Ajali tena MASEYU-MOROGORO

Ajali tena MASEYU-MOROGORO

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
14,593
Reaction score
5,582
Wadau nipo safarini kutokea Dar kwenda Morogoro,ila kumetokea foleni ndefu sana ya MALORI na mabasi machache baada ya kutokea ajali maeneo ya maseyu,
Ajali hiyo imehusisha FUSO lililokua linatokea Moro limesheheni mkaa,na SCANIA SEMI-TRAILER lililokuwa linatokea Dar,haya malori yamegongana,na baada ya kugongana Fuso imegeukia ilikotoka yaaan moro,na cabin ya Scania imeng'oka yote,watu watatu kwenye Scania wamekufa hapohapo.
Kinachohangaikiwa sasa ni jinsi ya kuitoa hii folen ambapo magar yanayokadiriwa 3000 yamenasa kwenye foleni......
Ila inaonesha uhaba wa vifaa kama vile BREAK DOWN ndo umesababisha foleni.
Hii si ajali ya kwanza maeneo ya MASEYU,mwezi mmoja au miwili nyuma,kuna watu walibanwa na lori lililopata ajali na mmoja alikufa baada ya kushindwa kuokolewa.
=======================
2013-06-02+14.35.15.jpg
 
Nchi yetu hiyo watu wanabanwa masaaa zaidi ya matano ,wanashindwa kuokolewa
 
Nchi yetu hiyo watu wanabanwa masaaa zaidi ya matano ,wanashindwa kuokolewa

sure mdau,lakini pia ukosefu wa vifaa vya uokozi naona serikali imewategea wamilik wa magar,hii ni kazi ya ZIMA MOTO,
ALIYEPONA KWENYE AJALI NDO AMEKATIKA VIDOLE
 
Kuna ajali imetokakea usiku huu na kwa saa kadhaa sasa barabara ya Moro Dar haitembei
 
pole Tina, ajali imehusisha magari gani, we unaelekea wapi? pole sana mugu akusaidie ufike!
 
pole Tina, ajali imehusisha magari gani, we unaelekea wapi? pole sana mugu akusaidie ufike!

ajali imehusisha lori semi-trailer na fuso iliyobeba mkaa ambayo ilikua inatoka moro,fuso imegeuka ilikotoka na cabin ya scania imeng'oka,watu wa kwennye scania wamekufa wote,na folen ina magari takriban 3000 ,me ndo naingia moro usiku huu,baada ya kupita porini
 
nchi hiii bwana, yaani kila kitu bora liende, nashangaa yakianza majigambo ya vyuo, eti UDSM wanatoka kifua mbele kuwa wanaongoza kutoa watu wenye madaraka mmakubwa serikalini, mmadaraka makubwa with no meaning ......mchumi gani huyu hawezi even kuona oppotunity costs?, mambo ya kipumbavu yanaendelea yeye yupo japan, hapo kijitonyama mtu ametumbukia kisimani, inawezekanaa asipate taarifa au anajuaa kilichofanyika lkn atkaa kinya kama babu na wajukuul azi ipo hiki kipindi kilichobaki, tunalo watz!
 
kwakweli watu wanaotia huruma pale ni abiria na wale wafanyabiashara wa NYANYA WANAOWAH KARIAKOO
 
Katika magari yaliyo ktk foleni, Fuso lingine linegongana na Scania na kuua driver wa Fuso Maiti hadi sasa haijatolewa ktk Fuso. Inaning'inia na polisi hawaonekani
 
Katika magari yaliyo ktk foleni, Fuso lingine linegongana na Scania na kuua driver wa Fuso Maiti hadi sasa haijatolewa ktk Fuso. Inaning'inia na polisi hawaonekani

da tina unadhan pale polisi watakuja leo,hao wanaoongoza magar ni MADEREVA WENYEWE,BADO UPO HAPO AU UHSTOKA?SIE TUMEINGIA MORO SAA 9
 
Katika magari yaliyo ktk foleni, Fuso lingine linegongana na Scania na kuua driver wa Fuso Maiti hadi sasa haijatolewa ktk Fuso. Inaning'inia na polisi hawaonekani

Eneo gani?
 
mh poleni sana wafiwa mungu atuepushe na haya majanga ila hao madereva wa lori na wa semi trailer ni wakorofi na viburi sana barabarani.
 
poleni sana ila tutaomba waokoaji toka japan waje kutufundisha uokoaji
 
Poleni sana mliokuwa mnasafiri usiku huo!sijui wahusika ni lini watakabiliana na changamoto za hiyo barabara!
 
Hapo mahala 'MISEYU'sijui kuna shetani gani.Maana wiki tatu zilizopita kuna ghari ya Azam ilikula mzinga hapo kwenye kona ya kutelemka kuelekea morogoro!
 
Back
Top Bottom