Ajali mkoa wa Dodoma ikihusisha basi la Osaka na lori

Ajali mkoa wa Dodoma ikihusisha basi la Osaka na lori

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,714
Hii ajali imetokea Dodoma maeneo ya Chuo cha CBE ikihusisha basi la kampuni ya Osaka na lori la Bhanji Transport.

Taarifa kamili nitawajuza hivi punde...

==========
==========

Ajali mbaya ambayo imetokea Usiku wa jana maeneo ya CBE Dodoma. Basi la Osaka Raha ambalo lilikuwa linatoka Mwanza kuelekea Dar. Chanzo cha ajali hiyo ni gari kubwa aina ya Semi-Trela lilikuwa limekata Trela lake katikati ya barabara kuu inayoelekea Dodoma Inn.

Na basi hilo inasemekana lilikuwa spidi sana na bila kujua kuwa katikati kulikuwa na trela hilo na katika jitahada za kujaribu kulikwepa liliingia kwenye mtaro na kugonga mti.

Inasemekana hakuna aliyepoteza maisha ila majeuhi ni wengi na wamekimbizwa katika hospitali ya General
..

View attachment 234553View attachment 234554
 

Attachments

  • 1426320126850.jpg
    1426320126850.jpg
    54.4 KB · Views: 2,107
  • IMG-20150314-WA0006.jpg
    IMG-20150314-WA0006.jpg
    171.7 KB · Views: 3,144
  • IMG-20150314-WA0004.jpg
    IMG-20150314-WA0004.jpg
    51.3 KB · Views: 3,090
Ajali zimezidi,siku moja ajali moja kazi tunayo
 
Kuna kitu hakiko sawa kwenye hii nchi kwa sasa
 
Kuna kitu hakiko sawa kwenye hii nchi kwa sasa

Zile damu za albino zinalia na watu ile mvua ya mawe shinyanga hujajifunza kitu kuuwa vikongwe na albino unafikiri Mungu hayupo yupo na anatenda .
 
Inasemekana hakuna aliyepoteza maisha ila majeuhi ni wengi na wamekimbizwa katika hospitali ya General..

  1. Mwendo kasi husababisha ajali, maafa na mauti, madereva fuateni viashiria vya tahadhari vinavyoongoza mwendo mwendo barabarani ikiwa ni pamoja na speed meter na mabango barabara kuonyesha speed limit.
  2. Poleni majeruhi na tunawaombea mpate nafuu haraka mrudi kwenye shughuli na familia zenu.
  3. Hospitali ya General, hiyo ni hospitali gani? Labda ni Dodoma General hospital? Sijasikia bado kama kuna hospitali inayoitwa General.
 
Mmh..hakika kuna kitu naamini hakipo sawa saa hivi katika anga la Tanzania kiroho na kimwili...let's take action brothers and sisters
 
Mwanasiasa wanakesha kwa waganga wanatambika sababu ya ajali kuwa nyingi na mauaji ya albino kurud tena
 
Ajali mbaya sana lakini hajafa hata mtu?
Tuwe makini na uandishi wetu.
Eneo la ajali ni jirani na ukumbi wa Bunge la JMT
 
Ajali mbaya sana lakini hajafa hata mtu?
Tuwe makini na uandishi wetu.
Eneo la ajali ni jirani na ukumbi wa Bunge la JMT

Hii sikuwahi kuijua aisee!hivi kumbe ajali ili iwe mbaya ni lazima kuwe na mtu aliepoteza maisha!!!
 
Kuna damu zilizo mwagika bila hatia zinaita damu nyingine. Waombaji waingie kazini usiku na mchana kwa kuiombea hii nchi yetu , Mungu aepushe huu umwagikaji wa damu kila siku.
 
Iv kama albino akiuawa, wanatafutwa waganga na kukamatwa, kwanini ajali zikitokea, madereva wote hawakamatwi?!
 
Back
Top Bottom