Ajali mkoa wa Dodoma ikihusisha basi la Osaka na lori

Ewe Mwenyezi Mungu tuhurumie, kwa kuwa wewe huna gadhabu ya dhambi tunazofanya tunaomba Rehema zako.
 
Ajali hizi watafiti wamekwisha sema 70% ni makosa ya kibinadamu (madereva wa vyombo vyote vya moto) hilo ndiyo tatizo,maana yake kama ni makosa ya kibinadamu yanaweza kupata ufumbuzi sasa nini ufumbuzi wake? tumekuwa tukishauri sana serikali hatua za kuchukua, hakuna kinachofanyika matokeo yake tunashikana uchawi!
Hizi ajali zinatokea zaidi miaka 10 si kama mwaka wa uchaguzi tuu.
Ajali Tanzania yetu chanzo kikuu ni mwendo kasi
 
Haa! kumbe ni barabara ya wanaume mwanza -dar eneo lenyewe lipo ndani ya mji speed za nini?
 
Hivi utaratibu wa ugawaji leseni za udereva Tanzania huwa ukovipi? Ninamashaka nahapo. Je rekodi za madereva wazembe huwa zinatunzwaje? Magari kabla yakutoa huduma yanakaguliwa nanani? Vidhibiti mwendo hivi bado vipo? Dereva mmoja anatakiwa aendeshe masaa mangapi ndo apumzike? Jamani kama ndo hivi tutakwisha.
 
shetani kazini..! Tuombe mwenyezi mungu aiponye nchi
 
Mmh..hakika kuna kitu naamini hakipo sawa saa hivi katika anga la Tanzania kiroho na kimwili...let's take action brothers and sisters

Mkuu hujui kama uchaguzi unakaribia??, watu wanajitolea makafara, shame on them.
 
@ mnyama k.....hili Taifa linahitaji mambo makuu mawili
1. Kuwajibika kwa kila raia kimatendo...ie..viongozi,. Idara za usalama husika, wenye vyombo, madereva, na RAIA (abiria)
2. Kiimani pia ni vyema kwa watanzania kuanzia viongozi kuacha makafara
 
Zile damu za albino zinalia na watu ile mvua ya mawe shinyanga hujajifunza kitu kuuwa vikongwe na albino unafikiri Mungu hayupo yupo na anatenda .

Aliyekwambia damu ya mtu huwa "inalia" ni nani?

Unataka kusema ile mvua ni Mungu ndiye aliyeileta?

Mafundisho kama haya ndiyo yanayofanya baadhi ya watu kubadili maamuzi na kuamini hakuna Mungu. Ni sawa na wale wanaofundisha kuwa kifo cha mwanadamu ni mapenzi ya Mungu. Yani mtu amefiwa na mama yake mzazi aliyekuwa anamtegemea kwa kila kitu, ada ya shule na mengineyo alafu unamwambia ni mapenzi ya Mungu!

Inasikitisha sana kuona kwamba katika kipindi kibaya kabisa katika maisha ya binadamu (msiba), mhusika mkuu shetani ibilisi hatajwi ila anatajwa Mungu.
 
Soma vizuri maandiko usikurupuke tofautisha kifo cha maradhi na kifo cha kuuliwa na binadamu mwenzio, ama ajali za kutengeneza bila kuvunja hayo maagano ni kazi bure,jaribu kuuwa uone kama utakuwa salama kiroho maishani mwako na kama si kwako ni kwa vizazi vinavyofuta bila kutambua na kuvunja maagano itawapa shida mpaka siku roho itakapo acha mwili.
 
Kuna kitu hakiko sawa kwenye hii nchi kwa sasa

You guessed right. Nimewaza hicho hicho. Ajali ya Arusha express jana, leo hii ya Osaka, juzi Lori kuangukia basi huko Iringa.

Mungu turehemu.
 
Soma vizuri maandiko usikurupuke tofautisha kifo cha maradhi na kifo cha kuuliwa na binadamu mwenzio, ama ajali za kutengeneza bila kuvunja hayo maagano ni kazi bure,jaribu kuuwa uone kama utakuwa salama kiroho maishani mwako na kama si kwako ni kwa vizazi vinavyofuta bila kutambua na kuvunja maagano itawapa shida mpaka siku roho itakapo acha mwili.

Taratibu mkuu, nataka kujifunza inawezekana kuna kitu sikukielewa.

Nimejitahidi kuyasoma ila sijaona sehemu inayosema kwamba damu ya mtu huwa "inalia" ndo maana nikakuuliza ili kama ipo nikasome nipate kuongeza kitu.

Ninachofahamu mimi, kifo ni kifo, kiwe cha maradhi, kiwe cha kuuliwa na binadamu mwenzako, kifo ni kifo na kifo kinasababishwa na shetani ibilisi. Mungu hapendi tufe kabisa na wale alivyotuumba haikuwa mpango wake sisi tufe.

Uwe na hakika kwamba Mungu hasababishi matatizo yanayotupata. Badala yake, anatupa tumaini pekee la utatuzi. Isaya 33:2.
 
Ntarudi ngoja nikuletee maandiko hapa uwe huru.
 
Back
Top Bottom