Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valeria Msoka amesema katika hali ya kusikitisha na kustaajabisha, baadhi ya vyombo vya habari vilisambaza picha hizo.
Amesema vyombo vya habari hivyo hususani 'Online TV' zaidi ya 15 zilichapisha na kutumia picha mbalimbali za miili ya watu waliofariki katika ajali kinyume na kanuni, miiko na maadili ya uandishi
Baadhi ya Viongozi wa vyombo vya habari walikiri makosa hayo na kuomba radhi mbele ye Kamati ya Maadili ya TCRA walipoitwa kuhojiwa
Viongozi wa Lemutuz Online TV na Global TV, vituo vilivyochapisha picha hizo, walifika mbele ya Kamati Agosti 28 kwa kushindwa kujirekebisha ndani ya muda wa Kanuni
Le Mutuz ilieleza kuwa kosa hilo lilisababishwa na uzembe wa Msimamizi wao wa maudhui ambaye hakutumia busara na weledi katika uchapishaji wa video ile
Aidha, Global TV ilisema ilichukua tahadhari kubwa ya kuziziba picha kwa kuweka kivuli lakini kulitokea tatizo la kiufundi na picha hizo zikaonekana
Baada ya utetezi wa viongozi hao Kamati ya maudhui ilivipa onyo kali chaneli hizo na kuziamuru kuomba radhi kupitia chaneli hizo kwa siku 7 mfululizo kuanzia Septemba 07