Ajali mbaya Mikumi kati ya Lori na gari ya Magazeti

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Ajali imetokea mchana huu maeneo ya Ruaha Mbuyuni ikihusisha gari ndogo pamoja na Lori.

Wenye Mamlaka watatoa taarifa kamili.

====

UPDATE;
JamiiForums imefanya mazungumzo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ALex Mukama aliyethibitisha kutokea kwa vifo 4 na majeruhi 3 waliopelekwa Hospitali ya Mikumi kwa Matibabu ambapo mmoja wao karuhusiwa.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 alfajiri baada ya gari ya Magazeti aina ya Noah iliyoparamia Lori lililokuwa limeharibika na kulingonga kwa nyuma.

Amewashauri Madereva kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani na kuendesha vyombo vyao kwa mwendo unaruhusiwa ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

ajali.jpg
 
Watanzania huwa nawashangaa hapa tu. Kweli ajali haina kinga, Ila ile kusifia mbio za magari ya magazeti huwa ni upuuzi uliopitiliza.

Kuna watu na akili timau kabisa anaenda kupanda gari za magazeti kisa zinakimbia sana na kuwahi kufika
Huu ni upuuzi, kweli wameshindwa kufunga printer kila mji mkuu ili wawe wanatuma soft copy tu halafu magazeti yanachaposhwa huko huko?! Mafuta na gharama za gari na dereva ni kiasi gani? Hayo magazeti ya thamani gani?
 
Back
Top Bottom