Ajali ya Lori na Noah yaua watano na kujeruhi wawili Dodoma

Umeona, eh? Mwendo nao haukuwa wa kawaida. Ukiwa barabarani assume watumiaji wengine wa barabara ni vichaa. Na kweli kuna vichaa - kuna walevi, wavuta bangi, madawa ya kulevya, mbuzi, ng'ombe, nk. Endesha kwa mwendo ambao kichaa/mnyama akitokea, basi unaweza simama ama usipoweza simama basi athari zitakuwa siyo kali.
R.I.P...ila hizi noah huwa ziko speed 120 hata maeneo ya speed 30..
Angekuwa hata speed 80 hapo hiyo gari isingekuwa kama can ya coca cola, iliyofinyangwa! Aisee hatari na nusu!

Everyday is Saturday............................ :cool:
 
Watu 5 wamefariki 2 kujeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Noah lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Dodoma kugongana na lori eneo la kibaigwa jijini Dodoma.

View attachment 1496248

Watu watano (5)wamepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea alfajili ya Leo katika eneo la Kibaigwa Mkoani Dodoma iliyohusisha magari mawili Toyota Noah na Lori la mizigo.

Akizungumza akiwa katika eneo la ajali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto amesema ajali hiyo imehusisha gari aina ya Noah T. 897 DCC toka Morogoro kwenda Dodoma na Lori la mizigo lenye namba T. 183 AXC lililokuwa likitoka Dodoma kuelekea Dar es saalam.

Kamanda Muroto akitoa taarifa za awali amesema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa Lori ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo aliyeingia barabarani toka upande wapili bila kuchukua tahadhari na kusababisha ajali hiyo.

" Ni kwamba huyu mwenye lori ambaye baada ya kusababisha ajali hiyo amekimbia na tunaendelea kumtafuta alitoka upande wa pili wa barabara na kuingia barabarani bila tahadhari na kusababisha ajali hii" amesema Kamanda Muroto.

Kamanda Muroto amesema majeruhi wawili wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Kongwa na miili hiyo imehifadhiwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya utambuzi.

Ametoa tahadhari kwa madereva wote kuwa makini wawapo barabarani ili kuepusha ajali Kama hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watanzania wasiona hatia.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amefika katika eneo la ajali na kuzungumza na wananchi katika eneo hilo sambamba na kuwapa pole ndugu na jamaa kwa ajali hiyo.

Ambapo amesisitiza kila mmoja katika eneo lake kuchukua tahadhari juu ya kutokea kwa ajali baya kama hizo na kuwataka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi kutekeleza maagizo ya kuondoa pakingi za magari makubwa katika sehemu zenye misongamano ya watu Kama Kibaigwa na Chalinze nyama ili kuepusha ajali Kama hizo.
Poleni sana wafiwa! Ni kweli kabisa maeneo ya Kibaigwa na Chalinze Nyama si salama sana, kwani yamefanywa ni parking ya malori wakati maeneo hayo ni finyu sana.
 
Huyo Mungu mbona hakuwasaidia ajali isitokee ?
Kim jong jr huna makosa Ila nalia sana na hawa moderators na mliki wao wanatakiwa kukufungia hata mwezi kukutia adabu lakini hawajari,I know this is the only place where we dare to talk openly,but not when it comes to GOD.max melo pitisha Sheria if your not a free Mason tell your members to stop judging OUR LIVING GOD asiyetaka aiache jamii forum na Mungu atakubariki
 
Kim jong jr huna makosa Ila nalia sana na hawa moderators na mliki wao wanatakiwa kukufungia hata mwezi kukutia adabu lakini hawajari,I know this is the only place where we dare to talk openly,but not when it comes to GOD.max melo pitisha Sheria if your not a free Mason tell your members to stop judging OUR LIVING GOD asiyetaka aiache jamii forum na Mungu atakubariki
Hahaha acha ujinga wewe Jibu kwa hoja ...
 
Ajali Haina kinga lakini sijawahi waza kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine kwa hvyo vigari(Noah). Sioni sababu ya kutumia Noah kutoka moro to dodoma coz mabasi makubwa yapo mengi sana.
 
Back
Top Bottom