Ajali mbaya Kibamba - Dar

Ndugu wafiwa poleni sana,Ninawaomba madereva wa magari yote kuwa makini ajali nyingi hapa nchini zinasababishwa na Uzembe wa madereva,mwendo kasi na ubovu wa chombo.

Poleni sana

Elisante Yona
 
Hii daladala inaonekana kama imelaliwa aisee what a bad way to die have mercy oh lord hii ni hatari sana and very very very sad

Hivi ziligongana au hili lori lilipindika na kuiangukia daladala hiyo?
 
Poleni jamani,

tufanyeje? kuna tabia ya malori kujiona wafalme wa barabara

sijui ajali imetokeaje hasa? mazingira yalikuwaje. kuna uwezekano lori lilikuwa na matatizo? naona sehemu nzuri kabisa ya barabara hapo

Dah! machozi hayazuilikia hapa
 
duh. Mungu atunusuru na haya masahibu. Naomba kuuliza: kwa nini serikali isifanye hiyo barabara kuwa 'double road'? barabara ni nyembamba na haitoi 'room' ya kuovateki na mengine yanayofanana na hayo. Nyingi ya Barabara za Tanzania zimekaa kijima jima na haziendani na kukidhi ongezeko la watu na magari.

Pia na madreva wengi wa Tanzania hawastahili kuendesha kwa sababu hawaoni vizuri, hawana leseni, hawajui sheria za barabarani, magari mengi ni mabivu hayana hadhi ya kuwepo barabarani.

Askari wa usalama barabarani wangekuwa wanafanya kazi zao vizuri nina hakika tungepunguza sana ajali za barabarani lakini wakishapewa rushwa wanaangalia pembeni na Watanzania tunaendelea kuangamia katika barabara zetu.
 
Pia na madreva wengi wa Tanzania hawastahili kuendesha kwa sababu hawaoni vizuri, hawana leseni, hawajui sheria za barabarani, magari mengi ni mabivu hayana hadhi ya kuwepo barabarani.

Askari wa usalama barabarani wangekuwa wanafanya kazi zao vizuri nina hakika tungepunguza sana ajali za barabarani lakini wakishapewa rushwa wanaangalia pembeni na Watanzania tunaendelea kuangamia katika barabara zetu.

Mkuu BAK, hapo umenena
 
Pia na madreva wengi wa Tanzania hawastahili kuendesha kwa sababu hawaoni vizuri, hawana leseni, hawajui sheria za barabarani, magari mengi ni mabivu hayana hadhi ya kuwepo barabarani.

Askari wa usalama barabarani wangekuwa wanafanya kazi zao vizuri nina hakika tungepunguza sana ajali za barabarani lakini wakishapewa rushwa wanaangalia pembeni na Watanzania tunaendelea kuangamia katika barabara zetu.

Thursday Mar 25, 2010

03_10_fsn88y.jpg

A semi-trailer being lifted from the accident scene at Kibamba Darajani area. The semi-trailer crushed a Toyota Hiace leading to ten deaths due to failure of breaks of the truck, early this morning. (Photo by Staff Photographer)
 
Thursday Mar 25, 2010

03_10_fsn88y.jpg

A semi-trailer being lifted from the accident scene at Kibamba Darajani area. The semi-trailer crushed a Toyota Hiace leading to ten deaths due to failure of breaks of the truck, early this morning. (Photo by Staff Photographer)

jamani hivi huo mtaro hapo ungekuwa umefunikwa,hilo lori lingelalia hio hiace??mi naona lingeigonga na kuisukuma pembeni,ingawa vifo vingeweza kutokea ila sio kwa hali ya kusikitisha hivi,hawa mainjinia wetu hawaoni hatari ya hio mitaro inayoweza kumeza hata hiace??
 
Serikali inafanya nini na hili tatizo la ajali? au mpaka ndugu wa viongozi wafe kwenye ajali kama hizi ndio wataanza kushughulikia? Inasikitisha kuwa japokuwa barabara ndogo lakini sheria hazifatwi kabisa. Someone need to go to jail. Waziri wa mambo ya ndani anatakiwa ajiuzuru mpaka sasa hivi. Very sad.
 
Inasikitisha sna kwa kweli yani Tanzania hatuna tofauti na nchi yenye vita ajari hizi zinatumaliza jamni!
 
Wafiwa na watanzania wenzangu poleni!
Kwa kuongeza kama wengi walivyosema ni kuwa madereva wetu nahisi shule yao ya udereva ndiyo ndogo. Pia wengi wanakuwa hawapumziki vya kutosha, na wengine huwa wanakuwa wanaendesha malori, mabasi na hizo dalala wakiwa wamelewa, ama bangi au pombe.
Na sisi wananchi hatuwasaidii tunapokuwa tunapenda kupanda magari yanayokimbizwa kupita kiasi ati ndiyo ubabe wenyewe! Utakuta watu wamesimama pembeni ya barabara wanashangilia uendeshaji huo.

La mwisho ni kuwa je si juzi juzi tu tulikuwa na wiki ya nenda kwa usalama barabarani?, hao trafiki walielimisha vipi watumia barabara na madereva? Ninavyokumbuka ni kuwa wao walikuwa wanashinikza kuuza sticker za wiki ya usalama barabarani tu.
 
Imeandikwa na Na Lucy Lyatuu; Tarehe: 25th March 2010
HabariLeo

UKOSEFU wa breki umeelezwa kuwa ndicho chanzo cha ajali ya lori na daladala iliyosababisha vifo vya watu 11 katika eneo la Kibamba, nje kidogo ya Dar es Salaam jana.

Hadi jana maiti watano kati ya 11 waliokufa katika ajali hiyo, walikuwa wametambuliwa akiwamo mjamzito na kondakta wa daladala. HabariLeo ilishuhudia kazi ya uopoaji maiti katika ajali hiyo iliyohusisha daladala Toyota Hiace namba T 615 AJW ikitoka Kibamba kwenda Ubungo na lori la mafuta aina ya IVECO Fiat namba T 189 ABP na tela lake namba T192 ABP.

Abiria wote wa daladala walikufa papo hapo baada ya kugongwa na lori hilo na kutumbukia mtaroni na kulaliwa.

Lori inadaiwa lilikuwa na shehena ya lita 30,000 za mafuta ya taa. Lori hilo linalomilikiwa na Mohamed Mahmoud lilikuwa likiendeshwa na Kudra Adam (30) ambaye alikimbia baada ya ajali.

Hiace inamilikiwa na Seleman Khalfan Rajab. Mamia ya wakazi wa Kibaha walifika eneo la tukio kwa ajili ya kutambua ndugu zao huku baadhi wakidai kuwa ajali hiyo ilitokea saa 11 alfajiri kulingana na muda ambao ndugu zao waliondoka majumbani kuwahi shughuli zao.

Miongoni mwa waliotambuliwa ni Shukuru Hussein (27) aliyetambuliwa na baba yake mzazi, Hussein Saleh, ambaye alisema mwanawe alikuwa kondakta wa daladala lingine, na alikuwa anawahi kufuata gari lake Mbezi.

Mwingine ni Faraj Ismail Ngalamba aliyekuwa kondakta wa daladala lililopata ajali ambaye alitambuliwa na kaka yake, aliyedai kuwa asubuhi ile alimpigia simu lakini hakumpata.

Maiti mwingine aliyetambuliwa ni Abdultwaibu Twalib aliyetambuliwa na mkewe, Shani Mustafa ambaye alidai kuwa mumewe alikuwa akiwahi kazini bandarini Dar es Salaam.

Aliyetambuliwa mwingine ni Ester Paulo, aliyekuwa mjamzito na alitambuliwa na ndugu zake baada ya mwili wake kuvutwa huku tumbo likiwa limepasuka; na Zainabu Ali. Maiti wote wanasadikiwa kuwa wa Kibamba kutokana na daladala hilo kuanzia safari yake Kibamba njia panda.

Hata hivyo, kazi ya uopoaji ilionekana kuwa ngumu na kuchukua zaidi ya saa sita tangu ajali itokee kutokana na askari Polisi na kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, kufika eneo la tukio lakini bila vifaa madhubuti vya kuopolea miili hiyo.

Sambamba na uopoaji maiti, wananchi wengine mawazo yao yalielekea katika jinsi ya kujichukulia mafuta ya taa huku wakionekana na ndoo kwa ajili hiyo. Baada ya saa tano kupita, lilipofika gari la kuvuta magari mabovu aina ya Effco Crane kutoka kampuni ya BMK lililokodiwa kutoka Oysterbay likijikongoja polepole na baada ya kufika, lilisababisha barabara ya Morogoro kufungwa kwa zaidi ya saa mbili kupisha kazi ya kutenganisha magari hayo.

Tukio hilo lilivuta watu wengi wakiwamo wasafiri waliokuwa wakipita eneo hilo, ambapo kijana aliyejulikana kwa jina la Sijali alijikuta akiangua kilio kilichowashtua mashuhuda hao, baada ya kumtambua mama yake kupitia kiatu chake.

Askari walimsaidia kumpeleka katika gari lenye miili ili kumtambua mama yake zaidi, na alikiri kuwa ni yeye na kuendelea kulia. Inadaiwa mama huyo hakuwa na muda mrefu tangu ahamie Kibamba.

Baada ya kazi hiyo, maiti wawili waliotolewa mapema walipelekwa katika hospitali ya Tumbi, Kibaha na wengine hospitali za Mwananyamala na Muhimbili.

Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga, alithibitisha kuwa lori lilikuwa na lita 30,000 za mafuta ya taa na inadaiwa lilikosa breki na kulipamia daladala na kuliburuza meta kadhaa mtaroni na kulilalia.

Alisema maiti wanane waliopolewa na vipande vya mikono na viwiliwili ingawa inawezekana kuwapo zaidi, lakini hakuna aliyenusurika. Hata hivyo, alisema ipo haja ya barabara ya Morogoro hasa eneo hilo kufanyiwa marekebisho, kutokana na kuwa tishio kwa ajali.

Alikiri kuwa tatizo kubwa linalolikabili Jeshi la Polisi ni kukosa vifaa vya uokoaji kutokana na kwamba tangu walipopata taarifa, yalifika magari matatu ya kuvuta magari mabovu lakini yote yalikuwa hayana uwezo wa kulivuta lori hilo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Mutani Suleiman, alisema alipokea maiti watano kati ya tisa ambapo wanne walipelekwa Muhimbili.

Wakati huo huo, kwa niaba ya uongozi wa Chadema mkoa wa Kinondoni Kanda Maalumu ya Dar es Salaam; Mwenyekiti wa Chama hicho katika kanda hiyo, John Mnyika, ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wafiwa wa ajali hiyo.

Pia ametoa mwito kwa Serikali na vyombo vya Dola, kufanya uchunguzi wa kina kuhusu vyanzo vya ajali za mara kwa mara katika eneo la Kibamba, ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

"Ikumbukwe, kuwa Desemba 2007 ajali nyingine ilitokea Kibamba Hospitali, ikihusisha malori na kusababisha vifo vya watu saba akiwamo mjamzito na wengine 11 kujeruhiwa," alisema Mnyika.

Aprili mwaka juzi, alisema jumla ya watu 181 walipoteza maisha kwa kugongwa na magari kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2007 katika eneo kuanzia Kibamba hadi Ubungo kwenye mataa.

"Mei mwaka jana, madereva wawili walikufa baada ya magari yao kugongana uso kwa uso maeneo hayo ya Kibamba … Januari mwaka huu, watu 18 walijeruhiwa katika ajali ya gari Kibamba Darajani ambapo magari matano yaligongana kwa wakati mmoja," alisema.

 
Jamani eeh excuse my ignorance.................Designer wa hii barabara ni nani?......akina Fundi Mchiundo/Moran75/Mkuu Webby.............jamani huu mfereji vipi......yaani nina maswali mengi sanaaa...............
Vipi kuhusu safety audits ya hizi barabara zetu...........it is Sad kwa kweli........poleni sana wafiwa
 
Serikali inafanya nini na hili tatizo la ajali? au mpaka ndugu wa viongozi wafe kwenye ajali kama hizi ndio wataanza kushughulikia? Inasikitisha kuwa japokuwa barabara ndogo lakini sheria hazifatwi kabisa. Someone need to go to jail. Waziri wa mambo ya ndani anatakiwa ajiuzuru mpaka sasa hivi. Very sad.

...........kwa kuongezea wahusika kutoka Wizara ya Ujenzi inabidi wawajibike.........mi naona huu mfereji ni death trap.............yaani...........inaumiza sana........
 
Back
Top Bottom