Ajali mbaya Kibamba - Dar

Ajali mbaya Kibamba - Dar

Natumaini Mh. Rais umeona hali hii inavyotisha. hapa si kandaar au Somalia, hapa ni maili chake kutoka Ikulu au kwenye makazi yako Lugoda. Mh Rais, natumaini kama mzazi na mwenye mapenzi na raia wako utaweza kukaa chini na baraza lako la mawaziri pamoja na watendaji wengine wa serikali yako na kufanya maamuzi mazito kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu na tukianza na hii bara bara ambayo ni kiungo kikuu cha nchi hii na nchi jirani [ umuhimu wa bandari na uchumi wa nchi]. Mh Rais, bara bara hii imepitwa na wakati na inabidi tuwekeze zaidi kwenye hii barabara na kuongeza utawala wa sheria katika watendaji wako pamoja na wananchi kwa ujumla.

RIP waliofariki. Poleni wafiwa na watanzania wote.

Shadow.
 
Maskini pole yao, majeruhi na pole kwa waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki zao!
 
so sad!! Very horrifying images. Nimeumia sana moyoni cant even take my lunch. Poleni sana wafiwa!!!
 
Dala dala lilikuwa linafanya route ya wapi na wapi, na wakati ajari inatokea lilikuwa linatoka wapi kuelekea wapi?!!!!
 
Ajali zilizo nyingi zinaepukika NA ZINAZUILIKA, na sidhani tukikaa na kuomba MUNGU atuepushe na hii kitu ni kumsingizia Mungu, Vitabu vinasema IMANI lazima iambatane na MATENDO,
KWA HIYO KAMA WATU WANA IMANI NA TUKABAKI KUOMBA MUNGU TU ATUSAIDIE KUTUEPUSHA NA AJALI BILA YA KUFANYA ACTION YOYOTE YA KUZUIA ILI JAMBO LISIJIRUDIE ITAKUWA HAINA MAANA,

HILO ENEO NI HAZARD NA SERIKALI IFANYE ACTION YA KUTATUA HILO TATIZO KWA SABABU LIKO CHINI YA UWEZO WA KIBINADAMU, KUOMBA MUNGU NI KUMSINGIZIA TU
 
Inasikitisha sana. Hawa madereva wa malori mara nyingi wanakuwa wazembe na wengine wanakuwa wamechoka mno na hata kusinzia barabarani. Pole sana kwa wafiwa na majeruhi.

Mzee Punch lorry katika hii scenario lilikuwa ndio linaanza safari so sidhani kama issue ya uchovu wa dereva inaingia hapa. Sina nia ya kumtetea dereva wa lorry kwani sikuwepo lakini hata madereva wa daladala ni wazembe wa kupindukia. Issue ya ajali ni combination of factors. Kuanzia serikali kwa maana ya ubovu wa barabara, rushwa za traffic n.k.Uzembe wa madereva ndio usiseme. Mimi ni mtumiaji sana wa barabara za Dar. Infact imefikia mahali ninasema ajali zinazotokea ni kidogo sana kama kila uzembe ungekuwa unasababisha ajali sielewi idadi ya ajali ingekuwaje.

Dar hasa madereva wa daladala are never serious barabarani. Juzi kuna mmoja ameingia main road pasipokuangalia nusura nigongangane naye. Nilionyesha kuchukia na kumkemea lakini sikuona abiria hata mmoja aliyeinua kinywa chake kumsema dereva wao. So kwa kiasi fulani huu upole wetu watz unatusababishia vifo visivyo vya lazima.
 
<TABLE cellSpacing=0 cellPadding=0 width="100%" border=0><TBODY><TR><TD align=left><TABLE height=23 cellSpacing=0 cellPadding=0 width="100%" bgColor=#dddddd border=0><TBODY><TR><TD width=606></TD><TD align=right width=139>Habari mbalimbali</TD><TD align=right width=12> </TD></TR></TBODY></TABLE></TD></TR><TR><TD bgColor=#999999>
pix.gif
</TD></TR><TR><TD class=shortnews vAlign=top align=left bgColor=#ffffff>
<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
<!--colorstart:#000066--><!--/colorstart-->Leo majira ya saa kumi na nusu alfajiri, lori lenye namba za usajili T 189 ABP na tela lake lenye namba za usajili T 192 ABP lililokuwa limebeba mafuta kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Kibaha Pwani, limepata ajali mbaya na kuliangukia basi dogo la abiria (Hiace) lenye namba za usajili T 615 AJW katika eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, na kusababisha basi hilo dogo kupondeka vibaya.

Ajali hiyo ya kutisha imesababisha vifo vya watu 7 waliokuwa ndani ya basi dogo, baada ya lori hilo kulilalia basi hilo lililokuwa likitokea Kibamba kwenda Ubungo. Akiongea na mwandishi wetu aliyefika eneo tukio, Kamanda Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga , alisema kuwa basi hilo dogo aina ya Hiace lilikuwa na abiria saba ambao wote wamefariki dunia, na kati ya maiti hizo, ni maiti mbili tu ndizo zilizoweza kutolewa hadi muda huu tena zikiwa vipandevipande.

Katika maiti hizo zilizotolewa, moja ni ya mwanamke ambae hakuweza kutambuliwa kwa wakati ule na na mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Shukuru Hussein, maarufu kama Kibwetere, mkazi wa Kibamba. Aidha Kamanda Mpinga aliongeza kuwa bado utaratibu unaendelea kwa kuwa lori lilikuwa limejaza mafuta hivyo imeleta ugumu katika utoaji hadi mzigo wote utakapoisha na kuweza kufanya utaratibu wa utoaji.

Kamanda Mpinga aliweza kumtaja dereva wa lori ambaye amekimbia mara baada ya tukio hilo kutokea kuwa ni Kudura Adam na mmiliki wa Lori hilo ametambuliwa kwa jina la Mahamudu Mohamed.

Hata hivyo baada ya ndugu wa mmiliki wa Hiace kupatikana na kudai mwenyewe yuko Mkoani Kilimanjaro, walisema kuwa mmiliki huyo anaitwa Selemani Khalfan na Hiace yake huwa inalala Ubungo Kibo maeneo ya Rombo na kumtaja Dereva wa Hiace hiyo kwa jina moja kuwa ni Seif na Kondakta wake Faraji Ismail Kalama ambao mpaka sasa bado maiti zao hazijatolewa eneo la ajali.

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
...lori likiwa limeangukia hiace ikiwa kama chapati..

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
...mwili ukiwa umenasa kwenye gari hilo

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
...waokoaji wakiangalia jinsi ya kunasua hiace lililo chini ya lori

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
...sura ya mbele ya lori hilo

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
...sura ya ajali hiyo nyuma ya lori...angalia jinsi hiace ilivyo!

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
...mwili wa mtu anayedhaniwa kuwa kondakta wa daladala hilo

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
...wana wa usalama eneo la tukio

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
...mashuhuda wa ajali

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
..mzee Hussein Mwagilo akilia kwa uchungu baada ya mwanae kufa katika ajali hiyo na kupatikana kipande cha mwili tu. mwanae alikuwa akijulikana kwa jina maarufu la Kibwetere au Shukuru Hussein

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
... ni majonzi na masikitiko!!

</TD></TR></TBODY></TABLE>
 
duh. Mungu atunusuru na haya masahibu. Naomba kuuliza: kwa nini serikali isifanye hiyo barabara kuwa 'double road'? barabara ni nyembamba na haitoi 'room' ya kuovateki na mengine yanayofanana na hayo. Nyingi ya Barabara za Tanzania zimekaa kijima jima na haziendani na kukidhi ongezeko la watu na magari.
Mpango wa Kujenga dabo rodi mpaka Mlandizi hupo zaidi ya miaka kumi! mpaka leo hupo kwenye makabrasha! inashangaza sana hakuna zaidi 40km pale hii njia ndo main exit ya Jiji la DSM na ndo inaunnganisha mikoa mingi ya TZ! but Bongo zaidi ya huijuavyo! Poleni Wahanga!
 
Mwanga wa mileleuwaangazie ua raha ya milele ee Bwanal
 
dahhh watu wanakatishwa maisha kikatili sana..nimeumia sana sana ......
 
Ni hatari!. Yote mipango ya Mungu. Tuwaombee waliofariki Mungu awasamehe dhambi zao, wapumuzike kwa Amani, Amina
 
JESUS CHRIST!....

raha ya milele uwape ee bwana....na mwanga wa milele uwaangazie!
WAPUMZIKE KWA AMANI-amina
 
Mpango wa Kujenga dabo rodi mpaka Mlandizi hupo zaidi ya miaka kumi! mpaka leo hupo kwenye makabrasha! inashangaza sana hakuna zaidi 40km pale hii njia ndo main exit ya Jiji la DSM na ndo inaunnganisha mikoa mingi ya TZ! but Bongo zaidi ya huijuavyo! Poleni Wahanga!

Matokeo yake bunge linapitisha bajeti kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya 'mkuu'. Yani kwa kweli tunasafari ndefu sana ya kutoka katika huu mzunguko wa 'ubibafsi et al'
 
Jamani hadi nimesisimka mwili. MUNGU Baba Uwarehemu marehemu hawa. Hebu semeni chanzo cha ajali hii mbaya ni nini?
 
Inasikitisha sana. Mungu azipokee roho za marehemu mahali pema Peponi, Amina
 
Back
Top Bottom