Ajali ya moto Morogoro; TCRA kuviadhibu vyombo vya habari vilivyochapisha picha zisizofaa

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,034
23,826
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valeria Msoka amesema katika hali ya kusikitisha na kustaajabisha, baadhi ya vyombo vya habari vilisambaza picha hizo.

Amesema vyombo vya habari hivyo hususani 'Online TV' zaidi ya 15 zilichapisha na kutumia picha mbalimbali za miili ya watu waliofariki katika ajali kinyume na kanuni, miiko na maadili ya uandishi

Baadhi ya Viongozi wa vyombo vya habari walikiri makosa hayo na kuomba radhi mbele ye Kamati ya Maadili ya TCRA walipoitwa kuhojiwa

Viongozi wa Lemutuz Online TV na Global TV, vituo vilivyochapisha picha hizo, walifika mbele ya Kamati Agosti 28 kwa kushindwa kujirekebisha ndani ya muda wa Kanuni

Le Mutuz ilieleza kuwa kosa hilo lilisababishwa na uzembe wa Msimamizi wao wa maudhui ambaye hakutumia busara na weledi katika uchapishaji wa video ile

Aidha, Global TV ilisema ilichukua tahadhari kubwa ya kuziziba picha kwa kuweka kivuli lakini kulitokea tatizo la kiufundi na picha hizo zikaonekana

Baada ya utetezi wa viongozi hao Kamati ya maudhui ilivipa onyo kali chaneli hizo na kuziamuru kuomba radhi kupitia chaneli hizo kwa siku 7 mfululizo kuanzia Septemba 07

Wana wazimu hao TCRA, mi nilijua wanawaambia ndugu wa marehemu wafuatilie vibari TCRA ili waendenavyo kwenye makampuni ya simu Kwa kila ndugu akaorodheshe namba alizokuwa anatumia marehemu wake ili ziangaliwe kama zina kiasi cha pesa na namna zakuwapa warithi au ndugu wa marehemu,,

Maana hizi ela huwa inasemekana zinapelekwa tcra baada ya muda Fulani kupita
 
Hiyo ni kazi ya ndugu wa marehemu bhana
 
Ujumbe wa picha ulikuwa onyo kuwatisha bodaboda waachane na tabia zao ukizingatia bodaboda wengi hawaelewi kwa kuambiwa ndio maana 95% ni failure hao jamaa wa bodaboda
 
Wasisahau pia kushirikiana na jeshi la polisi kuwakamata wale matapeli walioshindikana! badala ya ku deal na mambo mepesi mepesi tu.
 
Wote unadhani wanajua hilo??? tcra ndo watoe elimu hiyo kuwa ndugu yako akifariki fuatilia namba zake ili kuona kama kuna mpunga kwenye laini yake ndugu wazichukue ila hili kwa kuwa linafaida kwa jamii tcra haiwezi kuisemea wanataka ziendelee kukaa kwao ili wazipige kama wanavofanya mika yote
Hiyo ni kazi ya ndugu wa marehemu bhana
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valeria Msoka amesema katika hali ya kusikitisha na kustaajabisha, baadhi ya vyombo vya habari vilisambaza picha hizo.

Amesema vyombo vya habari hivyo hususani 'Online TV' zaidi ya 15 zilichapisha na kutumia picha mbalimbali za miili ya watu waliofariki katika ajali kinyume na kanuni, miiko na maadili ya uandishi

Baadhi ya Viongozi wa vyombo vya habari walikiri makosa hayo na kuomba radhi mbele ye Kamati ya Maadili ya TCRA walipoitwa kuhojiwa

Viongozi wa Lemutuz Online TV na Global TV, vituo vilivyochapisha picha hizo, walifika mbele ya Kamati Agosti 28 kwa kushindwa kujirekebisha ndani ya muda wa Kanuni

Le Mutuz ilieleza kuwa kosa hilo lilisababishwa na uzembe wa Msimamizi wao wa maudhui ambaye hakutumia busara na weledi katika uchapishaji wa video ile

Aidha, Global TV ilisema ilichukua tahadhari kubwa ya kuziziba picha kwa kuweka kivuli lakini kulitokea tatizo la kiufundi na picha hizo zikaonekana

Baada ya utetezi wa viongozi hao Kamati ya maudhui ilivipa onyo kali chaneli hizo na kuziamuru kuomba radhi kupitia chaneli hizo kwa siku 7 mfululizo kuanzia Septemba 07

Hatuangalii wapi tumejikwaa ili tusijikwae tena bali tunaangalia wapi tumeangukia na kutoa lawama kwa tulipoangukia.
 
Tuache ushabiki wa kupinga sheria na taratibu za Serikali, mbona Tv ya kimataifa Aljazeera iliyokua ya kwanza kuonyesha tukio hilo kabla hata Tv zetu hazijaonyesha haikuonyesha miili ya hao wahanga, sisi tunakwama wapi uvunjifu wa sheria?
 
Ndio vitu wanavyoviweza hawa TCRA! Vitu rahisi rahisi vya kukimbizana na ambaruti, sijui biriani... leo wamerukia kwenye vyomba vya habari.

Hawawezi kabisa mambo makubwa kama vile kuboresha huduma nafuu za data za intaneti, upatikanaji bora wa mtandao pamoja na kuwawezesha watu kutumia majukwaa ya mtandao bila urasimu wa leseni na maigizo uchwara!

TCRA ya kitanganyika hii anyways! Uswahili tu hakuna lolote!
 
Huwa najiuliza Ni lini Tcra watahusika ktk kuboresha mfumo wa GPS katika miji na kufanya kazi kwa mifumo hiyo kwenye magari yetu ?
 
Wana wazimu hao TCRA, mi nilijua wanawaambia ndugu wa marehemu wafuatilie vibari TCRA ili waendenavyo kwenye makampuni ya simu Kwa kila ndugu akaorodheshe namba alizokuwa anatumia marehemu wake ili ziangaliwe kama zina kiasi cha pesa na namna zakuwapa warithi au ndugu wa marehemu,,

Maana hizi ela huwa inasemekana zinapelekwa tcra baada ya muda Fulani kupita
 
Hawa wamiliki wa TANZANITE TV online kuna siku walirusha bila ku-edit jamaa anatumia maneno yasiyofaa lakini sijasikia wakiitwa TCRA kuhojiwa na kamati ya maudhui mtandaoni.

Labda sehemu ya mapato yake yanaimarisha chama
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom