Airtel wameshazingua tena! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Airtel wameshazingua tena!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Uswe, Sep 26, 2012.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa muda mrefu nimekua nikitumia airtel kwa internet, 2500 unapata mb 400, kuna kipindi walipandisha hizi bei zao na wananchi wakaamua kuwagomea, wengi tukasema bora tuka-banane kwenye kila ki-beetle kuliko kujiachia kwenye basi kubwa lakini lenye migharama isiyo na maana (wakati ule tangazo la airtel kuonesha watu wanahama kwenye ki-beetle cha tigo lilikua maarufu sana), Baada ya kugundua wanapoteza biashara Airtel walisitisha ule mpango wao wa kutaka kutengeneza BONGE LA FAIDA!

  Sasa wamerudi kulele, wamepandisha tena bei.

  wakati tulitegemea kuja kwa fiber kungekua mkombozi wa mawasiliano tz hali ni tofauti, gharama ya mawasiliano bado ni juu, kupiga simu au kupata internet bado ni anasa, mawasiliano ni kiungo muhimu kuelekea maendeleo ya nchi na uchumi.

  Wito: labda kama tulivyofanya wakati ule, tuachane na airtel ili wapati nafasi ya kujivua gamba kwanza
   
Loading...