mpita-njia
JF-Expert Member
- Dec 3, 2010
- 1,736
- 1,621
- Thread starter
- #21
Me naomba kujuzwa tofauti ya Boeing, airbus na hzi ndege zetu. Maana napata shida sana, ni majina ya kampuni, au majina ya ukubwa wa ndege husika? Msaada tafadhali...
Boeing ni kampuni ya kutengeneza ndege ambayo iko Marekani.
Ndege zao ni kama Boeing 737, 747 Jumbo Jet, 787 Dreamliner nk...
Airbus ni kampuni ya muungano wa nchi za Ulaya. Makao makuu ni France ila nchi zingine zinatengeneza body parts na kupeleka France.
Ndege zake ni nyingi lakini maarufu kwa sasa ni A380 Super Jumbo. Hii ndio ndege kubwa kwa sasa. Details zake zishawekwa hapo.
Bombardier ni ya wa Canada. Hawa wanatengeneza low Budget airline kwa nchi ambazo hazina miundombinu ya kisasa.