Ajali ya Ndege ya Precision Air imetuvua nguo wazi wazi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Je,_Unaridhishwa_na_utendaji_wa_Idara_za_Uokoaji_na_Zimamoto_linapotokea.jpg

Wakuu kwa mara nyingine tena nitoe pole sana kwa waliopatwa na ajali ya Ndege leo huko Bukoba baada ndege ya Shirika la Precision Air kupata hitilafu wakati wa kutua na kuingia Victoria pia wale waliopoteza maisha basi Mwenyezi Mungu awarehemu na kuzipumzisha nafsi zao pema peponi.

Kusema ukweli nashindwa kuelewa ni jambo lipi sisi kama taifa tunaweza kujivunia kulifanya kwa ukamilifu, nakosa majibu jamani. Hivi uwezo wetu wa kukabili majanga uko kwa namna ipi? hakuna siku limetokea janga nchi hii vyombo byetu vikafanikiwa kudhibiti kwa 100%. Kila wakati lazima madhara makubwa yatokee.

Leo tumeshuhudia mambo ya ajabu sana kama nchi utadhani tuko miaka 40 huko, Ndege imekaa kwenye maji zaidi ya lisaa hakuna hata helicopter ya uokoaji au boti za kuvuta ndege za kisasa zilizofika eneo la tukio matokeo yake ndege inavutwa kwa kamba na wananchi, mambo ya ajabu kuwahi kutokea.

Nashindwa kuelewa serikali inajali kweli maisha ya wananchi wake? ni mpaka afe nani ndio nchi hii itashtuka kuwa tunatakiwa kuwa tayari kukabili majanga badala ya kuripoti madhara? Inakera na inaumiza sana, narejea kukumbusha matukio makubwa ya yaliyochukua maisha ya watu wetu wengi, ni watu tu hawakuwajibika ipasavyo na kusababisha maisha ya watu kupotea.

Hii nchi inahitaji mageuzi makubwa sana ya kimfumo, viongozi wetu hawajali maisha ya wananchi, wamekuwa wabinafsi na wasio wabunifu kukabiliana na matatizo.

Leo tumeonesha dunia ni kiasi gani hatuna uwezo wowote wa kujiokoa wenyewe, hatuna vifaa, hatuna wataalamu mpaka napata shida kuwaza ni kiasi gani hii nchi iko salama kiulinzi? mbona kama siku tukikumbwa na mafuriko ya mwezi mmoja watu wote tutaelea kwenye maji jamani?

Kilichoshuhudiwa kwenye tukio la uokoaji baada ya Ndege hiyo kuanguka Ziwa Victoria kimeacha maswali mengi kuliko majibu dhidi ya Serikali na Idara za Uokoaji

Miundombinu iliyotumika wakati wa uokoaji haikuwa sahihi akitolea mfano wa Ndege kuvutwa kwa kamba na wananchi, na idadi ndogo ya maafisa wakionekana wamesimama pembeni kama watazamaji

Sasa yale mazoezi ambayo vyombo vya usalama hufanya kuonesha utayari wa kukabiliana na dharula yana maana gani ikiwa hayana msaada kwenye kukabili majanga ya ndani zikiwemo ajali?

Hawa watu hawatujali jamani, hawana muda na sisi.
 
Tangu ajali ya mv bukoba tumeshindwa kua ata na boti ya uokozi katika ziwa victoria.

Imekuja ajali ya ukara kule napo bado hatukujifunza. Ziwa victoria ni ziwa kubwa africa na lenye visiwa vingi vingi ambavyo shughuli kuu ni uvuvi. Lakini hatuna ata bot za speed kikosi kazi kwa ajili ya shughuli za uokozi.

Leo ata lile jeshi tunaloona kwenye maenesho viwanjani halijakuaa na msaada wowote.

Tungeweza kuokoa abiria wote ila tukachagua kupoteza muda kwa kuvuta ndege kwa kamba
 
Back
Top Bottom