SoC01 Ajira hakuna, maisha ni magumu. Nini kifanyike?

Stories of Change - 2021 Competition

Mkemia kay

Senior Member
Jan 25, 2020
125
122
Kila mwaka, vyuo vyote Tanzania vinatema kontena la Vijana wenye Diploma,Digirii na Masters zao nzuri tu. Vijana zaidi ya 200,000 wanabaki mtaani hawana kitu cha kufanya, Ajira hakuna. Mtaani huku wanakutana na waliowatangulia ambao taayari wameshapigwa na msoto wa maisha.

Fikiria, Mhitimu mwenye digirii yake, anaamka kila siku hajui ratiba zimekaaje, haoni mbele, na hata akigeuka nyuma anakuta wale “WAJOMBA” waliomwambia maliza chuo nitakupa CONNECTION, ila ata hao Wajomba nao Koneksheni zao zimeshakata kitambo. Mtaa unakuwa ni mgumu sana kihuhalisia kwa sisi graduate.

Embu fikiria tena, eti vijana wengi sasa hivi ajira yao imekua kubeti. Yani imefika kipindi ambacho mtu na elfu moja yake anatengeneza matumaini kwamba aende kubeti ashinde milioni 30 atoboe kimaisha. Je ndo uhalisia wa maisha ambayo tunatakiwa kuyaishi kweli? Maisha ya Kubeti? Nafikiria hapana.

Dada zetu wengi wamefika mbali zaidi wakaingia kwenye biashara ya kujiuza ili kupunguza ugumu wa maisha kwa sababu anaona akikutana na mwanaume usiku mmoja anapewa elfu 50 kwenda juu anaona bora kuliko kukaa tu na wengi wanajiingiza katika hii biashara tangu wakiwa vyuoni ili wapate japo pesa ya kujikimu, uhalisia maisha ya chuo ni tofauti na yale waliopo mtaani wanavyoyaona, waliopo mtaani wanaisi chuoni ni bata kwa sababu watu wanapewa pesa (boom) ni kinyume na matazamio yao. Nikipata nafasi ntaleta makala kuhusu uhalusia wa maisha ya chuo.

Kwa utafiti wangu mdogo katika jiji la dodoma nimebaini asilimia zaidi ya 30 ya madada poa ni wahitimu wa vyuo mbali mbali na wengi wao wana mtoto mmoja mpaka wawili ambao wanaitaji kuwahudumia ivo mpaka wanafikia kiwango cha kujiingiza katika hii biashara chafu ambayo ni kinyume na maadili ya kitanzania.

Kwa jinsi ninavyoujua mtaa, nina uhakika asilimia mia, wapo baadhi ya watakaosoma hii makala hawana uhakika wa kula leo, wengine hata usiku wa kuamkia leo wamekula kwa jirani. Ninasema hivi kwa sababu haya ni maisha ambayo mimi pia nayaishi, naujua msoto kwa rangi zake zote.

Baada ya maisha haya magumu nayopitia mtahani. Nilikutana na neno takatifu katika biblia, Mithali 3 5-6, linasema. “Mtumaini mwenyezi Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako. Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyoosha njia zako”.

Kiukweli nilipata nguvu ya kuendelea kupambana nakutia moyo kwamba katika kila mapambano yako usimuweke Mungu mbali maana neno la Mungu ni taa ya miguu yetu.

SASA TUNATOKAJE KATIKA HUU UGUMU WA MAISHA (MSOTO).
Kwa leo nitazungumzia njia moja nikipata nafasi ntakuwa na njia nyingine.
Tuna bahati 1 kwenye hizi kizazi chetu, haya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia yana Faida sana kwa upande wetu. Kupata fursa za kupata pesa kupitia Digital Platforms ni rahisi sana, lakini tu ukiwa na moyo na uthubutu wa kujifunza “NEW SKILLS”.

Sisi watanzania tunapitia changamoto moja sio watu wa kupenda kusoma na hatupo tayari kujifunza yani kwa utafiti niliofanya watanzania ni watu tusiojali chochote ni sawa tu. Fikiria vijana wa kitanzania tungekuwa na mwamko kama walionao vijana wenzetu wa Afrika kusini.

Yawezekana haupo katika Ajira lakini naamini kila mtu amewai kuajiriwa ata kama sio ajira Rasimi ivo anaelewa msoto uliopo katika ajira ya mtu unaweza kufa kwa madeni ndo maana naitaji kujadiliana na nyinyi ili tuone tunaweza vipi kujitoa katika kuajiriwa na kuanza kujiajiri wenyewe.

Fursa zipo nyingi ila lazima tujifunze ku-capitalise kwenye hizi Fursa zinazopatikana kwenye digital platforms. Ila kabla ya kufukuzia hizi fursa, lazima uwekeze muda wako kujifunza usiku na mchana, ujue vitu vinaenda vipi. USIKURUPUKE!

Baada ya kujifunza, lazima ujue unaweza vipi Ku-commercialise ujuzi wako ukupatie pesa kupitia digital platforms. Kuna youtube, Instagram, Twitter, Upwork, yani Freelancing websites ziko nyingi sana. Na kuna watu ambao ni wataalamu wapo na wanajitangazo wanato elimu bure unaweza kuwafatilia kwenye mitandao ya kijamii kama twiter.

Ujuzi kama Copywriting, Search Engine Optimization, Affiliate Marketing, Graphics & designing na Videography. Juzi zipo nyingi, na ukiamua kujifunza hukosi pesa. Lakini je huo utayari unao? Upo tayari kuwekeza muda, jasho na damu utoboe? Mafanikio sio kitu rahisi kijana mwenzangu.

Je, kwenye izo fursa zote hipi unaijua jiulize tofauti na kulike na kukomenti nini unakijua kweye huu ulimwengu wa teknolojia

Tutumie Digital opportunities vizuri, tufaidike nazo, tutakaa tunalilia Ajira za serikali mpaka lini? simanishi kwamba ajira sio lazima hapana, ila ebu zisiwe kipaumbele kwetu wacha zije kama baraka za Mungu.

Kaa ujitafakari, ujitafute, uelewe wapi unakosea wewe kama wewe, achana na mambo ya kulalamika kuhusu serikali, unapoteza muda wako. Maisha haya yameshakua kama SANDAKALAWE, Mwenye kupata apate, mwenye kukosa akose. Utachagua unataka nini.

"Mungu awabariki"
karibuni kwa mjadala mwenye maoni na swali
 
Cha kufanya ni kugawana mishahara na wanaolipwa milioni 12 kwa mwezi na wengineo kama hao

Serikali ihakikishe wote walosoma inawalipa kifuta jasho/machozi cha kuanzia laki moja mpaka laki mbili kila mwezi.
 
Binafsi sijaona suluhisho ulilolitoa,serikali inaowajibu mkubwa kukusanya kodi ipasavyo ili kukizi mahitaji ya wananchi wake na kwa kufanya hivyo ajira zitapatikana tu, nenda shule za sekondari unadhani walimu wanatosha? madaktari, manesi,nk zipo sehemu kibao ambazo zinaupungufu wa watumishi lkn serikali kwa uwezo mdogo wanasema hawawezi kuajiri.Na kadri serikali inavyoongeza ajira ndivyo na ajira binafsi zitaongezeka.
 
Binafsi sijaona suluhisho ulilolitoa,serikali inaowajibu mkubwa kukusanya kodi ipasavyo ili kukizi mahitaji ya wananchi wake na kwa kufanya hivyo ajira zitapatikana tu, nenda shule za sekondari unadhani walimu wanatosha? madaktari, manesi,nk zipo sehemu kibao ambazo zinaupungufu wa watumishi lkn serikali kwa uwezo mdogo wanasema hawawezi kuajiri.Na kadri serikali inavyoongeza ajira ndivyo na ajira binafsi zitaongezeka.
nashukuru kwa mchango wako lakini bado huoni kwamba hakuna serikali ambayo imefanikiwa kutoa ajira kwa wananchi wake asilimia mia, ivo basi huoni haja ya vijana sana sana graduate kuangalia namna ya kujikwamua kuliko kukaa kusubili ajira ya serikali
 
cha kufanya ni kugawana mishahara na wanaolipwa milioni 12 kwa mwezi na wengineo kama hao

Serikali ihakikishe wote walosoma inawalipa kifuta jasho/machozi cha kuanzia laki moja mpaka laki mbili kila mwezi.
ni ushauri mzuri kwa serikali lakini ni ndoto ambayo haiwezi kukamilika, kwa sababu mshahara wa mtu unalingana na ukubwa wa cheo na majukumu anayoyafanya kwa serikali husika nadhani kama unaitaji watu waliosoma wapewe posho ni serikali kuangalia namna ya kupata vyanzo vingine vya pesa na sio kukata mishahara
 
Sahihi Ndugu!
Nam kiongozi
 
nashukuru kwa mchango wako lakini bado huoni kwamba hakuna serikali ambayo imefanikiwa kutoa ajira kwa wananchi wake asilimia mia, ivo basi huoni haja ya vijana sana sana graduate kuangalia namna ya kujikwamua kuliko kukaa kusubili ajira ya serikali
Mipango mibovu ndio inapelekea kuwa hivyo unadhani nchi zilizoendelea wanamatatizo ya ajira kama sisi?
 
Back
Top Bottom