka huu? Kwenye uchaguzi mwaka huu si si CM lazima watatumwagia mpunga wa kutosha, tutaenda hata shopping sasa
 

Mkuu Malila kuna kitu unataka Sema hapa ila kama hutaki kufunguka zaidi.

Tushirikishane miradi ambayo kwa uzoefu yako mtu anaweza kuifanya huku akiwa na ajira na akaweza kuisimamia vyema
 
Ukiwa na maisha yasiyo na anasa mambo yatakwenda vyema,ila sasa wengi wanaishi kwa kuiga nakufuata mkumbo kama siyo kupelekeshwa na matukio na mahitaji ya watu wao ambao kimsingi hawajui mtu unaingiza kiasi gan
 
Mkuu Malila kuna kitu unataka Sema hapa ila kama hutaki kufunguka zaidi.

Tushirikishane miradi ambayo kwa uzoefu yako mtu anaweza kuifanya huku akiwa na ajira na akaweza kuisimamia vyema

Ni kweli nimeshuhudia wafanyakazi wengi wakikopa na kuingiza fedha ktk miradi inayoishia kuwaneemesha watendaji/wasimamizi wa miradi husika. Hata mimi kuna mradi uliishia kuwa mradi wa kijana wangu na mimi nikawa napewa hesabu feki, ila nilishituka mapema na kubadili mwelekeo.

Mradi wa vyumba uswahilini maeneo ya mijini unaweza kuwa bora zaidi kama hutaki stress. Nimejaribu wakati fulani, kidogo ni nafuu. Tafuta kiwanja Uswahilini, jenga vyumba vya kawaida kabisa,kodisha, na kila mwaka jenga vingine. Ukifikisha vyumba 20,unaweza kuishi bila hofu sana. Au ukiwa njema kidogo, jenga godown kisha kodisha. Ipo mingi, ila kwa leo tujadili hii miwili.
 

unazungumzia mtu mwenye mshahara tajwa hapo juu au???
 
Unachozungumzia hapa ni mshahara wa kijana kwenye sector binafsi. Kwa serikalini huo ni mshahara wa mtu wa midle age kwa wenge government scale zinazolipa, lakini rate hii wengi ni wale waliobakiza miaka michache kustaafu.
 
Aiseee.... nahisi hiyo breakdown inapotosha. pamoja na hayo, sioni kama kuna shida sana kama huyo kijana anaishi kwake.(amejenga..hiyo aliyoandika nyumbani..ni vitu vingine vingine..umeme maji etc,) kama ni hivi ..bado huyu kwenye jamii atakua na unafuu sana tu.
 

Nimekusoma sana mkuu

Nina eneo la ekari mbili segerea kama km moja kutoka gerezani, wazo la Godown litalipa kwa hiyo location?
 
Nimekusoma sana mkuu

Nina eneo la ekari mbili segerea kama km moja kutoka gerezani, wazo la Godown litalipa kwa hiyo location?

Nenda jiji kaangalie mipango ya baadae ya eneo lake ili ujue kama ware house itahitajika au godown la kawaida, au unaweza kuweka depot ndogo ya bidhaa kama saruji,soda na vinyavi vingine au super market.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…