Airtel mnazingua wateja na hasa kitengo cha huduma kwa wateja mnazingua sana!

Adimu

JF-Expert Member
Aug 22, 2013
655
284
Habari wanajamvi, nimeleta hoja hii ili kama kuna wahusika waliwasilishe hili.

Niliwai kusajili laini ya airtel miezi kadhaa iliyopita kisha nikaivunjilia mbali, hii ni kwasababu nilikua nikiunga bando nawasiliana gafla meseji zinakua hazitoki na ni kwa baadhi ya namba, nikaona ngoja niwapigie maana ilikua nachati na baby wangu tena story zimenoga usiku kama wa saa sita hivi, ile kupiga jibu nlopata ni "hakuna tatizo upande wetu labda subili baada ya lisaa limoja" nikakasirika sana usiku wa saa sita huyo anaesubili nimjibu si atakua amelala nikavunja lain siku ile ile. Ikapita miezi kadhaa nikaamua kusajili tena maana natokea tu kuupenda huu mtandao, sasa jana asubuhi nimenunua zangu vocha ile naweka mala napata majibu ya ajabu ajabu mala vocha imezuiwa subili baada ya saa 12, mala vocha haijaruhusiwa iludishe ulikonunua, nikaona ngoja niwapigie wahusika, majibu niliyopata ni "subili baada ya nusu saa" nikasubili dakika 45, kupiga tena nikaambiwa "subili kama lisaa limoja" nikaweka zangu vocha ya tigo nikafanya matumizi yangu. Sasa leo asubui nawapigia tena maana vocha haingii wanasema "ni tatizo we subili tu" nikasema tangu jana kwaiyo watu hawasiliani kwa airtel au ni mm tu? na nisubili kwa muda gani? majibu ni "mimi sio mtu wa IT kwaiyo ww subili tu"

Sikutaka kutukana kwa kuheshimu kazi ya hawa customer care ila airtel kitengo cha huduma kwa wateja wanazingua na wengi wanaonekana hawana msaada kwa wateja, wahusika chukueni hii kutoka kwangu, hapa nafikilia kuivunja kwa mala ya pili hii lain.
 
Back
Top Bottom