ajali ya ndege Moshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ajali ya ndege Moshi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtaalam, Feb 13, 2008.

 1. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  nimeingia kwenye blog mojawapo nimesoma kuna habari kuwa kuna ajali ya ndege wajimini sijui pasua moshi uko tz...wadau mlioko huko hebu tumuvuzishieni habari zaidi
   
 2. D

  Dotori JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndege yaangukia barabarani Moshi yahofiwa kua abiria wanne
  Na Daniel Mjema,Moshi

  ABIRIA wanne wakiwamo watatu wa kigeni, wanahofiwa kufa baada ya ndege ndogo waliyokuwa wakisafiria kuanguka katikati ya barabara mjini hapa.

  Ajali hiyo, ilitokea jana majira ya mchana katika barabara ya Viwandani karibu na sehemu ya kuhifadhi mafuta ya Kampuni ya Mafuta ya British Petroleum (BP) na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

  Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Polisi na baadhi ya wananchi walijitokeza kusaidia kisaidia kuokoa maisha ya abiria hao.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng�hoboko, alisema ndege hiyo iliruka katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi Mjini, majira ya saa 8:20 mchana na kuanguka dakika 10 baadaye kufuatia kupata hitilafu ikiwa angani.

  � Ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa abiria wanne walichukuliwa eneo la tukio wakiwa mahututi sana suala la kama wamekufa la hilo atathibitisha daktari, � alisema Ng�hoboko.

  Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Moshi, Macdonald Kulwa alisema kuwa, abiria wawili wa ndege hiyo wamethibitishwa kufa.

  Abiria hao ni Rubani wa ndege hiyo, Baraka Gilbert (36) ambaye ni Mtanzania na Hyden Rowan (26), Raia wa Kigeni. Wengine Issack Johanes (28) na Sylan Borton, wako mahututi.

  Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini hapa na Rubani wa ndege, Babu Sambeke alisema katika eneo la ajali kuwa, ndege hiyo aina ya Cessna 172 ni mali ya Kampuni ya Serengeti Balloon Safari(SBL).

  Kwa mujibu wa Sambeke ambaye ndiye aliyeiuza ndege hiyo kwa SBL na kwamba ilikuwa ikitumiwa na watu wanaoruka angani kisha kushuka kwa miavuli ilianguka baada ya kupata hitilafu.

  �Lengo la rubani lilikuwa aende futi 12,500 kutoka usawa wa bahari halafu awarushe wale jamaa wa miavuli, lakini akiwa juu akagundua matatizo katika pangaboi, �alisema Sambeke.

  Alifafanua kuwa, baada kugundua hililafu hiyo aliwasiliana na waongoza ndege katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili aweze kutua kwa dharura na kiwanja kilichokuwa karibu ni Moshi.

  Rubani baada ya kuzidiwa alijaribu kila njia kutua katika barabara ya lami, lakini kasi ya kushuka kutoka angani ilikuwa kubwa akashindwa kutimiza azma yake.

  Sambeke, alisema ndege hiyo ilianguka kwa kutanguliza kichwa kisha pangaboya kupasuka vipande.

  Taarifa zaidi zilizopatikana kutoka katika eneo hilo la ajali zilieleza kuwa, mwendesha baiskeli mmoja alijeruhiwa wakati ndege hiyo, ikianguka.

  Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaji Mussa Samizi, ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza wa kiserikali kufika eneo la tukio, alisema hakuwa na taarifa kamili juu ya ajali hiyo zaidi ya kutoa pole.

  SOURCE: MWANANCHI
   
 3. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  shukrani muzee kwa habari hizo...
   
 4. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  shukrani muzee kwa habari hizo...Mungu azilaze roho za marehemu pema peponi
   
 5. Kisura

  Kisura JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2008
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 363
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ajali hizi zitatumaliza. Mungu awarehemu!

  Huyu Babu Sambeki, (au kuna mwingine?) huyu si alikuwa anajulikana kwa Ujambazi miaka ya tisini kule Moshi/Arusha, kumbe bado yuko hai?! Naona sasa anaitwa Mfanyabiashara.
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Bob Sambeki wizi ameacha- amekuwa mtu mwema mwenye pesa nyingi sasa!
   
 7. Kisura

  Kisura JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2008
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 363
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  It's no wonder nilijiuliza, kuna mwingine, maana one I remember aliitwa "Bob", sasa nimeona Babu nikadhani pacha lake eti.

  No kidding, I guess the man has paid his dues!
   
 8. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..ngoja nami niibe halafu niwe mtu mwema!
   
 9. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..ndio hao hao tu! anyways,kama wameacha vizuri!
   
 10. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Babu Sambeke ni mwizi hatari wa magari, hajaacha hata sasa, tofauti ni kwamba tu yeye sasa anafanya coordination, hana tena kikosi anachomiliki kama zamani. Lakini bado anaheshimika miongoni mwa majambazi sugu. Pale Moshi ukiibiwa gari, kama unafahamiana na Babu Sambeke, wahi tu nyumbani kwake mlilie, atapiga simu gari yako unarudishiwa! Baada ya kutajirika sana ndipo alianza fantacy kama za michezo ya golf na mbio za magari (ana magari mengi ya mchezo huo). Kisha alinunua ndege na kujifunza urubani ambao alifaulu vizuri na amerusha ndege yake mara nyingi tu. Habari za yeye kuiuza hiyo ndege yake ndio nimeziona leo zikiambatana na hiyo ajali, lakini nadhani atakuwa amenunua nyingine. Yaani habari za huyu jamaa zinafanana na movie fulani, ukihadithiwa utadhani za kutunga, lakini ni za kweli!
   
 11. PastorPetro

  PastorPetro Senior Member

  #11
  Feb 25, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa sasa tushukuru kuwa ni ndogo ambazo zinaanguka TZ. Mungu ataunusuru siku ndege kubwa ikianguka!
   
 12. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Kazi kwelikweli . . . . Huyu ndugu si ndo yule alyekamatwa Moshi wakati wa hekaheka za Majambazi ambazo na Alex Massawe alikamatwa?

  Nasikia alikuwa na ndege na magari ya kifahari kibao pamoja na nyumba ya thamani sana. Account za Mabillion na anakopesha wadau pesa kwa kuwapa cash on spot na kisha anaandika jina kwenye note book. Unaacha shangingi lako uani kama dhamana.

  Anyway Poleni sana wafiwa wote na Mungu awatie nguvu na kuwafariji

   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2013
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,586
  Likes Received: 1,955
  Trophy Points: 280
  Ndiye huyo huyo mkuu...

  May he Rest In Peace!
   
 14. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2013
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,653
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Huyu kaka inaonekana alijiweka above the law, rules, guidelines, etc kama rubani mwenye PPL, sababu alikuwa na strong personal influence na bureaucrats, na aliweza kwa kiasi fulani ku-get away na mambo yaliyo nje ya qualifications na experience zake kama rubani bila madhara makubwa kwa muda mrefu sababu mamlaka husika inayodhibiti Wana-anga na mambo ya anga Tanzania ni dhaifu, and he could break as many rules as he wished with little if any consequences.

  Lakini, at end of the day, it all got back to bite him in the ass, and he had to lose his life like a bitch because he, of all the people, should have known what was in his store for him all this time as any serious aviator would.
   
 15. ldd

  ldd JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2013
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 794
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Si yule anayeoa kwa muda maalum madem,akimaliza mkataba anamjengea demu nyumba na wala hazai nae!!
   
 16. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2013
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,855
  Likes Received: 629
  Trophy Points: 280
  Wapumzike kwa amani marehemu wote. Msije mkasema chanzo ni magaidi. Najaribu kuwaza tu kwa sauti ila msije kuning'oa kucha na meno
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2013
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  At long last.
  Babu sambeke namsikia toka niko praimare! Enda salama baba.
   
 18. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2013
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 280
  yeye mwenyewe ni historia tangu jana kwa ajali ya ndege.
   
 19. u

  uwoya Senior Member

  #19
  Apr 14, 2013
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 167
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  pole wafiwa
   
 20. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2013
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Duuuh watu kwa KUCHIMBA
   
Loading...