Ndege yaangukia barabarani Moshi yahofiwa kua abiria wanne
Na Daniel Mjema,Moshi
ABIRIA wanne wakiwamo watatu wa kigeni, wanahofiwa kufa baada ya ndege ndogo waliyokuwa wakisafiria kuanguka katikati ya barabara mjini hapa.
Ajali hiyo, ilitokea jana majira ya mchana katika barabara ya Viwandani karibu na sehemu ya kuhifadhi mafuta ya Kampuni ya Mafuta ya British Petroleum (BP) na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Polisi na baadhi ya wananchi walijitokeza kusaidia kisaidia kuokoa maisha ya abiria hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng�hoboko, alisema ndege hiyo iliruka katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi Mjini, majira ya saa 8:20 mchana na kuanguka dakika 10 baadaye kufuatia kupata hitilafu ikiwa angani.
� Ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa abiria wanne walichukuliwa eneo la tukio wakiwa mahututi sana suala la kama wamekufa la hilo atathibitisha daktari, � alisema Ng�hoboko.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Moshi, Macdonald Kulwa alisema kuwa, abiria wawili wa ndege hiyo wamethibitishwa kufa.
Abiria hao ni Rubani wa ndege hiyo, Baraka Gilbert (36) ambaye ni Mtanzania na Hyden Rowan (26), Raia wa Kigeni. Wengine Issack Johanes (28) na Sylan Borton, wako mahututi.
Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini hapa na Rubani wa ndege, Babu Sambeke alisema katika eneo la ajali kuwa, ndege hiyo aina ya Cessna 172 ni mali ya Kampuni ya Serengeti Balloon Safari(SBL).
Kwa mujibu wa Sambeke ambaye ndiye aliyeiuza ndege hiyo kwa SBL na kwamba ilikuwa ikitumiwa na watu wanaoruka angani kisha kushuka kwa miavuli ilianguka baada ya kupata hitilafu.
�Lengo la rubani lilikuwa aende futi 12,500 kutoka usawa wa bahari halafu awarushe wale jamaa wa miavuli, lakini akiwa juu akagundua matatizo katika pangaboi, �alisema Sambeke.
Alifafanua kuwa, baada kugundua hililafu hiyo aliwasiliana na waongoza ndege katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili aweze kutua kwa dharura na kiwanja kilichokuwa karibu ni Moshi.
Rubani baada ya kuzidiwa alijaribu kila njia kutua katika barabara ya lami, lakini kasi ya kushuka kutoka angani ilikuwa kubwa akashindwa kutimiza azma yake.
Sambeke, alisema ndege hiyo ilianguka kwa kutanguliza kichwa kisha pangaboya kupasuka vipande.
Taarifa zaidi zilizopatikana kutoka katika eneo hilo la ajali zilieleza kuwa, mwendesha baiskeli mmoja alijeruhiwa wakati ndege hiyo, ikianguka.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaji Mussa Samizi, ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza wa kiserikali kufika eneo la tukio, alisema hakuwa na taarifa kamili juu ya ajali hiyo zaidi ya kutoa pole.
SOURCE: MWANANCHI

Ajali hizi zitatumaliza. Mungu awarehemu!
Huyu Babu Sambeki, (au kuna mwingine?) huyu si alikuwa anajulikana kwa Ujambazi miaka ya tisini kule Moshi/Arusha, kumbe bado yuko hai?! Naona sasa anaitwa Mfanyabiashara.
Bob Sambeki wizi ameacha- amekuwa mtu mwema mwenye pesa nyingi sasa!

It's no wonder nilijiuliza, kuna mwingine, maana one I remember aliitwa "Bob", sasa nimeona Babu nikadhani pacha lake eti.
No kidding, I guess the man has paid his dues!
Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini hapa na Rubani wa ndege, Babu Sambeke alisema katika eneo la ajali kuwa, ndege hiyo aina ya Cessna 172 ni mali ya Kampuni ya Serengeti Balloon Safari(SBL).
Kwa mujibu wa Sambeke ambaye ndiye aliyeiuza ndege hiyo kwa SBL na kwamba ilikuwa ikitumiwa na watu wanaoruka angani kisha kushuka kwa miavuli ilianguka baada ya kupata hitilafu.
SOURCE: MWANANCHI
Ndiye huyo huyo mkuu...Kazi kwelikweli . . . . Huyu ndugu si ndo yule alyekamatwa Moshi wakati wa hekaheka za Majambazi ambazo na Alex Massawe alikamatwa?
Nasikia alikuwa na ndege na magari ya kifahari kibao pamoja na nyumba ya thamani sana. Account za Mabillion na anakopesha wadau pesa kwa kuwapa cash on spot na kisha anaandika jina kwenye note book. Unaacha shangingi lako uani kama dhamana.
Anyway Poleni sana wafiwa wote na Mungu awatie nguvu na kuwafariji
Ndiye huyo huyo mkuu...
May he Rest In Peace!
Ajali hizi zitatumaliza.
Mungu awarehemu!
Huyu Babu Sambeki, (au kuna mwingine?) huyu si alikuwa anajulikana kwa
Ujambazi miaka ya tisini kule Moshi/Arusha, kumbe bado yuko hai?! Naona
sasa anaitwa Mfanyabiashara.