Ajabu: Hali tete kanisa la Sinza Christian Centre

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
e71115bb-f2c6-472d-b74f-06b17d93e685.jpg

Mmiliki wa jengo anasema hajalipwa kodi miaka 19.

Sinza Christian Centre walikuwa wanadaiwa zaidi ya sh mil 100 sasa walitakiwa lipa tangu mwaka 2004 kwa mujibu wa Mwenye nyumba. Amesema ameshinda kesi ndo mana wale wametolewa pale.

Sinza Christian Centre wanasema eti Mungu aliwaonesha pale so hawalipi kodi.

Aliyefanya kazi ya kutoa nje ni dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua kutokana na kile kilichoelezwa kuwa wanadaiwa TZS milioni 100. Aliyekuwa kiongozi wa kanisa hilo anadaiwa kulitumia eneo hilo kinyume na makabuliano na kushindwa kulipa deni hilo.

9.JPG

6.JPG

11.JPG

15.JPG

19.JPG

20.JPG

21.JPG

3.JPG

Kushoto kwa mbali ni Mke wa Mmiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya kuendelea kutoa vitu.

Stay tuned..
 
nimepita hapo nimekuta viti na maspika yametolewa nje nikajua labda ni mnada kumbe ni habari ya kodi duh kweli sadaka zimekuwa adimu siku sizi
 
Mbwembwe zote zile kumbe walikuwa wamepanga..mimi nilijua ni eneo lao..sasa sadaka zilikuwa zinakwenda wapi?
 
Hapo kuna mgogoro mkubwa Wa umiliki Wa jengo hilo inasemekana Mzee aliokoka ktk hiyo huduma akawapa hapo wafanyie ibada then akapatwa na maradhi Mara hao jamaa wakasema ni kwao mambo km hayo.....
 
Kwa hiyo waumini wana sali wapi?halafu Hugo mchungaji miaka 19 sadaka anatia ndani tuu!!!
 
Busara itumike kutatua tatizo, kwani inaweza sababisha imani za waumini kurudi nyuma sababu ya hali hiyo.
 
Hapo kuna mgogoro mkubwa Wa umiliki Wa jengo hilo inasemekana Mzee aliokoka ktk hiyo huduma akawapa hapo wafanyie ibada then akapatwa na maradhi Mara hao jamaa wakasema ni kwao mambo km hayo.....
Hivi huyo Mzee wa hilo eneo bado yupo kweli?maana kitambo sana
 
Hapo kuna mgogoro mkubwa Wa umiliki Wa jengo hilo inasemekana Mzee aliokoka ktk hiyo huduma akawapa hapo wafanyie ibada then akapatwa na maradhi Mara hao jamaa wakasema ni kwao mambo km hayo.....
Au huyo mzee sasa hivi karudi nyuma kiimani maana mtu unaweza kupata matatizo kama maradhi yakakutesa hadi ukapoteza imani yako kwa Mungu. Na baada ya kurudi nyuma pengine ameamua kuchafua hali ya hewa kanisani kwa kudai kodi hadi na ya miaka ya nyuma alipokuwa katoa eneo waumini kusali bure.
 
Back
Top Bottom