Kassim Awadh
JF-Expert Member
- Mar 12, 2012
- 884
- 187
Imetokea asbh leo. Basi la kampuni ya RS limegongana na lori la kampuni ya Dhandho. Basi ilikuwa linatokea Dar kwenda Bukoba ambapo Lori lilikuwa linatokea Ushirombo kwenda Dar. Chanzo ni dereva wa lori kumkwepa mwendesha baiskeli ambapo alihama upande wake na kumfuata mwenye basi. Watu watatu wamekufa palepale na wengine kujeruhiwa vibaya ikiwemo kukatika miguu. Picha mojawapo anaonekana askari polisi akiwa ameshika mguu uliokatika ukiwa ndani ya kiatu na nyingine ni majeruhi aliyekatika mguu akiwa hospitali.