Airtel wameniibia leo

Airtel wameniibia leo

Somi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2009
Posts
3,955
Reaction score
4,899
Kwa wale tunaotumia simu na mitandao kampuni za simu zimetufanya shamba la bibi.
leo nimeongeza vocha ya 1000 airtel nilipotaka kujiunga na bando ya intaneti wakaniambia nijaribu tena baadae ingawa nilijaribu mara mbili sikupata mafanikio.
nilipojaribu mara ya tatu wakaniambia salio halitoshi kumbe walinichukulia sh 2 wakijua itabidi ninunue vocha nyingine ili nijiunge na bando .
ujumbe kwenu airtel pamoja na kutuibia kwanini hamboreshi huduma zenu?? Baadhi ya maeneo ya mijini intaneti ni shida kupatikana au spidi ni ndogo sana hata simu ya kuongea ikipigwa hamuelewani ujumbe wangu ni kuwa
hizo ela munazotuibia nunueni minara iwe mingi huduma iwe nzuri sio kutuibia halafu wanahisa wanakula ela yetu iliyoibwa.
 
Wamenitapeli elfu 40 huu mtandao ni wa ******* sijapata wahi ona....

Ila hiyo elfu 40 lazma wairudishe naona wameni block nikipiga 100 siwapati...

Kesho nampango wa kuwafuata pale morocco makao makuu...
 
Pole sana mdau
2(tsh) x 10m(watu) = 20mtsh
Wanapiga mpunga si mchezo asee
Maana wamenizungusha wiki imeisha bila msaada wowote...

Leo nimewatafuta tokea asubuhi naona wananiambia watoa huduma wanahudumia wateja wengine so nijaribu baadae....

Naona wameniblock kabisa kwanini iwe tokea asubuhi?
 
Hivi tcra kazi yao hasa ni nini?
Sijaona msaada wao wowote kesho naenda ofisini kwao halafu nitakuletea mrejesho wanataka kutufanya watanzania wapumbavu.....

Hawajui watu tunatofoutiana maana nimejitahidi kuwavumilia kesho imekuwa kesho hatimae naona wamefungia namba yangu ili nisiwapate hawajui kuwa niko jirani yao tu hapa....
 
Tcra walitakiwa kuwa na dawati ambalo watu wenye malalamiko dhidi ya mitando, watalitumia na kupata majawabu ya mitanziko hii.
Sio kuwa na dola isiyo mtete mwananchi dhidi ya hawa mabelari.
Pole sana mkuu.
Mie nasubiri mrejesho.
 
Kwa wale tunaotumia simu na mitandao kampuni za simu zimetufanya shamba la bibi.
leo nimeongeza vocha ya 1000 airtel nilipotaka kujiunga na bando ya intaneti wakaniambia nijaribu tena baadae ingawa nilijaribu mara mbili sikupata mafanikio.

nilipojaribu mara ya tatu wakaniambia salio halitoshi kumbe walinichukulia sh 2 wakijua itabidi ninunue vocha nyingine ili nijiunge na bando .
ujumbe kwenu airtel pamoja na kutuibia kwanini hamboreshi huduma zenu?? Baadhi ya maeneo ya mijini intaneti ni shida kupatikana au spidi ni ndogo sana hata simu ya kuongea ikipigwa hamuelewani ujumbe wangu ni kuwa
hizo ela munazotuibia nunueni minara iwe mingi huduma iwe nzuri sio kutuibia halafu wanahisa wanakula ela yetu iliyoibwa.

Yaani hiyo ndiyo style yao mpya, WEZI wakubwa hawa Airtel. Ukiingiza vocha tu wanakuibia bila aibu fedha kidogo, jana waliniunga na 'magic voice' na kunikata sh 240 bila ridhaa yangu. Kuwapigia customer care wananiambia eti nitakuwa nimejiunga bila kujua. Nikamuuliza kwani mtu anajiungaje? kanitaji code ndefu kabisa, nikamwuliza hivi inawezekaneje mtu abonyeze namba zote hizo za code bila kujua? akawa anabwabwaja tu. Airtel wameanza wizi wa mchana kweupe, zamani ndiyo walikuwa wanaonekana kustaarabika lakini kwa sasa ni robbers by all accounts. Na Halotel nao leo wameniibia shilingi moja. Shida ni kuwa huwezi kujiunga na kifurushi cha internet mpaka uingize vocha nyingine na ukiingiza ya sh500 basi sh 499 zinakuwa redundant - huwezi ukapata kifurushi cha 499 ili ujiunge. Sijui niende kuwashitaki wapi hawa watu, wanakera balaa.
 
Na tigo wana huo ujinga wa kukata hela. Ukiwapigia wanakuambia umejiunga na hadithi halafu walivyo matapeli hata hadithi hawatumi. Hii mitandao ishakuwa ya kitapeli
 
Pole sana mdau
2(tsh) x 10m(watu) = 20mtsh
Wanapiga mpunga si mchezo asee
Ni uwelewa Mdogo tu wa mambo. Hakuna cha kuibiwa hapo. Hivi ukiweka vocha ya tsh 1000, afu data ipo on unadhani kitakachotokea nini? Watu wanajisahau na vifurushi sana, wanadhani vifurushi ndo vocha sahihi, wakati ile ni promosheni tu. Kwa taarifa tu, kama data yako ipo on, na umeongoza vocha, lazima vocha yako itatumika.
 
Ulikuwepo wakati wahusika wanajaza vocha?
Unauhakika gani kwamba data ilikua on?
Mashtaka haya ni ya kwanza kutolewa na wahusika hawa?
 
Screenshot_2018-04-18-09-09-59.png
Mimi wemeniunganisha na magic voice usiku wa manane
 
Ni uwelewa Mdogo tu wa mambo. Hakuna cha kuibiwa hapo. Hivi ukiweka vocha ya tsh 1000, afu data ipo on unadhani kitakachotokea nini? Watu wanajisahau na vifurushi sana, wanadhani vifurushi ndo vocha sahihi, wakati ile ni promosheni tu. Kwa taarifa tu, kama data yako ipo on, na umeongoza vocha, lazima vocha yako itatumika.
Ungeuliza kwanza kama data ilizimwa ama la kabla ya kuandika shairi refu namna hii ingekuwa vema sana.
 
Kuwa makini wakati unajiunga zima data kama data zikiwa on lazima walambe
 
Back
Top Bottom