AJALI: Basi la UDA laigonga treni eneo la Gerezani - Kariakoo, Dar

Kuna shida kubwa sana hasa maeneo ambapo treni linakatisha. Juzi kidogo niiache dunia kwa sababu ya uzembe wa dereva wa daladala.

Tulikuwa Karume pale reli inapokatisha. Dereva kakimbiza gari ile anawahi foleni na taa za makutano ya Pugu na Kawawa road.

Kabla hatujafika relini kibendera kanyoosha kibendera sijui dereva hakumuona au alimpuuza. Ile tunafika kwenye reli gari ikawa inacheza tu kucheki kushoto kwangu kichwa cha treni kinakuja kasi balaa na kelele za honi.

Nilipokiona nguvu ziliisha maana abiria wote tukawa tushachanganyikiwa hatujui la kufanya. Kama muujiza ila kichwa kimebakiza mita chache kama tano basi likafanikiwa kutoka pale. Sikuamini maana kichwa cha treni kilipita nyuma yangu hata siamini kimepita vipi. Naamini kama tungegongwa siku ile wengi wangefariki.

Nashauri trafic watafute utaratibu mzuri pale maana kuna maeneo yana shida sana hasa pale Karume na Buguruni. Kuna siku itatokea ajali kubwa sana na kulihuzunisha taifa.

Mungu aweke roho za marehemu mahala pema peponi. Na awajalie majeruhi wepesi na kuwaponya majeraha.
Pole sana mkuu zidisha maombi kwa muumba kwa kukuokoa na janga ilo aisee
 
Pole kwa wote waliopoteza ndugu zao ktk ajali hii.. Nilikuwa aneo la tukio lkn pia nielekeze lawama kwa wafanyakazi wa TRL coz sehemu iliyotokea ajali kuna geti na zime wekwa kwa ajili ya kufunga barabara pindi treni inapopita sasa wahusika wanao tabu gani kuzishusha wakati treni inapita
 
poleni sana mliopoteza ndugu na jamaa zenu katika ajali hiyo in shaa allah allah (s.w) awape subira katika kipindi hiki kigumu.
 
Inauma Sana uzembe wa mtu mmoja unapogharimu maisha ya wengi, nimeiona mazingira ya ajali ilipotokea hadi saa hizi sina amani kabisa. Poleni majeruhi Na wafiwa wote!
 
Back
Top Bottom