AIRTEL, VODA Mkome kudhalilisha dada zetu..!

AIRTEL, VODA Mkome kudhalilisha dada zetu..!

umeshawahi kuwaona wanavyotia huruma kwa kukosa hata shilingi hamsini...??? Hata kazi unaifanya wewe na wengine, kuna watu wanakuonea huruma...

halafu kwani ni wadada tu ndio wanaosimama mbona hata wakaka wapo

au mtoa mada hajawaona!!!!!!
 
Mkuu umefanya upelelezi ukajua wanalipwa bei gani kwa siku?, kama wanalipwa 50,000 kwa siku utasemaje?, fanya upelelezi kwanza. Kazi ni kazi, kibaya kulazimishwa. Vipi traffic wanaoshinda wanaongoza gari siku nzima wakikumbana na moshi, vumbi?
 
Hivi huyo na dada anayegongwa na mwenyekiti wa chama ili apewe ubunge wa viti maalumu nani anadhalilika zaidi?

Deo ondoa hii kitu haraka kwenye thread yangu bwana.., we vipi.., anzisha thread yako uweke hii habari nadhani ita-make headline.., afu kesho yake ujikute mabwepande shauri yako..
 
Mkuu umefanya upelelezi ukajua wanalipwa bei gani kwa siku?, kama wanalipwa 50,000 kwa siku utasemaje?, fanya upelelezi kwanza. Kazi ni kazi, kibaya kulazimishwa. Vipi traffic wanaoshinda wanaongoza gari siku nzima wakikumbana na moshi, vumbi?

Am not intrested na how much they earn per day.., by the way traffic hasimami kama sanamu.., get it.??!
 
Kuna mtu humu kasema labda mtoa mada kaitaja Centre of attension yake...

Jamani ile ni kazi halali tena ya kutokea jasho, binafsi nawapongeza hao voda na airtel kwa kubuni kitu kizuri kuwapunguzia tatizo la ajira wadogo zetu.
 
Am not intrested na how much they earn per day.., by the way traffic hasimami kama sanamu.., get it.??!

Ndio kazi yao kusimama kama sanamu labda ungekuja na constructive ideas to make their work better sio kumwaga povu tu kuwa wanalazimishwa
 
Kuna wamama na wadada wanaponda kokoto mchana kutwa mbona husemi serikali iwatafutie kazi. Kuna watu wanaitwa makuli wanabebeshwa mizigo zaidi ya punda. Watu tumekulia vijijini tunalima na jua na mvua sembuse kusimama tu!. Wewe iko shangaa jua? Kwa hiyo mtu akisema nitajie kazi 20 ngumu na za kudhalilisha nchini utaiweka na hii pia?.....Acha hizo bana. We umeajili wangapi mpaka sasa. Huu ni muda wa kuwashukuru hawa jamaa wa mitandao.
 
bora kusimama siku nzima kwa kazi halali kuliko kusimama kwa masaa machache usiku viwanja.
 
Sasa kazi hakuna unafikiri Airtel au voda wanawalazimisha kuchukua kazi za kusimama na mabango ......ugumu wa maisha ndo maana sister yuko tayari kushika bango masaa 12 kwa hela <=10000 per day

Alafu kule wale maboya wanaodai wanakwenda kuwawakilisha watanzania wa hali ya chini wanadai laki 3 haitoshi... Very awkward.......
 
Leo nimesikitika kuona wadada vigori wakisimamishwa barabarani huku wamebeba mabango ya matangazo ya kampuni ya AIRTEL, yaani wanasimamishwa tangia mchana jua kali mpaka jioni.., wana kula moshi na vumbi la magari pale ubungo kama masanamu.., yaani daaa..!, hivi hayo matangazo mkiweka kwenye mabango mtapungukiwa na nini.., ndo mnakwepa kodi au..??! MKOMEE!! Ona huyu dada mwenye shirt la airtel hapo (shirt jekundu, picha nimepiga kwa mbali)
View attachment 140563

Mbona huwasemei wabeba zege juani au ndio haki yao?
 
Hii aina ya matangazo ni ya kipuuzi sana. Tuungane kuikomesha. Hata kama ni ajira, hii siyo kabisa!!
Ndio kabisa Mheshimiwa Jackton Manyerere, ni bora tu waendelee kutangaza kwenye page zenu kwa nguvu zaidi kuliko huu upuuzi wanaofanya..!
 
Ajira ní lazima narudia tena ní LAZIMA ijali na kuthamini utu wa mwanadamu. Ajira yoyote inayodhalilisha utu wa mwanadamu ní kosa kisheria na ní dhambi mbele za Mungu. Tatizo la nchi yetu haina mamlaka(kama ipo ní bure tu) inayoangalia hizo haki za wafanyakazi. Kama mtu anajua masuala ya kitabibu na afya ya jamii atuambie binadamu anaweza kusimama kwa muda bila kuleta matatizo, matatizo ya kiafya yatokanayo na vumbi, moshi na kelele, matatizo ya kisaikolojia, na namna hiyo ajira inavyowajibika kwa hayo. Nenda pale twiga cement angalia šera zao za usalama ona wanavyojitaidi kuzisimamia...halafu fananisha na hao mnaowapongeza wamepata ajira...ní hatari tupu...
 
Leo nimesikitika kuona wadada vigori wakisimamishwa barabarani huku wamebeba mabango ya matangazo ya kampuni ya AIRTEL, yaani wanasimamishwa tangia mchana jua kali mpaka jioni.., wana kula moshi na vumbi la magari pale ubungo kama masanamu.., yaani daaa..!, hivi hayo matangazo mkiweka kwenye mabango mtapungukiwa na nini.., ndo mnakwepa kodi au..??! MKOMEE!! Ona huyu dada mwenye shirt la airtel hapo (shirt jekundu, picha nimepiga kwa mbali)
View attachment 140563

Mkuu karibu huku kwetu uswahilini ushuhudie hali halisi ya mtanzania, karibu hukukwetu utambue kuwa ni heri kupatakitu kuliko kukosakitu, karibu utambue maana halisi ya maisha magumu.
 
Back
Top Bottom