Ajali mbaya Kibamba - Dar

Dah inasikitisha sana.
Uzembe wa dereva mmoja wapo umegharimu maisha ya watu wasio kuwa na hatia.
 
wakuu its a sad scene kwani for over four hours kuna maiti bado zimebaki kwenye gari na inasemekana hakuna aliyepona, wametoa maiti mbili tu hadi sasa... ya mwanaume na mwanamke

ila a positive note maana wanasema watu wanweza wasiwe zaidi ya kumi ndani ya hiyo daldala
 
mungu azipokee roho za marehemu na kuwatia nguvu wafiwa!
mi nimechoka kuona watu wanakufa kila siku kwa ajili zinazoweza kuzuiliwa!
hivi sisi tunajiita magreat thinkers,naamini humu ndani kuna wasomi wa aina zote na wa level zote,hivi kwa nini tusiandike japo barua ya wazi kwa wahusika tuwaeleze jinsi tunavyokereka na kuishi roho juu as if we r in a combat zone!
hasa wkt huu ambapo wanaelekea kuchaguliwa upya hebu tujaribu japo kuwaandikia barua ya wazi!
we have to try to stop this,hata tukilia haisaidii lazima kitu kifanyike jamani!
 
mungu azipokee roho za marehemu na kuwatia nguvu wafiwa!
mi nimechoka kuona watu wanakufa kila siku kwa ajili zinazoweza kuzuiliwa!
hivi sisi tunajiita magreat thinkers,naamini humu ndani kuna wasomi wa aina zote na wa level zote,hivi kwa nini tusiandike japo barua ya wazi kwa wahusika tuwaeleze jinsi tunavyokereka na kuishi roho juu as if we r in a combat zone!
hasa wkt huu ambapo wanaelekea kuchaguliwa upya hebu tujaribu japo kuwaandikia barua ya wazi!
we have to try to stop this,hata tukilia haisaidii lazima kitu kifanyike jamani!



Kamwe hawawezi kusikia maana hatuwezi kufanya lolote thats all
 
Tatizo kubwa la sehemu husika ni kuwa kuna mteremko mkali, kona kali na kidaraja chembamba sana. Hizi ajali zimekuwa zikitokea kwenye hili eneo mara kwa mara na mpaka madhehebu mbali mbali yamekuwa yakifanya ibada pale kuomba msaada wa Mungu maana inaelekea "limekuwa nje ya uwezo wa binadamu". Pamoja na hayo, wito wangu kwa serikali ni kupanua daraja hilo na barabara kwenye eneo hilo kama ilivyofanyika kwenye maeneo yenye mwinuko mkali kati ya Chalize na Moro. Itasaidia sana hiyo, endapo maroli yamezidiwa, yanapita pembeni.
Vile vile, madereva wengine wanapenda kuwa na haraka sana katika eneo hilo, tuliangalie pia hasa wale wa maroli ya mchanga na dala dala.
Ahsante.
 
Hii ni habari mbaya sana moyo wangu unazidi kunyong'onyea kwa nini mwaka huu umeanza kwa ajali nyingi na mbaya namna hii??
eeh mungu ziweke pema roho za marehemu wote Amen
 
namba moja uendeshaji wetu mitz sio Drive responsibly' ukichange gear zikakubali waala hauwazi kuna mambo ya kona emergency, nimebeba abiria, nimebeba mzigo ni mjini hapa naweza leta madhra, gari yangu may be haipo na smart breaking system! mtu akiona lami basi anakandamiza hadi mwisho! hata nimeona magari yanacruise hovyo barabara za mitaani, sisi tushamshusha dereva alikuwa anamleta kibosile wa govt mtaani, akirudi anatimua mbio kweli, one day kasababisha ajali ya mtoto mdogo, tulimshusha tukamchapa viboko!anadai eti anawahi jam ubungo kabla haijakolea, u see sababu za ajali nyngi ndo hivyo, au anawahi dem wake mahali! why wanawake wanadrive sana but ajali hizi sana hazitokei kwao? umakini! hongereni mama na dada zangu!
 
Poleni sana wafiwa.

Ajali nyingi sana zinatokana na uzembe wa madereva hasa daladala.

Wakati malamka ya kudhibiti usafirishaji ilipowapa kazi majembe Auction kazi ya kupambana na madereva wazembe na magari mabovu barabarani discepline katika sector ya usafirishaji ilikuwa imeanza kurejea. madereva wasio na lesini waliondoka barabarani, madereva wenye leseni hasa wa daladala walizingatia sheria za usalama barabarani.

Operation kama hii ingeendelea kwa muda mrefu japo ni painful kwa baadhi ya watu mwisho wa siku ingejenga mazingira ya madereva kuzingatia sheria za barabarani.

Kwa bahati mbaya sana wanasiasa wakaingilia kati na ile operation ikafa baada ya maagizo ya mkuu wa mkoa Bwana Lukuvi. Uvunjaji wa sheria baada ya agizo la lukuvi ukawa even worse.

Hivyo ajali nyingi zinaweza kuzuiwa lakini watawala wetu hawako tayari kuona sheria kali zinatekelezwa ili kuleta discepline katika sector ya usafirishaji. Nafikiri wanaambiwa na waganga wao kuwa watu wanapokufa kwa wingi is a sign of good omen for their polical carriers.

Nimeshuhudia lori la sement katika barabara ya Bagamoyo limekaa katikati ya barabara kwa siku mbili kutokana na Pancha. Hawana spare tyre wala jack. Vyombo vyote vya dola viko hapa lakini hakuna hatua iliyochukuliwa. Shame on Kikwete and his lazy GVT.

If there is a will on the side of the gvt ajali nyingi zitokanazo na uzembe zitaisha.

Wakajifunze kwa wenzetu wa Rwanda. In Rwanda any traffic offence even if is an idicator not working will attract a minimum fine of US$ 500!! Hapa fine ya shs 100,000/= iliyokuwa implemented na majembe madereva wakagona na serikali magoti yakalegea na Lukuvi anasema msiwaguse madereva wetu. kwa hiyo ajali kama kawa

If there is a will there is a way.
 
:(it is a high time now insurance policyshould now take their part,what is the role of insurance? they should become more serious and strict on what they cover.
Hivi walioathirika wataambulia chochote? au kilichokuwepo ndani hakiwi covered
 
Daaaaaaa kaka hii haijatulia, i think bad driving ndo chanzo hasa ya kipanya.Mungu azilaze roho za marehemu pema peponi na awaponye majeruhi wote.Amen
 
Majembe kuondolewa ilikua kosa sana maana walikua wanarekebisha madereva wabovu!!

Shame on LUKUVI!!!
 
kwa mujibu wa waliofanya zoezi la kutoa watu... wametoka maiti kumi... so far! no survivors... hakuna mwili timilifu kwani gari ndogo imekua kama carpert.... wale mlio muhimbili au waandishi wa habari watakowahi kufika muhimmbili waone

Nina imani hii horror scene itatumika kutuamsha na uzembe wetu!!! maiti zimeharibika vibaya sana,

I am hoping for some photos ili tuzitumie kuleta awareness ya road safety watanzania
 
humu ndo kulikuwa na mama mjamzito nae kafa ee! duh jamani weee, barabara zitatumaliza
 
1269494529_breakingnuznewwwwww.jpg



ONYO PICHA HIZI SI NZURI KABISA



Leo majira ya saa kumi na nusu alfajiri, lori lenye namba za usajili T 189 ABP na tela lake lenye namba za usajili T 192 ABP lililokuwa limebeba mafuta kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Kibaha Pwani, limepata ajali mbaya na kuliangukia basi dogo la abiria (Hiace) lenye namba za usajili T 615 AJW katika eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, na kusababisha basi hilo dogo kupondeka vibaya.

Ajali hiyo ya kutisha imesababisha vifo vya watu 7 waliokuwa ndani ya basi dogo, baada ya lori hilo kulilalia basi hilo lililokuwa likitokea Kibamba kwenda Ubungo. Akiongea na mwandishi wetu aliyefika eneo tukio, Kamanda Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga , alisema kuwa basi hilo dogo aina ya Hiace lilikuwa na abiria saba ambao wote wamefariki dunia, na kati ya maiti hizo, ni maiti mbili tu ndizo zilizoweza kutolewa hadi muda huu tena zikiwa vipandevipande.

Katika maiti hizo zilizotolewa, moja ni ya mwanamke ambae hakuweza kutambuliwa kwa wakati ule na na mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Shukuru Hussein, maarufu kama Kibwetere, mkazi wa Kibamba. Aidha Kamanda Mpinga aliongeza kuwa bado utaratibu unaendelea kwa kuwa lori lilikuwa limejaza mafuta hivyo imeleta ugumu katika utoaji hadi mzigo wote utakapoisha na kuweza kufanya utaratibu wa utoaji.

Kamanda Mpinga aliweza kumtaja dereva wa lori ambaye amekimbia mara baada ya tukio hilo kutokea kuwa ni Kudura Adam na mmiliki wa Lori hilo ametambuliwa kwa jina la Mahamudu Mohamed.

Hata hivyo baada ya ndugu wa mmiliki wa Hiace kupatikana na kudai mwenyewe yuko Mkoani Kilimanjaro, walisema kuwa mmiliki huyo anaitwa Selemani Khalfan na Hiace yake huwa inalala Ubungo Kibo maeneo ya Rombo na kumtaja Dereva wa Hiace hiyo kwa jina moja kuwa ni Seif na Kondakta wake Faraji Ismail Kalama ambao mpaka sasa bado maiti zao hazijatolewa eneo la ajali.

1269506599_1.jpg

...lori likiwa limeangukia hiace ikiwa kama chapati..

1269506599_3.jpg

...mwili ukiwa umenasa kwenye gari hilo

1269506599_4.jpg

...waokoaji wakiangalia jinsi ya kunasua hiace lililo chini ya lori

1269506805_5.jpg

...sura ya mbele ya lori hilo

1269506805_8.jpg

...sura ya ajali hiyo nyuma ya lori...angalia jinsi hiace ilivyo!

1269506805_10.jpg

...mwili wa mtu anayedhaniwa kuwa kondakta wa daladala hilo

1269506805_11.jpg

...wana wa usalama eneo la tukio

1269506805_12.jpg

...mashuhuda wa ajali

1269506805_15.jpg

..mzee Hussein Mwagilo akilia kwa uchungu baada ya mwanae kufa katika ajali hiyo na kupatikana kipande cha mwili tu. mwanae alikuwa akijulikana kwa jina maarufu la Kibwetere au Shukuru Hussein

1269506805_16.jpg

... ni majonzi na masikitiko!!
 
ya rabbi mungu wangu, wasamehe makosa yao na uwajaalie pepo.

hizi picha zinatisha ......nisingetaka kuziangalia mara mbili
 
Back
Top Bottom