Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Inasemekana jana kwenye Kisiwa cha Kelebe, Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera boti iliyokuwa inatokea Ukerewe kuelekea Bukoba ilizama na kati yao 25 waliokolewa, huku mtu mmoja akiwa hajulikani alipo.
Ikiwa imepita siku tatu bila ya mtu huyo kupatikana katika uokozi huo itachukuliwa kama amefariki.
Kwa upande mwingine chanzo kingine kimedai kuwa boti ilikuwa na watu 50 na waliookolewa ni watano pekee.
Taarifa zaidi zitakujia kadri zitakavyopatikana.
===============
UPDATES...
Alipoulizwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda amesema “Boti ilizama saa tatu asubuhi ya Julai 22, 2023, ilibeba watu 29, kati ya hao mmoja hajulikani alipo wengine wameokolewa, sababu ya kuzama ni upepo mkali na sio kweli kuwa ilibeba watu 50, Boti za huku hazina uwezo wa kubeba watu wote hao.”