Air Tanzania yapandisha nauli zake

Rockcity native

JF-Expert Member
Dec 31, 2012
2,167
1,403
Habari za leo wanajanvi.... tokea jana ndege yetu penda Air Tanzania nauli zake zimepanda kwa asilimia kubwa sana kutoka zile za awali.

Nimejaribu kununua tiket online kama kawaida yangu lakini bei niliyokutana nayo tofauti na sikuzote.

Nikaona isiwe taabu nikaenda ofisi zao za town, kufika pale wakanambia nauli ni kweli zimepanda.

Kwenda Mwanza na kurudi nilishazoea kupata bei nafuu ya laki 365,000 lakini jana nikakutana na kitu cha laki 420,000.

Kuna haja ya mamlaka husika kupitia tena hivi viwango vya nauli, vina tuumiza sana sisi wananchi.
 
Nafuu 365,000/= Kipindi cha Fastjet ulikuwa unapanda nini ? Hio unayoita nafuu kipindi kabla hatujapata hizo ndege bei ilikuwa nzuri kuliko hio unayoiona nafuu

Atcl hawana mpinzani kwa route za ndani... Kuzidisha nauli Mara dufu Ni kufukuza wateja...
 
Habari za leo wanajanvi.... tokea jana ndege yetu penda Air Tanzania nauli zake zimepanda kwa asilimia kubwa sana kutoka zile za awali....
Hilo shirika la ATCL alina mda mrefu kwenye biashara kwasababu aliendani na hari halisi ya uchumi wa wananchi, Mtu aende Mbeya kuenda na kurudi kwa 520k kufanya nini kuna biashara gani huku ya kurudisha hiyo gharama. Watabaki na abiria watchache sana ili route zita anza kufa automatically
 
Habari za leo wanajanvi.... tokea jana ndege yetu penda Air Tanzania nauli zake zimepanda kwa asilimia kubwa sana kutoka zile za awali.

Nimejaribu kununua tiket online kama kawaida yangu lakini bei niliyokutana nayo tofauti na sikuzote.

Nikaona isiwe taabu nikaenda ofisi zao za town, kufika pale wakanambia nauli ni kweli zimepanda.

Kwenda Mwanza na kurudi nilishazoea kupata bei nafuu ya laki 365,000 lakini jana nikakutana na kitu cha laki 420,000.

Kuna haja ya mamlaka husika kupitia tena hivi viwango vya nauli, vina tuumiza sana sisi wananchi.
Kwa hadhi yako hutakiwi kulalamika mkuu
 
Mkuu mbona kesho kuna ndege ya go and return mwanza kwa 341,600 (170,800x2) tena ni less ya hio 365,000 unayosema ni cheap..hio 420,000 unataka business class ama?km ndivyo then stop complaining and spread lies.
View attachment 1705645
 
Attachments

  • Screenshot_20210218-191508_Chrome.jpg
    Screenshot_20210218-191508_Chrome.jpg
    36.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom