Ajali ya Meli Zanzibar: Meli kama chombo na mazingira ya ajali

Hii meli ikilinganishwa na meli za kubeba ndege za kivita ni ndogo sana lakini tofauti na meli hizo  hii ilikuwa ni neema kubwa kwa wakulima wa Tanzania nzima.Siku ikifika kule Tanga huwa ni sherehe kwa wafanyabiashara wa bidhaa za aina zote.Mara nyingi wafanyabiashara hao huwa wameagiza mazao kutoka umbali hata Iringa na Arusha wachilia mbali Lushoto ili kuwahi soko.Mafuso pale bandarini yasiyo idadi hupanga foleni kupeleka bidhaa kuanzia Jumapili inapotia nanga mpaka Jumanne inapoondoka
Hivyo tofauti na meli za kivita hii meli ilikuwa inazalisha mamilioni ya fedha
Anayetilia shaka idadi ya abiria zaidi ya 2000 hajui maana ya meli na uwezo wake wa kubeba.
Jee umewahi kuona feri za pale Mtongwe na Likoni Mombasa zinaposhusha watu na magari?.Huwezi kuamini,utadhani wanatoka uwanja wa taifa Temeke.Basi hii meli mv spice kwa abiria ni zaidi.na abiria wenyewe wengi watoto

Meli ya MV Spice Islander muonekano wake ktk picha source: Apostolos P - IMO 8329907 - Callsign HQWZ7 - ShipSpotting.com - Ship Photos and Ship Tracker

1091610.jpg

1091612.jpg
 
Serikali serikali serikali, tatizo wabongo sie ni wabwekaji sana na wapiga majungu makubwa. Ukifika wakati wa uchaguzi tunawapa kula han hao. Sasa hebu angalieni. Bandarini meli zinajiondokea tu hakuna hata chombo cha serikali kinachosimamia na kuhakikisha meli hazibebi kuzidi uwezo wake. Ukienda kwenye basi tangu waanze kupiga kelele kuhusu milango ya dharura lkn hakuna kilichofanyika wanaangalia tu. Siku moja mv magogoni ikizama watakufa watu wote.
 
Mhh, au wanatutoa kafara nini? Maana huyu leader wetu ni rafiki mkubwa na hawa jamaa ***. Ajali za ajabu ajabu ambazo zimekaa kimakusudi tu. Gongolamboto, mbagala na hiyo meli pia. Duh! Misaada huwa haitolewi hivi hivi tu.
 
Uzembe, Meli imezama saa saba usiku, Mabaharia wakariporti bandarini muda kabla ya kuzama -- cha ajabu uokoaji ukaanza saa 12. Watanzania tunaonekanaje mbele ya macho ya dunia.

Tunarudia makosa yale yale, MV Bukoba imeanza kuzama saa 12 alfajiri - uokoaji ukaanza saa 8 mchana.
 
Mpk jana waliookolewa ni 750,maiti zimepatikana 263,na mudahuu wa saa3 asubuh meli yauokozi mv serengeti imeshusha maiti zaid ya 800 mm nipo hapa bandarini unguja hao maiti wameokotwa wakielea bado meli hawajaifikia iko ktk kinakirefu sana chini ya bahar,sasa kwamahesabu waliookolewa 750,mait zajana karibu 300 naleo zimepatikana maiti 800 sasa hapo ni hesabu 1850,serikali iache kudanganya watu.tunajionea kwa macho kila kitu hatudanganyiki.
Ni uzembe wa kutisha sana na ninakosa hamu ya kwenda visiwani.Na hii ni kwa vile mimi huwa napenda kuwa mtalii wa ndani na nimefika visiwani na kukaa pale Machomanne , Chakechake.
Lawama zinatembea utafikiri pale bandarini palikuwa a vipofu watupu!
Tujifunze sasa kuwa mlinzi namba moja wa maisha yako ni wewe mwenyewe.Mimi nilisafiri na meli kubwa hapo sehemu za Nungwi na mawimbi ya hapo ni balaa!
Nime google depth ya hapo Nungwi na kina ni mita 500 hadi 700.
Pamoja na tofauti zetu Wazenj twawapenda, na katika hili kuilaumu serikali peke yake haitoshi.
Haya tuliyoyaona ni ezembe wa kutisha kiasi cha kuweka thamani ya binadamu kuwa ya chini kabisa, kuanzia kwa serikali hadi kwa mtu binafsi.
Kwa hali iliyopo ,Mwananchi wa kawaida lazima atambue dalili za awali zinazahatarisha maisha yake.
Poleni sana wafiwa na Mungu awarehemu waliopoteza maisha.
AMEN.
 
Waziri anayehusika na usafirishaji SMZ anasubiri nini? Na nasikia anatokea CUF. Siyo ndo wakati wa ndugu zetu CUF kuonyesha tofauti yao na CCM.
Kwenye red wa KIJIUZURU MARA MOJA AU SIYO !
 
Huwa tunatoa takwimu potofu ili kulinda maslahi ya serikali iliyopo madarakani!!huu ni utumwa wa kifikra!
 
Mpk jana waliookolewa ni 750,maiti zimepatikana 263,na mudahuu wa saa3 asubuh meli yauokozi mv serengeti imeshusha maiti zaid ya 800 mm nipo hapa bandarini unguja hao maiti wameokotwa wakielea bado meli hawajaifikia iko ktk kinakirefu sana chini ya bahar,sasa kwamahesabu waliookolewa 750,mait zajana karibu 300 naleo zimepatikana maiti 800 sasa hapo ni hesabu 1850,serikali iache kudanganya watu.tunajionea kwa macho kila kitu hatudanganyiki.

Mwera, nashukuru kwa taarifa hizi endelea kutupa ukweli
leo nimesoma gazeti moja la kimarekani (Stars and Strips) hapa Afghanistan linalochapishwa na kusambazwa na kusambazwa bure kwenye kambi za Jeshi wanasema watu waliokufa ni zaidi ya 100, nahofia kuwa kuna watu wako pale kwa ajili ya kupindisha ukweli na hii ni mbaya kweli kwa taifa. Tunaficha kwa faida ya nani jamani? Si ndugu zetu watanzania wenzetu ndo wamekufa na hawatarudi kuwa hai sasa unapoficha ukweli wa kiMungu unamfaidisha nani?
Inasikitisha sana
 
Tupatie jina kabisa, mbona kuficha kuficha?!

Leo nimesoma gazeti la mwananchi wanasema Serikali ya Zanzibar haimjui mmiliki wa meli ya Spice Islanders wakati Wikipedia na sources zengine online zinasema ni mtu mmoja anaitwa Makame Hasnuu. Vile kwenye gazeti la mwananchi ilisema mmiliki wake anaitwa Salim Said Bacwash sasa sijaelewa inakuwaje gazeti limeweza kujua mmiliki wa meli ila serikali haijui mmiliki wake nani na nani mmiliki halisi wa hii meli Makame Hasnuu au Salim Said Bacwash. I THINK I SMELL A RAT SOMEWHERE!!!!
 
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
Ami! Yaelekea unapoteza kumbukumbu sometime,kwa sbb hii pigo la leo ni cha mtoto kwa ile ya Mv Bukoba. Ile kuwa kiboko kwani takwimu pamoja na serikali ya awamu ya tatu kukataa kutangaza lakini hakika ilikuwa zaidi ya watu 4,700 walipoteza maisha ila kumbuka kbs ya kwmb mapapa waliipotezea wakasema watu walikuwa 1500 tu. Yani bila mabadiliko ya haki hakika tutaendelea kuwapoteza ndg,jamaa na hata marafiki we2. Walale kwa Amani ya Bwana wale wote waliotutangulia mbele ya haki. Mapapa kweli ni janga kwa Taifa le2.

Hapo mkuu nakukatalia.Jamani MV bUKOBA kalikuwa kameli kadogo mno kubeba watu 4700!!!!!!!!!!
 
Leo nimesoma gazeti la mwananchi wanasema Serikali ya Zanzibar haimjui mmiliki wa meli ya Spice Islanders wakati Wikipedia na sources zengine online zinasema ni mtu mmoja anaitwa Makame Hasnuu. Vile kwenye gazeti la mwananchi ilisema mmiliki wake anaitwa Salim Said Bacwash sasa sijaelewa inakuwaje gazeti limeweza kujua mmiliki wa meli ila serikali haijui mmiliki wake nani na nani mmiliki halisi wa hii meli Makame Hasnuu au Salim Said Bacwash. I THINK I SMELL A RAT SOMEWHERE!!!!
CCM ndiyo walivyo.....wanafichiana siri
 
Kama leo tu zimepatikana maiti zaidi ya 800 na bado meli haijafikiwa basi tuna tatizo kubwa mno. Ni kama kawaida yao wanajaribu kuficha ukweli ili vibarua vyao viwe salama kamwe hawajali uhai wa Watanzania
 
Dear fellows back home,

1.) Has there been any information on the last time this vessel attended routine maintenance??

2.) Are there records of such maintenance and what areas are regularly checked??

3.) Who is the owner back there. Is it the same person as the one highlighted here??

4.) Was she insured?? If yes, what company arranged the insure??

5.) Are passengers covered in that insurance policy??
 
Meli inamilikiwa kwa ubia,mmojawapo wa wabia ndio hao watu katika serikali ya umoja wa kitaifa.
Pamoja na hivyo kwani jina la mmiliki lina umuhimu gani wakati uzembe uliofanyika yeye hakuwepo gatini.
Na kweli unaamini kwamba eti lazima nimtaje mie!.
Wanajuwana wenyewe wanatafuta wa kumtoa kafara tu.
 
Katika kipindi hiki tuweke siasa na ukereketwa wetu pembeni tuungane kuomboleza pamoja.Tanzania ni moja,Janga ni letu sote...... Rai kwa vyombo vya habari vizingatie uhuru wake,vitupe taarifa sahihi...nasikitika kuona CNN na BBC vinatoa details kiundani while vyakwetu havifanyi hivyo....Mungu ibariki Tanzania Mungu wape nguvu waathirika .Amen.
 
Back
Top Bottom