GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,450
- 127,624
Deo ondoa hii kitu haraka kwenye thread yangu bwana.., we vipi.., anzisha thread yako uweke hii habari nadhani ita-make headline.., afu kesho yake ujikute mabwepande shauri yako..
Kuwa Kama Mwanamume na Usiwe Mwanaume!!! Unaogopa Nini Chini Ya Jua hili? Waoga Kama Nyie Ndiyo Mnatuponza Sisi Wapenda Mabadiliko na Maendeleo Ya Nchi Yetu hii. Mtu Mkweli na Muwazi hata Mwenyezi Mungu Anampenda na Siku Zote Mtu Mwoga Huwa Ni Mbumbumbu na Asiye na Thamani hata Ya Kuishi Duniani. Hivi Edward Snowden Angekuwa Mwoga Kama Wewe Leo Hii Tungejua Siri Kubwa na Za Kwamba Wamarekani Wanafanya Ujasusi ktk Simu Za Viongozi Wakubwa Kabisa Duniani, Mitandao Ya Kijamii na Hata ktk Nchi Nyingi Duniani hadi Ikapelekea Rais Wao Akaomba Radhi? Hivi Unajua Kwanini Wakazi Wengi Waliokuwa Wanaishi Pale Zamani Drive in Cinema ambapo Sasa Kuna Ofisi za Kampuni Ya Simu Ya Zantel na Ubalozi Wa Marekani Wamehama na Kuuza Maeneo Yao? Kwa Taarifa Yako tu na Kwa Faida Yako Eneo Lile Zima Kwa Urefu wa Mita 500 East, West, North and South Kila Kinachofanyika ktk Nyumba Jamaa Ubalozini Wanaona na Wanajua Siri Nyingi Sana za Wakazi wa Pale na Kwa Kukupa tu Taarifa Nyingine Juzi tu Siku Ya Alhamisi Kuamkia Ijumaa Nyumba Ya Mwarabu Ipo Kama Mita 100 Tu Kutoka Uwanja Wa Msasani Magunia Usiku Walivamiwa na Majambazi na Cha Kushangaza Wenye Nyumba Walikuwa Hawajui na Wamelala Fofofo ila Watu wa Ubalozini Walikuwa Wana Monitor ktk Mitambo Yao Wakaona Tukio Zima na Kuwatuma Askari Wao Kwenda ktk Nyumba Na Kufanikiwa Kuwafurumusha Wale Majambazi Ndipo Mwarabu Kushtuka na Kuamka na Mitongotongo Yake Machoni na Akishangaa. Nimekudokolea Baadhi tu na Siku Nyingine Nikijisikia Nitakuambia ni Kwanini Watu Wengi Walionunua Yale Magari Ya Mnada Yaliyokuwa Yanauzwa Pale Ubalozi wa Marekani Mwaka Jana Sasa Hawayaendeshi tena na Pia Kwanini Siku Hizi Watu Wenye Akili Wanakwepa Simu za Blackberry Zile Original Za Kutoka US na Pia Nikijisikia Nitawaambieni Ni Kwanini Mara Baada tu Ya Ujio wa Rais Wa Dunia Mwenye Asili Ya Kenya Alipoondoka tu Jijini Kesho Yake Zile Simu Zote Takribani 1000 ( Elfu Moja Nasisitiza ) Zilizotumika ktk Mawasiliano Zilisagwasagwa na Zikawa Nyang'anyang'a na Lile Gari Maalum La Kushindilia Kifusi au Lami. Kwa Wamarekani Sisi Tuko Uchi ( Utupu ) Wa Mnyama Na Wanatusanifu na Kutukejeli Watakavyo. Wajinga Ndiyo Waliwao......................................!!!!!!!! Jumapili Njema Wana JF Wote.