Ajali zimezidi katika eneo la Zebra, Kimara Suka, TANROADS tunaomba tuwekewe mataa ya kuvukia

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Anaandika Honest Theobald Mtalo kupitia Ukurasa wake wa X

"Tukio lakusikitisha Kimara Suka Eneo la kivuko cha waenda kwa miguu TANROADS tunaomba mataa
ya kuvukia watu eneo hili. Kati ya tarehe 24-27/12/2023 zimetokea ajali sita tena ni eneo la kivuko cha waendakwa miguu bado za miezi.

TANPOL tunaomba pia msimamie sheria za barabarani madereva wakiona kivuko cha waenda kwa miguu ndio kwanza wanaongeza speed badala ya kusimama watu wanaovuka wavuke.

Mtu anagongwa kwenye eneo ambalo ni salama kwake kuvuka, Zebra za Dar sio salama, TANPOL tunaomba mfuatilie hili.

Ajali ni mbaya sana.

IMG_8875.jpg
 
Namkumbuka dada Nancy aligongwa hapo kama miezi tatu iliyopita, RIP, ila Tanroads wakubali hii barabara imejengwa bila usanifu WA kuzingatia watumiaji wengine, hata taa hazitasaidia sana, Kuna kitu kinaitwa refugee Island, hiki kitu ni muhimu sana watenge Kwa lane mbili mbili na sehemu ya kupumzika kati kati waache kudharau utaalamu huku watu wanateketea
 
Naishi hapo juu upande wa pili. Naweza kusema hii ni moja ya sehemu hatari zaidi kwa watembea kwa miguu jijini Dar es Salaam. Sasa kama mchana inakuwa hivi, Je, Usiku? huwa sitamani kuvuka usiki hapo. Mbaya zaidi hamna taa za barabarani.
Juzi nimepita hapo na rafiki yangu nikamwambia miezi miwili iliyopita kuna mdada aligongwa hapo night.

Mamlaka husika zipo kimya zinaona kila kitu sawa.

Vijana wangu wakiwa wanatoka mjini kama siku hiyo wamepanda daladala huwa namwazo sana kama watavuka salama eneo hilo hasa nyakati za usiku.
 
na wewe unapovuka usivuke kama zebra angalia usalama wako kwanza …

yaani mtu unakuta anavuka kwa maringo eti kisa yuko kwenye zebra anaona kabisa chuma imeiva ila yeye anajishebedua barabarani.
 
Yan hii barabara ni janga. Sijui CCM na serikali yake huwa wanawaza nn kuhusu maisha ya watanzania kwakweli. Thika superhighway ni almost sawa na hii barabara cha ajabu huku vituko.
 
Namkumbuka dada Nancy aligongwa hapo kama miezi tatu iliyopita, RIP, ila Tanroads wakubali hii barabara imejengwa bila usanifu WA kuzingatia watumiaji wengine, hata taa hazitasaidia sana, Kuna kitu kinaitwa refugee Island, hiki kitu ni muhimu sana watenge Kwa lane mbili mbili na sehemu ya kupumzika kati kati waache kudharau utaalamu huku watu wanateketea
Highway na matuta wapi na wapi? Waweke kivuko cha juu kama mbezi mwisho na kimara
 
Highway na matuta wapi na wapi? Waweke kivuko cha juu kama mbezi mwisho na kimara
Exactly sio vivuko vya waenda kwa miguu hadi vivuko vya kupita magari. Eneo kama hapo temboni, suka waweke daraja la juu kupunguza kusimama ovyo ambako mara chache kunazingatiwa na madereva wengi hawasimami kuruhusu gari na wengine wa pande tofauti kupita
 
Highway na matuta wapi na wapi? Waweke kivuko cha juu kama mbezi mwisho na kimara
Ni kweli unachosema.
Barabara hiyo ilikosewa tangu hatua za awali kabisa za Designing. Wahandisi waliofanya Feasibility Study ya hiyo Barabara walipaswa kupendekeza Ujenzi wa Vivuko vya Watembea kwa Miguu aidha kwa kujenga Madaraja ya Chini ya ardhi (Underpass) au Madaraja ya Juu (Bypass) ili watu wasiingiliane na vyombo vya usafiri kama magari au pikipiki.
Ujenzi wa Madaraja ya Chini ya ardhi ( Underpass) au Madaraja ya juu ( Bypass) ndio suluhisho la kudumu kwenye kudhibiti tatizo hili la ajali za mara kwa mara, madaraja hayo yanatakiwa kujengwa kila baada ya interval ya umbali fulani e.g. Mita 300 au mita 500.
 
Anaandika Honest Theobald Mtalo kupitia Ukurasa wake wa X

"Tukio lakusikitisha Kimara Suka Eneo la kivuko cha waenda kwa miguu TANROADS tunaomba mataa
ya kuvukia watu eneo hili. Kati ya tarehe 24-27/12/2023 zimetokea ajali sita tena ni eneo la kivuko cha waendakwa miguu bado za miezi.

TANPOL tunaomba pia msimamie sheria za barabarani madereva wakiona kivuko cha waenda kwa miguu ndio kwanza wanaongeza speed badala ya kusimama watu wanaovuka wavuke.

Mtu anagongwa kwenye eneo ambalo ni salama kwake kuvuka, Zebra za Dar sio salama, TANPOL tunaomba mfuatilie hili.

Ajali ni mbaya sana.

View attachment 2854543
liwekwe tuta mbuzi haruki na alama za tahadhari
 
Highway na matuta wapi na wapi? Waweke kivuko cha juu kama mbezi mwisho na kimara
Sijasema matuta ndugu, nimesema "refugee Island " hii maana yake barabara ni pana sana!! Watu wanagongwa hapo stop over, namaanisha waweke split ya barabara kuwa njia mbili mbili kwenye vivuko, anavuka Lane 2 na kutulia ili aendelee kuvuka!! Tanroads wanajua sana ila wanajitoa ufahamu
 
Nilishuhudia mtu akigongwa live mbele yangu hapo kwenye zebra sitasahau lile tukio.

Serikali ifanye namna irekebishe hilo eneo, hapo na Temboni hapako salama kabisa.
 
Hapo suka mbele kidogo kuna taa.

Temboni pia kuna taa.

Zebra crossing ipo temboni suka na hapo kwenye mataa suka na temboni.

Nachoona hapo ni uzembe wa madereva tu na pia uwepo wa kituo bubu cha bajaji na bodaboda.

Nimezipata pia taarifa za ajali kama tatu maeneo hayo kwa siku mbili hizi.
 
Sijasema matuta ndugu, nimesema "refugee Island " hii maana yake barabara ni pana sana!! Watu wanagongwa hapo stop over, namaanisha waweke split ya barabara kuwa njia mbili mbili kwenye vivuko, anavuka Lane 2 na kutulia ili aendelee kuvuka!! Tanroads wanajua sana ila wanajitoa ufahamu
Hii siyo suluhisho sahihi.
Suluhisho sahihi na lililo la kudumu ni kujenga vivuko vya madaraja ya chini ya ardhi (underpass) au madaraja ya juu (bypass) kila baada ya interval ya umbali fulani.
 
Inakubidi uwe na timing kali kuyapigia hesabu magari 4 ya hawa madereva wetu wengi wao wasiojali waenda kw miguu.

Madereva wa daladala na matoli /gari kubwa huonekana wako rafu sana road ila ni moja ya watu wanaoheshimu mno zebra, wakiona mwanafunzi hata mmoja wengi wao husimama avuke.

Shida ni hizi gari ndogo na bodaboda, hawa watu zebra huwa hawaioni kabisa, usitegemee gari ndogo au bodaboda ama bajaji isimame kwenye zebra wewe uvuke, utasombwa aloo.
 
Back
Top Bottom