Ajali mbaya Nyololo: Basi la Newforce laua watatu!

Ajali mbaya Nyololo: Basi la Newforce laua watatu!

nkisumuno

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
208
Reaction score
72
Kuna ajali mbaya imetokea Nyololo ikilihusisha basi la Newforce likitokea mbeya kwenda Dar, watu watatu wamekufa hapohapo na wengine wamejeruhiwa. Basi liliacha njia majira ya saa nne tatu asubuhi. source nipo Nyololo

Samahani picha sijaweka simu yangu haina camera natumia laptop
WAKATI ikiwa ni siku ya nne tangu kuuanza mwaka mpya wa 2013, watu watatu wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya Mafinga wilayani Mufindi, mkoani Iringa, baada ya basi la Newforce, walilokuwa wakisafiria kutoka mkoani Mbeya kwenda Dar es salaam kuacha njia na kupinduka.

Ajali hiyo, ilitokea jana saa 4.30 asubuhi, eneo la Nyololo wilayani Mufindi katika barabara kuu ya Dar es salaam-Mbeya, ikihusisha basi la Newforce lenye namba za usajili T 465 BBY aina ya U-Tong, baada ya kushindwa kupanda mlima Nyololo.

Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda aliwataja waliokufa kuwa ni Rogers Boniface (42), mkazi wa Mbeya, Anon Mwaijande (28) mfanyabishara wa Mbeya na Witnes Minja (25) mfanyabishara wa jijini Dar es salaam.

Alisema sababu za ajali hiyo, ni mwendo kasi wa basi hilo ambalo, lilipokumbana na utelezi dereva wake alishindwa kulimudu jambo lililosababisha kuaacha njia na kupinduka.

"Bado hatujaweza kumkamata dereva wa basi hili, amekimbia japo tunaendelea kumtafuta, majeruhi wanaendelea vizuri na miili ya waliofariki imeandaliwa kwa ajili ya kuhifadhiwa hospitali ya Wilaya ya Mufindi kusubiri ndugu," alisema Kamuhanda.

Hata hivyo, alisema idadi kamili ya majeruhi na majina yao haijajulikana kutokana na harakati za kuhakikisha wanapatiwa matibabu ya haraka.

Hata hivyo, aliwataka madereva kuendesha magari ya abiria kwa umakini, ili kuepuka ajali zinazoweza kutokea kutokana na mvua ambazo zimeanza kunyesha.

Baadhi ya majeruhi waliozungumza na mtanzania, walisema kuwa mwendo kasi na uzembe wa dereva wa basi hilo ndio vilivyosababisha ajali.

"Tangu tunatoka Mbeya, basi lilikuwa likikimbia japo mvua ilikuwa ikinyesha, tulipofika Nyololo hali ikawa mbaya zaidi kwa sababu ya utelezi ajali hii ikatokea," alisema Enock Mwaibabile, mmoja wa majeruhhi.

Hata hibaadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo, walisema mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana katika eneo hilo, ulisababisha barabara hiyo kuwa na utelezi mkali.

Source: Mtanzania
 
Newforce tena? juzi moja c imegongana na fuso pale Inyala,, mabasi haya mhhhhhhhhhhhhhhhhhh!
 
R.I.P wote waloathirika
A%20S%20angry.gif
 
nasikitika sana hilo basi la new force likitokea kyela kwenda Dar kafa ndugu ya mmoja anaitwa Witness Minja R.I.P my sister.
 
Rest in Peace marehemu wote na pole kwa majeruhi wapone haraka
 
Kuna ajali mbaya imetokea Nyololo ikilihusisha basi la Newforce likitokea mbeya kwenda Dar, watu watatu wamekufa hapohapo na wengine wamejeruhiwa. Basi liliacha njia majira ya saa nne tatu asubuhi. source nipo Nyololo

samahani picha sijaweka simu yangu haina camera natumia laptop
Laptop yako haina webcam?
 
Habari nilizopata hivi punde basi la new force limepata ajali na kuuwa watu watatu akiwemo na ndugu yangu r.i.p maiti wote.
 
Inasikitisha sana, poleni sana wafiwa na majeruhi
 
Hivi kwanini wanajukwaa mnapenda sana picha hata kwenye mambo yaliyo dhahiri?

Ni siasa au kitu gani kinawaharibu ndugu watanzania?
 
Habari nilizopata hivi punde basi la new force limepata ajali na kuuwa watu watatu akiwemo na ndugu yangu r.i.p maiti wote.
Hilo si ndiyo lile eneo ambalo kamanda Kamuhanda alipowaamrisha vijana wake wamlipue kwa bomu Daudi Mwangosi? R.I.P wale wote mliopoteza maisha. Amina
 
duuuh Mungu wangu mwaka umeanza vibaya, Mungu warehemu woote, pole mleta maada kwa kufiwa na ndugu.. Mungu atuepushe na hya maafa, hungo angola na ivory cost watu wamekufa ktk sherehe za mwaka mpya, hapa jana daraja limebomka singida, kifo cha sajuki, haya leo tena ajali zimeaanza daah... Mungu TUEPUSHE NA MABAYA HAYA.
 
Back
Top Bottom