Ajenda za viongozi wa vyama vya upinzani ni nini?

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
7,115
2,000
Chama chochote cha siasa nia yake kuu ni kuingia IKULU ili kiunde Serikali kuongoza nchi. Kuongoza nchi ni kuleta maendeleo ya wananchi kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiteknolojia na kulinda/kuhifadhi mazingira (maendeleo endelevu), kwa ajili ya kizazi cha leo na kijacho.

Viongozi wa vyama vya siasa upinzani:
1) Walio bungeni wanaporomosha matusi, kususia vikao na wakiwa nje wanasema ambayo walipaswa kuyasema bungeni na wakibaki bungenu wanapinga miswada ya maendeleo, hadi bajeti.

2) Wanapinga juhudi za Serikali iliyoko madarakani katika vita ya kiuchumi km mmoja amefikia hatua ya kuita ripoti za wataalamu wa makinikia ati ni professorial rubbish, kwamba Rais aliyeunda hizo tume na kupokea ripoti yao ni rubbish, Watanzania tuliomchagua ni rubbish, vyuo na waajiri wa wajumbe wa hizo tume ni rubbish, wafanyakazi wenzao ni rubbish, ndugu, rafiki, majirani, na familia zao ni rubbish, matokeo ya hizo ripoti yatakuwa rubbish, nk.

Hivi kweli kwenye karne hii, hata za watu wa kale wa mistuni, upinzani ulikuwa wa aina hii tunao ushuhudia Tanzania!

Naamini siyo tu kwamba upinzani hauna agenda ila unaongozwa na watu wasiojitambua. Kwangu nawaona hao viongozi kama wamechanganyikiwa kutokana na spidi, uthubutu na utashi wa kisiasa wa Rais Magufuli. Wanahitaji msaada wa madaktari mabingwa wa akili, na/au waende kwenye vyuo vya mitala ya uongozi (Chuo cha Uongozi cha CCM Kigamboni) ili wapigwe msasa na kupikika kiuongozi.

Asubuhi njema, NAWASILISHA.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
24,144
2,000
Ukitaka kujua kama wapinzani nchi hii ni wasanii,angalia walivypinga bajeti,halafu kikao kijacho utawasikia pesa za barabrara sijaletewa,majosho hakuna n.k,ukimuuliza ulitegemea nini kupinga bajeti halafu upate pesa anatoa povu
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
3,908
2,000
mambo ya upinzani yatakusaidia nini? mwambie huyo jamaa yako hapo IKULU kuwa kule kibiti watu wanalala saa 12 jioni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom