masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,925
- 13,256
Sasa viongozi wameanza kufa naeneo haya ya Inyala.Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia huku wengine wakijeruhiwa baada ya Lori kufeli breki na kugonga Magari madogo mawili, katika mteremko wa Inyala mkoani Mbeya.
Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi.
ITV
==============================
Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, wadaiwa kufariki dunia hii leo huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya Lori kufeli breki na kugonga magari madogo mawili, katika mteremko wa Inyala Mkoani Mbeya.
Kwa mwezi wanakufa watu 5 hadi 20.
Mwezi wa July maeneo hayo lori lililofeli breki liliua watu 20 pale Inyala crissing ya TAZARA.
Mimi niliona kwa macho.
Tumelia watu wa Mbeya juu ya barabara hii hadi tumechoka wenyewe.
Sasa viongzi wanakufa, pengine serikali itafumbua macho.