Air Tanzania yaongeza safari za Dodoma

Air Tanzania yaongeza safari za Dodoma

Disclaimer:

There are daily flights Monday to Sunday including the added flights!

----------------

Shirika zima la ATC ikiwemo idara yao ya sheria hawajui matumizi ya neno "disclaimer"

Which means kuna mambo kibao ya kitaalam na kiuendeshaji hawayaelewi hawa watu
Kabisa, Hili neno linalenga kuiweka public aware na mischief inayoweza kujitokeza in the cause of enjoying my service hivyo nakuweka uwe informed ili kuepuka liability ya kesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu Joka kuu, hakuna sehemu nimesema kigezo lazima mji uwe katikati hapana ila kila nchi in sababu zake mimi binafsi sijajuwa sababu zetu inawezekana zipo na zina nguvu ndio maana wameamua. ilikuwa sababu zianishwe halafu kupimwa. kila nchi ina mazingira yake ziko usafiri uko wa haraka na nchi zingine kama majimbo yanakuwa na huduma zote kila jimbo sisi kwetu ilikuwa kila kitu Dar hata ukiwa Mwanza au Songea huko ni lazima uende Dar. kosa ilikuwa kuweka kila kitu pembeni ya nchi ila kama ingekuwa kila mkoa unatoa sawa hapo hakuna shida hata mji mkuu uende Pemba tatizo mfumo wetu wa huduma. Kuhusu ndege sio shida ni kitu kizuri cha maendeleo watalii wakija ndani ndege ni kuwafanya wepesi wa kusafiri ndani ila sikuona sababu ya kununua ndege kubwa kama Airbus ilikuwa tujikite na safari za ndani ni muhimu sana. leo kama mtu ana business meeting Mwanza anenda asubuhi jioni karudi kazi zinafanyika zamani hakuna hizo mtu akifikiria safari ya Mwanza hata kama kuna fursa inabidi aache. ndege ni kitu kizuri na sio ndege tu train na usafiri wetu wa mabus hii itachangia ukuaji wa uchumi ni kama kupunguza foleni mjini inachangia uchumi kazi ya kufanya masaa 3 labda robo saa tu.

..mimi hoja yangu imejikita ktk GHARAMA.

..tayari tulishawekeza ktk Dsm kama mji wetu mkuu.

..Kwa hiyo hakuna sababu ya kuwekeza au kutumia fedha kwa jambo lilelile.

..Uamuzi wa kujenga mji mkuu Dodoma unaonyesha kuwa hatuko makini ktk matumizi ya fedha zetu.

..kuhusu Dsm kuwa "pembezoni" sidhani kama ni hoja yenye ushawishi wa kutosha.

..Kuna nchi nyingi zimepiga hatua kubwa ya maendeleo na miji yao mikuu iko pembezoni.

..Washington DC, London, Stockholm, Helsinki, Oslo, Berlin, Paris, ni miji mikuu na iko "pembezoni."

..Tukija kwenye usafiri wa anga naunga mkono serekali kujenga viwanja vya ndege maeneo mbalimbali ili yaweze kufikika kwa urahisi na uharaka zaidi.

..Siungi mkono kuwa na shirika la ndege kwasababu ya gharama kubwa tutakazoingia ktk ununuzi wa ndege na uendeshaji wa shirika.

..mashirika ya ndege ya nchi zote zinazotuzunguka yanaendeshwa kwa hasara.

South Africa, ambao wana uchumi mkubwa kutuzidi, na wanapokea wasafiri wengi zaidi yetu, mwaka huu shirika lao la ndege imebidi lipewe ruzuku ya zaidi ya usd 300 million.

..Uwekezaji ktk shirika la ndege haukuwa uamuzi makini na utaliingiza taifa ktk gharama kubwa na hasara.
 
..Uwekezaji ktk shirika la ndege haukuwa uamuzi makini na utaliingiza taifa ktk gharama kubwa na hasara.


na imeshaanza kutuingiza gharama

bilioni 600 ya ukarabati wa ndege mpya imetoka fungu gani?

Waziri Kamwele kasema Rais ame approve, which means hazitoki ndani ya ATC, tumeomba kujua zime apruviwa kutoka wapi? hakuna majibu
 
Hiyo ni kwa maslahi mapana yao, yaani ijumaa jioni Dom to Dar. Jmosi, Jpili Dar halafu Jumatatu huyooo saa moja asubuhi wanawahi Dar to Dom!!


Hizo siku za safari za weekend na Jumatatu usingizi wa mang'amung'amu
 
Bei ya Dar-Dom round trip kwenda pekee
Screenshot_20190314-153913.png
 
Back
Top Bottom