Ajali ya basi la adventure: Kigoma-dar es salam muda huu

OMEGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
693
Reaction score
301
Basi la adventure kutoka Kigoma kwenda Dar limepata namba T 880 DDJ limepata ajali muda huu eneo la karibu na daraja la Mlagarasi wilayani Kasulu,ajali hiyo ni kugongana uso kwa uso na Nissan truck,hakuna fatality lakini majeruhi ni 10 ,kati yao 05 wako serious mno,muda huu wamelazwa hospitali katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.Kati ya majeruhi serious ni dreva na Konda wake ambao wote wamekatika kabisa miguu.
 
mkuu mbona pale ni peupe sana jamaa alikuwa anaovertake au ni vumbi sana au ni vipi
Poleni kwa majeruhi wote
 
MUNGU awape uponaji wa HARAKA majeruhi...Barabara zetu na uendeshaji mbovu wa madereva wetu utatumaliza wa Tanzania jamani!!!
 
Poleni majeruhi, Mwenyezi Mungu awapunguzie maumivu na kuwaponya haraka.
 
Huyo dereva na konda waliovunjika miguu ni wa basi la adventure au wa Nissan truck?, pole zao wahanga wote wa ajali hii!
 
Duuh,Poleni sana,nilisafiri na hii gari wiki mbili zilizopita kutoka KG to Dom
 
Basi la adventure kutoka Kigoma kwenda Dar limepata namba T 880 DDJ limepata ajali muda huu eneo la karibu na daraja la Mlagarasi wilayani Kasulu,ajali hiyo ni kugongana uso kwa uso na Nissan truck,hakuna fatality lakini majeruhi ni 10 ,kati yao 05 wako serious mno,muda huu wamelazwa hospitali katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.Kati ya majeruhi serious ni dreva na Konda wake ambao wote wamekatika kabisa miguu.
Hayo mabasi nayafaham, nishaapa siwezi kuyapanda labda siku nitakaponyweshwa madawa ya kulevya halafu waniingize nikiwa sijitambui.
 
Usiyapande tena ndg yangu labda kama unalako jambo moyoni la kutuachia familia yako! Ajali haina kinga lkn sio Adventure,basi linaendeshwa kama limeibwa!
 
Hii post umeipost saa 13h08 na muda huo ndio umesema kuwa ajali imetokea, nachojua basi linalotokea KG kwenda Dar linapita mitaa ya mto Malagarasi mida ya kabla ya saa nne asubuhi na la kutokea Dar kwenda KG ndilo linapita mida hiyo ya saa 13h00
 
Huyo dereva na konda waliovunjika miguu ni wa basi la adventure au wa Nissan truck?, pole zao wahanga wote wa ajali hii!

Jamani haya maswali mengine, sasa kwenye nissan truck konda anatoka wapi? It is obvious konda ni wa bus ila huyo dereva ndiye tungeuliza kupata ufafanuzi. Nina assume ni dereva wa bus.

Tiba
 
Hii post umeipost saa 13h08 na muda huo ndio umesema kuwa ajali imetokea, nachojua basi linalotokea KG kwenda Dar linapita mitaa ya mto Malagarasi mida ya kabla ya saa nne asubuhi na la kutokea Dar kwenda KG ndilo linapita mida hiyo ya saa 13h00
Wewe umekariri au umekurupuka, kipindi hiki ni cha mvua, mabasi handouts Kasulu leo saa tatu na barabara ina tope jingi hivyo malori yamekwama barabarani, ni kweli ajali imetokea, nimeshuhudia na Picha zipo nimeshindwa kuziweka hapa. Naendelea kujaribu kuziupload. Lori limetolewa nje kabisa ya barabara ila basi ndio limeharibika mbele sehemu yote. Usiongee tu kujifurahisha. Kipindi cha mvua mabasi yanafika Kibondo saa kumi jioni
 
Usiyapande tena ndg yangu labda kama unalako jambo moyoni la kutuachia familia yako! Ajali haina kinga lkn sio Adventure,basi linaendeshwa kama limeibwa!

Me nilienda kigoma mwezi wa saba kusalimia familia,kwa kweli nilikuwa naomba mungu tufike salama tu,aiseee hawa jamaa walikuwa wanafukuzana na Sumry kufika mapema sasa kutoka kasulu mpa kuingia Shinyanga koteEe vumbi tupu ila walivyokuwa wanaendesha hawa jamaaa nikasema mwenyezi mungu ni mkubwa tukifika salama,maana kwa ule mwendo kama mmepata ajali lazima vifo vitokee,also kuoga vumbi sasa ni hatari tupu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Wewe umekariri au umekurupuka, kipindi hiki ni cha mvua, mabasi handouts Kasulu leo saa tatu na barabara ina tope jingi hivyo malori yamekwama barabarani, ni kweli ajali imetokea, nimeshuhudia na Picha zipo nimeshindwa kuziweka hapa. Naendelea kujaribu kuziupload. Lori limetolewa nje kabisa ya barabara ila basi ndio limeharibika mbele sehemu yote. Usiongee tu kujifurahisha. Kipindi cha mvua mabasi yanafika Kibondo saa kumi jioni
Wala hakuna haja ya kunijibu vibaya nilikuwa naomba kujulishwa tu basi
 
Hayo mabasi nayafaham, nishaapa siwezi kuyapanda labda siku nitakaponyweshwa madawa ya kulevya halafu waniingize nikiwa sijitambui.
Kweli kabisa kinga ni bora kuliko tiba....
 
Ajali za barabarani nazo ni janga lingine kwenye hili taifa...dah
 
Back
Top Bottom