AJALI: Basi la Princess Muro lapata ajali maeneo ya Kimara, Dar

AJALI: Basi la Princess Muro lapata ajali maeneo ya Kimara, Dar

gari imekatiwa comprehensive insurance bosi hana mawazo hapo alipo .
 
Alishaagiza mabasi mapya? maana kuna wakati mabasi yake yalifungiwa au ilikuwa mazingaombwe ya serikali ya chama chetu?hahahaaa!!!!!
 
Serikali iliyopo madarakani ni ya tiketi ya chama kipi?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?


Unaongelea tiketi gani??

We unaona izo barabara au vichochoro tembea uone barabara
 
Ahsante kwa taarifa ila umekosea, sio AJARI ni AJALI. Hivi hili tatizo la kuchanganya herufi za R na L halina tiba?
Na herufi A na H. Tena na hawa waimbaji wa bongo fleva ndo wanatumia vibaya hizo herufi. Poleni wahanga wa ajali
 
Upo sahihi kabisa mkuu inavyosemekana jamaa alikuwa mwendo tena kwenye njia ya mabasi yaendayo kasi.sasa ikatokea mbele akachomekewa akapiga mahesabu ya haraka kushoto magari na watu kulia hivo hivo magari akaona bora aisokomeze mule ndani.na ukitaka kujua alikuwa anajua anachokifanya alikuwa kashaandaa mazingira so wakati anaisokomeza yeye dereva akarudi faster kwa abiria akaacha gari inaingia yenyewe.ukiangalia hiyo gari pale kwa dereva pameharibika vibaya sana na yeye hajaumia kwa vile alishakuwa katoka kwenye usukani.BASI LILIKUWA NA ABIRIA WACHACHE ALIYOWAZOA NJIANI BAADA YA WALE ALIOKUWA NAO KUFAULISHWA.so hao abiria ilikuwa ni deal ya konda na dereva.kwa vile tajiri alikuwa anajua gari lake bovu so linakuja bila abiria baada ya kufaurishwa wale wengine.hii nimetoa kwenye group la nyumban kimara na mashuhuda wa ajali.

You have said very well and at least ina make sense sasa on the possible causes
 
image.jpeg Kikao cha viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na wadau wa mafuta kujadili fursa za uwekezaji zitakazotokana na mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kupitia Kagera hadi bandari ya Tanga. Kikao hicho kimefanyika Leo Tarehe 28/3/2016 Wizarani. Hapa kazi tu
 
WAZIRI WA KENYA NA KATIBU MKUU WAKE WAZUILIWA WAKITAKA KUINGIA AIRPORT YA TANGA BILA KIBALI

Kama mlisia Jana Wakenya wanekamatwa Tanga Airport wakitaka kwenda kukagua Bandari ya Tanga, Kwa kudandia msafara wa Waziri wa Uganda. Habari tulizopokea ni kwamba, Waziri wa Uganda aliomba kibali Cha kuja na Helikopta Moja na msafara wake, baada ya kupewa kibali na kuruhusiwa kuingia Tanzania, hali ilibadilika baada ya wataalam wa Tanzania Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Mkuu wa Mkoa wa Tanga kushangazwa na ujio wa Helikopta nyingine 3 zikiwa zimewabeba Waziri wa Kenya, Katibu Mkuu wake na wataalam wao. Kilichoshangazwa ni kwamba Ujumbe wa Kenya ulikuwa mkubwa karibu Mara 2 ya Waganda ambao Ndio walioruhusiwa kuingia nchini. Baada ya wana Usalama kuiona Hilo waliamua kuchukua hatua za haraka kuwazuia Wakenya wasiingie na kusubiri Airport hadi Waziri wa Uganda alupomaluza ziara yake Bandari ya Tanga na wakaruhusiwa Kurudi kwao Kenya. Watanzania tuwe macho, Kwa nini hawa Wakenya waje kukagua Miundombinu yetu wakati ni washindani wetu kwenye Mradi huu wa Bomba? Watanzania tuwe Makini sana na hawa wenzetu tunaweza kuingia kwenye mtego wa Wakenya, Kwa Kuwa mwenye maamuzi ya Mradi huu upite wapi ni Uganda, ushauri wangu Uganda waende Kenya na Tanzania wenyewe na wataamua wao, kukagua ili kupata uwezo wa Bandari husika na vivutio vya nchi husika. Tukiruhusu Wakenya kuja huku Kama walivyofanya Tanga watataka kujua hata vivutio ambavyo tunaweza kuwapatia Uganda na kushusha Vya kwao ili kuongeza ushindani.

Watanzania wenzangu sioni sababu za msingi za Wakenya kuja kutembelea Bandari yetu Kwa Kuwa tunashindana kupata Mradi huu. Kama kuna Mtanzania atafanya Hilo kosa na kuruhusu hili wanaweza kuja na hoja ya kutaka kupita maeneo yetu ambayo Bomba litapita, na wanaweza kutumia hii Kama kigezo cha kuongea na wanganda kutukandamiza.

Kwa Kuwa tupo kwenye mapambano, Rais wetu JPM Sasa muda umefika wa yeye kwenda Nje ya nchi, mwenzake Uhuru Kenyata wa Kenya anakwenda Uganda kila kukicha kuhakikisha anabadilisha mawazo ya Uganda. Sasa Kama sisi Rais wetu kagoma kwenda Nje ya nchi, wataalam na Viongozi wengine nao hawatoki hadi kibali je tutaweza kwenda Kwa kasi ya Kenya? Naawambia kama Rais wetu hata toka Mradi huu tusahau kuupata na tutajilaumu. Tunajua Juhudi zinazofanywa na Mhe. Muhongo tangu Marais wetu (TZA na UG) watoe maamuzi ya Mradi kupita Tanzania 1/3/2016 Jijini Arusha, na baadae kufuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu wa UG na TZA 16/3/2016 Jijini Arusha na kusainiwa Kwa makubaliano ya mpangokazi wa Mradi Kati ya Waziri Muhongo wa TZA na mama Irene wa UG 17/3/2016. Makubaliano hayo yalileta mshtuko Kwa Serikali ya Kenya na Kulazimu Rais wa Kenya kufanya ziara ya kushtukiza kwenda kumuona Rais wa Uganda wiki Moja baada ya kusainiwa Kwa malubaliano hayo. Licha ya Rais huyo kwenda Uganda hawakupewa jibu la kuridhisha kwani kigezo Cha Usalama kimekuwa kikwazo kikubwa Kwa Uganda kupitisha Bomba nchini humo. Baada ya kukwama katika hatua hiyo, Wakenya Wamepanga kwenda tena Uganda kuendeleza majadiliano, na Ndio maana wametaka kuja Bandari ya Tanga kuchunguza ili wakikutana tena wapeleke taarifa za Uongo Kuwa Bandari yetu sio salama, tunawashukuru wanausalama wetu Kwa Kuwa Makini na kuzuia hilo. Tuongeze mshikamano, tumuunge mkono Waziri Muhongo Kwa kusimamia sekta hii Kwa karibu, ongeza kasi zaidi na Kama utaweza kaweke Kambi Uganda, Wakenya wakienda wanakuta Mzee upo huko unakula mazoezi ya kuchukua Mradi.
 
image.jpeg
Kikao cha wadau wa Nishati na Madini kujadili Utekelezaji wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga Tanzania. Kazi ya Magufuli na Prof. Muhongo. Chapeni kazi kutuvusha hapa tulipo
 
Back
Top Bottom