Aina za watu hatari katika kufanikisha ndoto zako

MMASSY

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
290
193
Na Jerome Mmassy,Arusha

Mwandishi wa vitabu maarufu Jim Rohn alisema kuwa “Wewe ni wastani wa watu watano unaokaa nao muda mwingi”.- Alisisitiza kuwa Kama unataka kufanikiwa hakikisha unatumia muda mwingi kukaa na watu ambao watakuwa na msaada kwenye mafanikio yako.

Katika Maisha ya kawaida unahitaji watu ili ufanikiwe. Kama unafanya biashara unahitaji watu( wateja wako na wafanyakazi). Kama unafanya kazi unahitaji watu ( bosi wako na wafanyakazi wenzako). Unahitaji amani unaporudi nyumbani. Unahitaji marafiki watakaoendana na wewe na wakukusaidia na kukufariji kipindi unapokuwa na shida.

Hebu jaribu kufikiria dunia hii ungekuwa peke yako ingekuwaje. Ukweli ni kwamba binadamu tumeumbwa kwa kutegemeana. Kuna vitu viko ndani yako kwa ajili ya wengine, pia kuna vitu unahitaji kutoka kwa wengine. Siku zoteunahitaji kupendwa, unahitaji kufarijiwa, unahitaji kuthaminiwa, unahitaji kusikilizwa. Yote haya bila watu huwezi kuyapata. Ijapokuwa watu ni muhimu sana kwa mafanikio yetu, lakini wanaweza kugeuka na kuwa mwiba mkubwa kwa mafanikio yetu kama tusipokuwa makini. Watu ambao tulidhani watatutia moyo kipindi kigumu ndio haohao wanatukatisha tamaa. Marafiki ambao tuliwaamini ndio hao wanatusaliti. Watu ambao tunadhani watatuhamasisha kupiga hatua katika mafanikio yetu, ndio hao wanaturudisha nyuma. Watu ni muhimu kwa mafanikio yetu, lakini pia inatakiwa kuwa makini sana ni watu wa namna gani wamekuzunguka. Kama usipokuwa makini na watu waliokuzunguka itakuwa ngumu sana kwako kufanikiwa. Hawa hapa chini ni watu unaotakiwa kuwaepuka katika maisha yako kama kweli unataka kufanikiwa:

Wakatishaji tamaa.

Watu kama hawa ukiwashirikisha mipango yako, lazima wakukatishe tamaa. Watakuambia maneno kama ‘ wewe huwezi’, ‘wengine wameshindwa utakuwa wewe?’, ‘haiwezekani’, na mengine kama hayo. Wao siku zote ni kukatisha tamaa na wanataka kukuona unabaki hivyo ulivyo. Ubaya wa hawa watu wanaweza kuwa ndugu zako wa karibu, wanaweza wakawa wazazi wako, akawa mpenzi wako, au ndugu wengine wa karibu na unaowaamini sana. Kumbuka hawakukatishi tamaa kwa sababu ya ulivyo,wanakukatisha tamaa kwa utakavyokuwa. Waepuke watu hawa katika maisha yako. Kama ni watu wako wa karibu sana unaweza ukaanza kupunguza muda unaokaa nao au ukaacha kabisa kuwashirikisha ndoto zako. Lakini pia unaweza ukawafundisha kwa kuwaelimisha kuhusu ndoto yako kwa kuwapa mifano ya watu ambao wamefanikiwa. Kama ukishindwa kuwaelimisha basi kaa nao mbali kadiri unavyoweza na usiwashirikishe mipango yako.Tafuta watu watakao kutia moyo na sio kukukatisha tamaa. Waweke pembeni watu wanaokukatisha tamaa kama kweli unataka kufanikiwa.

Walalamikaji na wanung’unikaji.

Hawa ni watu wanaolalamika na kunung’unika kila wakati. Wanalalamika kwa kila kitu na kila mtu. Hakuna kitu chochote kizuri wanachokiona kwenye maisha yao. Ni watu ambao hawako tayari kuwajibika na maisha yao. Ni watu wanaoilalamikia serikali kwa kila kitu. Wanaiona serikali kama ndio inawajibika na maisha yao.Hawa utawakuta vijiweni,utawakuta ofisini,kwenye makundi lakini pia unakaa nao hapo nyumbani. Jitahidi sana kuwaepuka watu hawa, ukiambatana nao muda si mrefu na wewe lazima utaanza kulalamika na kunung’unika. Na ukishaanza kulalamika na kunung’nuka utashindwa kuwajibika na maisha yako.Utakuwa umeupa ubongo wako jukumu la kufikiri kuwa hatima ya Maisha yako iko mikonononi mwa serikali ama mtu mwingine.ikiwa hivyo utaliwa unajidanganya.

Watu wenye mtazamo hasi.

Hili pia ni kundi la kuepuka sana. Hawa wanafanana na walalamikaji. Watu wanao ona na kuwaza mambo hasi tu. Siku zote wao kila kitu ni hasi. Mawazo yao ni hasi. Wanayoyasema ni hasi. Kila kitu wanakiona kibaya, hakuna kizuri kwenye maisha yao.Watu hawa wanatafuta habari mbaya. Wanapenda kusikia watu wanashindwa. Hawasikii habari nzuri kwenye maisha yao. Habari mbaya ndo wanazopenda na hupenda kuzipigia debe sana. Watu kama hawa wakiwa karibu yako watakufanya na wewe uwe hasi. Watakufanya uanze kuwaona watu wengine pia ni hasi na utatengenza uadui usio lazima na watu. Kila kitu utakiona hasi. Hata mawazo yako yataanza kuwa hasi.

Hakikisha unakuwa na watu ambao wako tayari kubadilisha hali hata kama ni hasi kuwa chanya. Watu ambao hata kama wanaona udhaifu wako wanakwambia kwamba inawezekana kubadilika a kuwa bora zaidi. Ambatana na watu chanya kwenye maisha yako, watakuamasisha kufikia ndoto yako.

Wavivu na wapenda starehe.

Hawa ni watu wengine wakuwaweka pembeni kwenye maisha yako kama kweli unataka kufanikiwa. Watu ambao hawataki kufanya kazi kwa bidii. Watu wanaotaka mafanikio kwa njia rahisi. Watu ambao hawataki kujitoa kwenye kile wanachofanya.Hawa mara nyingi watakuaminisha kuwa unaowaona wamefanikiwa wametumia njia za ushirikina ama walirithi mali za wazazi wao.Watakuaminisha kuwa kama huna bahati maishani huwezi kufanikiwa. Lakini pia watu wanaopenda starehe ni wa kuwaepuka. Watu wanaotanguliza starehe mbele na hawataki kufanya kazi. Sisemi kwamba starehe ni mbaya, kuna muda kweli unahitaji upumzike. Lakini starehe ikizidi inakuwa mbaya.Waepuke hawa watu kama kweli unataka kufanikiwa.

Waongo na wasio waaminifu.

Watu wako wa karibu wakiwa waongo ni hatari sana kwa mafanikio yako.Uongo matokeo yake unaweza usiyaone kwa muda mfupi.Ingawa Dunia ya sasa watu wakweli na waaminifu ni wachache lakini wapo, watafute na uambatane nao kwenye mafaniko yako. Unahitaji watu wakweli na watu wa kuwaamini katika safari yako ya mafanikio. Mtu ambae ukimpa kitu kufanya anakifanya kwa uaminifu. Unahitaji watu ambao wako tayari kukwambia ukweli hata kama unaumiza na sio watu wa kukwambia uongo ili ucheke.kumbuka mtu muongo atakupa taarifa za uongo na utazifanyia kazi na zitaisha kukukwamisha na kamwe hauwezi kufanikiwa kwa kutumia taariza za uongo.

Wabinafsi.

Watu hawa wanajijali wao tu, na hawawajali wengine. Wanaangalia kitu kitakachowanufaisha wao tu bila kuangalia kama kina madhara kwa wengine. Watu kama hawa wanapenda kupokea tu, hawapendi kutoa.Naomba nieleweke hapa, binadamu tumeumbwa na ubinafsi. Kila binadamu ana ubinafsi ndani yake. Lakini ninachoongelea hapa ni ubinafsi ulio na madhara kwa wengine. Yaani unakuta mtu yuko tayari kufanya kitu chochote ajinufaishe yeye tu bila kuangalia madhara kwa wengine. Watu kama hawa waepuke kwenye maisha yako. Watu kama hawa wanaweza wakawa na wewe kama rafiki kwa kukutumia tu wakamilishe haja zao. Wanachoangalia ni faida kwao tu. Watu kama hawa wanachukia sana wakiona wengine wanafanikiwa. Wanapenda wafanikiwe wao tu. Waweke pembeni watu hawa kwenye maisha yako, kwa sababu ukiwa nao watakutumia tu.

Watu wasio na malengo na maisha yao.

Hawa ni watu walioridhika na maisha na hawana ndoto yoyote na maisha yao. Watu hawa hawana malengo na maisha yao, wanaishi ilimuradi siku zimeenda.Watu kama hawa hawajisumbii kuwaza wafanye nini kubadili hali zao za maisha. Ni watu ambao wanakubaliana na hali zao za maisha na wanaamini ndivyo walivyo na wanaendelea kuishi hivyo kila siku. Rafiki watu wasio na malengo na maisha yao hawatakupa hamasa yoyote ya kwenda mbele. Na hawa wanaweza kugeuka na kuwa wakatishaji tamaa namba moja kwenye mafanikio yako.Watu kama hawa watakufanya na wewe uweke pembeni malengo yako na kukubaliana na hali uliyonayo hata kama ni mabaya. Na utaanza kusema maneno kama ‘haya ndio maisha’, ‘hivi ndivyo maisha yalivyo’, na wakati ungeweza kuisha maisha mazuri zaidi ya hayo. Waepuke watu hawa rafiki kama unataka kufanikiwa.

Watu wenye majivuno na wenye kiburi.

Hawa wanajiona wao ni bora sana kuliko wengine. Wanajiona wao wako juu kuliko wengine. Wanapenda kuwaona wengine wako chini yao siku zote. Wakifanikiwa basi mtaa mzima utajua. Watu hawa ukifanikiwa lazima waumie. Na siku zote wanaamini hakuna mtu aliye bora kuliko wao. Wanawashusha wengine ili wajione ni dhaifu kuliko wao. Kama kweli unataka kufanikiwa, waweke pembeni watu hawa rafiki.

Wakosoaji.

Hili ni kundi lingine la watu la kuwaepuka. Ndio kukosolewa kupo katika maisha. Tunahitaji kukosolewa ili tuwe bora wakati mwingine. Kama kuna kasoro mtu kaiona na kakwambia haina budi kuingalia na kuifanyikia kazi. Lakini kuna watu wao ni kukosoa tu, hakuna uzuri wowote wanao uona kwa mtu au kitu. Yaani watu kama hawa wanaangalia kasoro iko wapi siku zote. Hata ufanye vizuri kivipi watakukosoa tu. Hata kitu kiwe kizuri kivipi watatafuta kasoro iko wapi, utadhani wameumbwa kukosoa tu kwenye maisha yao.

“You are the average of the five people you spend the most time with”- Jim Rohn

mmassyfm@hotmail.com
 
Tutajie maendeleo yako Kwanza halafu ushauri wako ndo tuusikilize usikute na wewe ni kinyamkela
 
Jim Rohn
Brian Tracy
Zig zigler
Robert Kiyosaki

Wamepata Pesa mingi kwa kuandika haya.

Duniani unaweza kutajirika kwa Kutoa taarifa kuhusu kutajirika.

Komaa Mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom