Ajali mbaya Nyololo: Basi la Newforce laua watatu!

Ajali mbaya Nyololo: Basi la Newforce laua watatu!

Hilo si ndiyo lile eneo ambalo kamanda Kamuhanda alipowaamrisha vijana wake wamlipue kwa bomu Daudi Mwangosi? R.I.P wale wote mliopoteza maisha. Amina
Hilo eneo sio zuri.R.I.Pmarehemu wote majeruhi tunawaombea mpone haraka.
 
Hii mbaya sana,poleni sana wafiwa na majeruhi MUNGU awaponye
 
Habari nilizopata hivi punde basi la new force limepata ajali na kuuwa watu watatu akiwemo na ndugu yangu r.i.p maiti wote.

Mkuu,
Basi lilitoka wapi kwenda wapi? Ajali ilitokeaje/ilitokana na nini?
 
Duh! Mbaya sana. Tarehe 24 Dec hili basi lilipata ajali Inyala, na mpaka leo hawajalitoa pale TAZAMA pipeline, leo hii tena Nyololo. Hawa wachina na wao wameingia kwenye mazindiko nini???
 
Poleni sana. Maisha ya myz hayana thamani. Hapo hakuna cha insurance wala compensation!
 
Nasikitika kusema kuwa ajali hii imesababisha kifo cha rafiki yangu, kaka yangu, ndugu yangu RODGERS BARAKA.
Tulikupenda ila mungu amekupenda zaidi.
 
Mimi pia nilipata ajali hapo hapo mlima mkali tarehe 24 december 2012 nikiwa na private car, gari iligongwa nyuma vibaya sana. Hadi wakifa watu 100+ labda ndo serikali itaona umuhimu wa kupanua barabara hapo!
 
Kuna ajali mbaya imetokea Nyololo ikilihusisha basi la Newforce likitokea mbeya kwenda Dar, watu watatu wamekufa hapohapo na wengine wamejeruhiwa. Basi liliacha njia majira ya saa nne tatu asubuhi. source nipo Nyololo

samahani picha sijaweka simu yangu haina camera natumia laptop

Sawa lakini hakuna ajali nzuri duniani
 
Nasikitika kusema kuwa ajali hii imesababisha kifo cha rafiki yangu, kaka yangu, ndugu yangu RODGERS BARAKA.
Tulikupenda ila mungu amekupenda zaidi.
Dah!pole sana aisee.R.I.P baba ivan.
 
Kazi ya Mungu haina makosa.

Wala hairekebishwi na binadamu yeyote.

Sisi tuliwapenda, lakini Mungu akawapenda zaidi.

Jina lake lihimidiwe, Bwana apewe sifa, kwa kuwaua.
 
pole sana kaka, ajali haina kinga, ila tuliobaki tukumbuke kumuomba MUNGU sababu mambo ya barabarani ni mengi, "Mkabidhi Bwana njia yako, na umtumaini naye atafanya.
Zab: 37.5
 
Back
Top Bottom