Airtel simu ya mkopo "Wanataka kutapeli"

IQup

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2018
Posts
1,845
Reaction score
2,909
Habarini!, kuna ndugu yangu alichukua simu airtel kwa mkopo...simu yake ilipata hitilafu kidogo na akawarudishia ili waitengeneze...wakamuahidi baada ya wiki 3 watamrudishia...akalipa gharama ya matengenezo huku akiendelea kulipa malipo ya siku...mwezi wa pili sasa yaani ana wiki 6 sasa hawajamrudishia simu na wanamtaka aendelee kulipia....amewafata mara 4 na anajibiwa kuwa Bado haijafika...na asipolipa malipo ya siku anapigiwa simu wakimkosa anapigiwa aliyemdhamini kumsihi afanye malipo na simu wanayo wenyewe airtel. Ameona anatapeliwa waziwazi na kuniomba nimsaidie ila Mimi Sina hata pa kuanzia japo nimemjibu nitawatafuta airtel hewani ...

Naombeni msaada anayejua inatakiwa afanye Nini hapa alipofikia, anadai inaenda wiki ya Saba...asipolipa anapigiwa simu anatishwa...na Ile simu alipoirudisha airtel walimwambia atoe laini yake na atoe password zote za simu ndipo akawakabidhi...

Mwenye uelewa anisaidie afanye Nini katika hili?

NB: simu Hadi sasa amebakiza miezi 2 kumaliza mkopo
 
Ila haya mambo ya kukopa simu, au pesa mtandaoni. Mi naona kuna utapeli sana. Ni bora kuvumilia tu ununue moja kwa moja
Nadhani ni ukata wa kupata hela ya pamoja...ndio maana akaona ni Bora akope tu simu
 
Aende hapo airtel alipoacha simu ashinde nao na aahakikishe haondoki bila simu
Ameenda mara mbili siku tofauti tofauti ila kaambiwa simu imetoka kwa fundi imerudi makao makuu dar alafu anaambiwa asubirie inatumwa atapigiwa simu...ashakata tamaa anaona kama siye ndugu zake hatumsaidii simu yake kupatikana...wahudumu wanamjibu simu Bado haijafika...Kila akienda anajibiwa hivyo
 
Haya makampuni ya kukopesha simu ni kama vikundi vya utapeli kuna KESI Moja mtu kakopa simu imefika siku ya marejesho hata muda haujafika anapokea sms za vitisho na kuambiwa usipolipa tutakutangaza kwamba wewe ni tapeli mitandaoni mara usipolipa ndugu zako watakusaidia kulipa yaani ni vitisho mwanzo mwisho na wakati kipindi anakopa aliambiwa ukishindwa kulipa ni simu ndio itakayofungwa
 
Wanasumbua sana...hivi akienda mahakama ya mwanzo ataweza kusaidiwa?, au kituo Cha polisi chochote wanaweza msaidia??
 
Nimeshakopa simu Y9 nikashindwa malipo yao nikatupa nikakopa watu tz credit na yenyewe Kuna mjinga ananidai nimemuachia na deni lake la 336k Cha ajabu sijawahi pigiwa simu Wala hakukua na mdhamini
 
Una Bahati...Huwa wanataka uandike namba ya simu ya mtu mwingine huyo ndiye wanaye mpigia wakikukosa wewe muhusika...yaani wanasumbua sana aisee
 
Habarini!, kuna ndugu yangu alichukua simu airtel kwa mkopo...simu yake ilipata hitilafu kidogo na akawarudishia ili waitengeneze...wakamuahidi baada ya wiki 3 watamrudishia...akalipa gharama ya matengenezo huku akiendelea kulipa malipo ya siku...mwezi wa pili sasa yaani ana wiki 6 sasa hawajamrudishia simu na wanamtaka aendelee kulipia....amewafata mara 4 na anajibiwa kuwa Bado haijafika...na asipolipa malipo ya siku anapigiwa simu wakimkosa anapigiwa aliyemdhamini kumsihi afanye malipo na simu wanayo wenyewe airtel. Ameona anatapeliwa waziwazi na kuniomba nimsaidie ila Mimi Sina hata pa kuanzia japo nimemjibu nitawatafuta airtel hewani ...

Naombeni msaada anayejua inatakiwa afanye Nini hapa alipofikia, anadai inaenda wiki ya Saba...asipolipa anapigiwa simu anatishwa...na Ile simu alipoirudisha airtel walimwambia atoe laini yake na atoe password zote za simu ndipo akawakabidhi...

Mwenye uelewa anisaidie afanye Nini katika hili?

NB: simu Hadi sasa amebakiza miezi 2 kumaliza mkopo
Airtel mbona ni matapeli kitambo wanaeleweka hao.
 
Back
Top Bottom