Air Tanzania yaongeza safari za Dodoma

Air Tanzania yaongeza safari za Dodoma

..Exactly.

..ni GHARAMA / HASARA za kuhamishia makao makuu ya serekali Dodoma.

..kwa maoni yangu Dodoma kuwa makao makuu ya bunge ilikuwa inatosha kuuenzi uamuzi na ndoto ya Mwalimu Nyerere.
Suala la kuwa na flight mara mbili kwa siku linahusu nini Dodoma kuwa makao makuu? hivi ni vitu viwili tofauti ATCL wana ndege tayari na wanachagua route zenye biashara kwao na wazi Dodoma kumekuwa na ongezeko kwa hiyo ni fursa. Sio kila jambo ni kupinga tu ndege zikikaa airport maneno ndege zikianza route au kuongeza maneno ni kama kusema hatutaki ndege. Kuna option nyingi hutaki ndege gari ziko kuna watu wanataka ndege. Dodoma kuwa makao makuu imetangazwa 2015 kabla hata ya ndege ni mambo mawili tofauti. mambo ya urasimu kama wazamani kila kitu Dar umeisha na hii imewauma sana watu wa Dar( actual hakuna mtu wa Dar wengi wametoka huko mikoani) siku hizi ukitaka hata passport hukohuko uliko kama Mbeya, Iringa sijui Mwanza unapata. vizuri kuanisha hasara gani tunaongelea hapa? mtu alikuwa anatoka Tabora mpaka Dar kufuatilia mambo ya kiserikali leo Dodoma iko karibu na kwake na mikoa mingi kufika Dodoma ni rahisi kuliko Dar sababu ya kuwa katikati hapo nashindwa kuelewa hasara za nini? gharama kuhamia tu baada ya hapo kazi kama kawaida tu. Serikali imeshaamua na hata kabla vyama vya siasa mikutano mikubwa ilikuwa Dodoma sababu ya kupunguza gharama kufika ilikuwa rahisi kuliko Dar.
 
Heijah,

..angalia ramani ya nchi za Afrika na miji yao mikuu.

..hoja kwamba mji mkuu unapaswa kuwa katikati ya nchi ni mufilisi.

..kilichotakiwa kufanyika ni kupeleka huduma za serekali karibu zaidi na wananchi mikoani waliko.

..siyo busara kuingia gharama za kujenga mji mkuu mpya wakati nchi bado inategemea misaada ya wahisani kwa bajeti ya maendeleo.

..kuhusu ununuzi wa ndege, kwa ujumla biashara ya usafiri wa anga ni hasara. ATCL ni sawa na "KUPE" atakayenyonya fedha nyingi za ruzuku toka serekalini.


1552451581790.png
 
Nashauri kuwe na ratiba ya MWANZA - DODOMA - DAR NA DAR - DODOMA - MWANZA.
 
Kuna watu walitaka ipunguze safari, kwa hiyo wanavyoona hivi wanakua katika wakati mgumu kweli.

Wamenuna
Nilitegemea labda wameanza kwenda nje ya mipaka ya Afrika kumbe ni local routes zinashindana na yutong na scania?

In God we trust
 
Heijah,

..angalia ramani ya nchi za Afrika na miji yao mikuu.

..hoja kwamba mji mkuu unapaswa kuwa katikati ya nchi ni mufilisi.

..kilichotakiwa kufanyika ni kupeleka huduma za serekali karibu zaidi na wananchi mikoani waliko.

..siyo busara kuingia gharama za kujenga mji mkuu mpya wakati nchi bado inategemea misaada ya wahisani kwa bajeti ya maendeleo.

..kuhusu ununuzi wa ndege, kwa ujumla biashara ya usafiri wa anga ni hasara. ATCL ni sawa na "KUPE" atakayenyonya fedha nyingi za ruzuku toka serekalini.


View attachment 1044414
Ndugu yangu Joka kuu, hakuna sehemu nimesema kigezo lazima mji uwe katikati hapana ila kila nchi in sababu zake mimi binafsi sijajuwa sababu zetu inawezekana zipo na zina nguvu ndio maana wameamua. ilikuwa sababu zianishwe halafu kupimwa. kila nchi ina mazingira yake ziko usafiri uko wa haraka na nchi zingine kama majimbo yanakuwa na huduma zote kila jimbo sisi kwetu ilikuwa kila kitu Dar hata ukiwa Mwanza au Songea huko ni lazima uende Dar. kosa ilikuwa kuweka kila kitu pembeni ya nchi ila kama ingekuwa kila mkoa unatoa sawa hapo hakuna shida hata mji mkuu uende Pemba tatizo mfumo wetu wa huduma. Kuhusu ndege sio shida ni kitu kizuri cha maendeleo watalii wakija ndani ndege ni kuwafanya wepesi wa kusafiri ndani ila sikuona sababu ya kununua ndege kubwa kama Airbus ilikuwa tujikite na safari za ndani ni muhimu sana. leo kama mtu ana business meeting Mwanza anenda asubuhi jioni karudi kazi zinafanyika zamani hakuna hizo mtu akifikiria safari ya Mwanza hata kama kuna fursa inabidi aache. ndege ni kitu kizuri na sio ndege tu train na usafiri wetu wa mabus hii itachangia ukuaji wa uchumi ni kama kupunguza foleni mjini inachangia uchumi kazi ya kufanya masaa 3 labda robo saa tu.
 
Disclaimer:

There are daily flights Monday to Sunday including the added flights!

----------------

Shirika zima la ATC ikiwemo idara yao ya sheria hawajui matumizi ya neno "disclaimer"

Which means kuna mambo kibao ya kitaalam na kiuendeshaji hawayaelewi hawa watu

Nikajua labda ni mimi tu nitakuwa kilaza Hilo neno disclaimer hapo sio mahala pake


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilitegemea labda wameanza kwenda nje ya mipaka ta Afrika kumbe ni local routes zinashindana na yutong na scania?

In God we trust
Hakuna shirika la ndege lililofanikiwa nje kabla ya kujiimarisha ndani
 
Disclaimer:

There are daily flights Monday to Sunday including the added flights!

----------------

Shirika zima la ATC ikiwemo idara yao ya sheria hawajui matumizi ya neno "disclaimer"

Which means kuna mambo kibao ya kitaalam na kiuendeshaji hawayaelewi hawa watu
Mkuu hongera kwa kuliona hilo, mimi nimetupia jicho sikuamini. Nimetafakari sana nikaona aibu kwetu watanzania kwa shirika kubwa la safari za anga nchini wanajiandikia bila kuangalia matumizi ya neno. Uwezo mdogo wa ngeli alio nao jiwe zinaambukiza hata mashirika yetu!
 
Kwa kweli hili neno "Disclaimer" halijakaa vizuri kabisa.
Hutumika kwa ajili ya kujitenga na madhara (liability) ambayo yanaweza kujitokeza na hivyo unajiwekea wigo wa usalama wako dhidi ya fidia inayoweza kudaiwa na waathirika wa taarifa yako.
Katika suala hili, kujulisha safari zingine kuwa zinaendelea kama kawaida, kwa upande wa ATCL ni faida (asset) wala sio madhara (liability), hivyo halifai kutumika hapo.
Lingetumika hata neno NB: "Nota Bene", "Note Well", "Remember" hata asterisk mark * ingefaa zaidi.

Lakini jambo lingine ni kuwa ukiwa na mawazo ya disclaimer utaanza kuchukua tahadhari hata kwa vitu visivyohitaji tahadhari hizo. Mfano kuna woga gani wa kutotoa price range, kama ambavyo FastJet alikuwa akifanya na mpaka sasa hivi Precision Air anafaya? Hii inamfanya mteja ajipange mapema badala ya kumuacha gizani na kuanza kucheza mchezo wa kuviziana ndio maana utamaduni wa kutumia ndege kwa nchi yetu upo chini sana kwa mazingira haya.
Mkuu hawa vilaza wanazidiwa na baadhi ya mabasi ya abiria yenyewe hutumia neno 'Discaimer' vuzuri kabisa. Utakuta tiketi zao zimeandikwa: "KILA ABIRIA ATUNZE MZIGO WAKE LA SIVYO HATUTAHUSIKA NA UPOTEVU WA KITU CHOCHOTE". Sasa hii kampuni ya jiwe, duh!
 
Back
Top Bottom