Hii meli ikilinganishwa na meli za kubeba ndege za kivita ni ndogo sana lakini tofauti na meli hizo hii ilikuwa ni neema kubwa kwa wakulima wa Tanzania nzima.Siku ikifika kule Tanga huwa ni sherehe kwa wafanyabiashara wa bidhaa za aina zote.Mara nyingi wafanyabiashara hao huwa wameagiza mazao kutoka umbali hata Iringa na Arusha wachilia mbali Lushoto ili kuwahi soko.Mafuso pale bandarini yasiyo idadi hupanga foleni kupeleka bidhaa kuanzia Jumapili inapotia nanga mpaka Jumanne inapoondoka
Hivyo tofauti na meli za kivita hii meli ilikuwa inazalisha mamilioni ya fedha
Anayetilia shaka idadi ya abiria zaidi ya 2000 hajui maana ya meli na uwezo wake wa kubeba.
Jee umewahi kuona feri za pale Mtongwe na Likoni Mombasa zinaposhusha watu na magari?.Huwezi kuamini,utadhani wanatoka uwanja wa taifa Temeke.Basi hii meli mv spice kwa abiria ni zaidi.na abiria wenyewe wengi watoto
Meli ya MV Spice Islander muonekano wake ktk picha source: Apostolos P - IMO 8329907 - Callsign HQWZ7 - ShipSpotting.com - Ship Photos and Ship Tracker