Airtel nao wale wale, hakuna afadhali

Airtel nao wale wale, hakuna afadhali

Nashukuru naishi karibu na chuo... Nafaidika na offer za university za tigo...*148*01*20#
 
airtel iko poa ila mie leo nimeitoa kwasabu ya gps kt jiwasha..charge haimaliz siku bhanaa

Hilo tatizo nimekutana nalo baada ya kuanza kutumia laini yao.Nahisi kuna tatizo katika laini zao.kuna kiprogram kinahitwa GPSD kinafyonza betri ni balaa
 
Pata ongezeko la ziada la data, dakika ukinunua Yatosha bando kupitia Airtel Money... Piga*150*60# sasa na chagua 6.
Ukiweza tafuta airtel yatosha vocha, 125 MB, dk 15, SMS 300 kwa tsh. 500/- 24hrs
 
Hivi 10MB mtu utafanyia nini? TCRA wapo kufanya nini sijui. Inatakiwa waweke ukomo wa chini wa MB, huu ni unyimwaji wa kupata habari kwa wananchi.
 
nahisi kama Airtel wamenitosa. Nina 900MB, nasikitika siwezi kushusha mafaili yangu, mafaili yamekwama njiani. Mbaya zaidi nina siku chache za kuyashusha. Naishia kuperuzi tu. Sioni anayeweza kuleta suluhisho, kwani machagua yanapungua kwa wale tunaoishi mikoa 'iliyosahaulika'
 
Zantel hawana 3G mikoani ni Upuuzi kwa Watu wa Huko... Dar na Zanzibar wanafaidi... ila Nilitumia Siku Moja Nikapiga Customer Care akapokea Mzenji na Kiswahili chake Mi kicheko tu

Hata tigo 3G mikoani ni shida tupu. Few weeks zilopita nilikuwa bukombe nilishindwa kupata tigo 3G internet. Nikaenda geita hali ikawa vile vile kama bukombe, no internet 3G. Nilihuzika sana.
 
Hii mitandao kwa upande wa internate ni kwa watu washio miji mikubwa tu. Hata mwanga kil. 3g ni 0
 
Back
Top Bottom