Aina za wanawake na tabia zao

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
8,378
12,573
1. Mommy Types
Ni aina ya wasichana au wanawake ambao huonyesha tabia ya umama. Hupenda kujali kupita kiasi. Mfano katika mahusiano usipomtumia ujumbe wa kufika sehemu uliyomwambia unaenda tarajia kupokea simu zisizopungua 10.

2. The Listener
Ni aina ya wasichana au wanawake inayopendwa na wanaume wengi zaidi Duniani. wapole wenye nidhamu, wanyenyekevu na huonekana kujali sana. Huwa niwasikilizaji bila kuhukumu au kuwa na usumbufu wowote katika mazungumzo yao.

Katika mahusiano huonekana ni wakimya sana ikiwa hawatapewa nafasi ya kuzungumza, na niwatunzaji wa matukio. siku ukitokea ugomvi na akapata nafasi ya kuongea atapanga mtiririko wa matukio yote na ikiwa ugomvi ni mkubwa, wako tayari kuvunja mahusiano au kufanya jambo lolote baya.

3.Superwomen
Ni aina ya wasichana au wanawake ambayo huwa ni wagumu kwa asili yao. Vipaumbele vyao wakati wote huwa ni malengo yao. Wanafanya kazi kwa bidii. Na huwa ni wagumu sana kukueleza kile wanachopitia. Hupenda sana kuungwa mkono maamuzi yao. Hawapendi kuhukumiwa au kutiliwa mashaka. Wanapenda kujitegemea zaidi.

Huwa na mihemko sana katika ufanyaji wa mambo yao kwahiyo hukoswa utulivu. Huficha hisia zao. Ikiwa umepata mtu wa aina hii katika mahusiano inahitajika kuwa mwangalifu sana juu ya matendo yao kwa sababu haijalishi ana nguvu kiasi gani, wao wanahitaji mtu wa kuwaangalia sana.

4. Ms. Perfectionist
Ni aina ya wasichana au wanawake wanaopenda kufanya mambo yao kwa uzuri na umakini mkubwa.
Wanapenda kutii kanuni na taratibu kulingana na mazingira waliyopo. Niwenye nidhamu, hupenda usafi na kupangilia vitu vyao katika ubora. Hawapendi kukosolewa, hupenda kusapotiwa na kusifiwa katika kila kitu wanachokifanya. Katika mahusiano huwa ni wazuri ikiwa utaendana nao, lakini huwa niwasumbufu ikiwa utakuwa kinyume nao.

5. Panda girl's
Ni aina ya wasichana au wanawake ambao huwa wavivu sana. Hupenda maisha ya starehe yasiyochosha miili yao. Hupenda kufanyiwa kila kitu. Ni ving'ang'anizi sana ikiwa watataka kitu wanapenda wakipate kwa huohuo mda katika mahusiano.

Hupenda maisha ya bata sana, na niwasumbufu hupenda kila muda waoonekane usoni mwa mwanaume waliyenaye katika mahusiano. Ikiwa huna TV basi wao ndiyo huonekana kama video mbele yako. Ni aina ya wanawake ambao wanauwezo wa kumtengenezea mwanaume ratiba ya maisha yake kutokana na mihemko yao.

6. Boss lady
Nia aina ya wanawake hodari, huru na wasioogopa kusema mawazo yao. Wana ndoto kubwa ni waongeaji na hupenda kutetea haki zao. Ni wanawake wenye ujuzi na huonekana jasiri kupitia mafanikio yao.

waaminifu, hupenda mamlaka, na hupenda kujitegemea. Katika mahusiano hupenda kumiliki na kuongoza kila kitu. Wanapenda kuongoza kwani hujiona ni wenye mamlaka.

Huwa hawana hofu huamini wanaume na wanawake wana uwezo sawa wa kuongoza na kunyakua kila fursa.
Hawapendi kushughulikiwa kama watu wa kawaida (wabinafsi sana). Huwa wanajua nafasi zao ziko juu hivyo watakupiga vita ikiwa utaingilia malengo yao.

7. Drama Queen
Ni aina ya wasichana au wanawake ambao hupenda kuzidisha hali walizopewa iwe ni katika maumbile yao au katika maisha yao ya kila siku. Hupenda kucopy sana kila kitu katika kila watakachokiona, huwa sio wabunifu. Wanapenda kujaliwa sana na hupenda kuwa tegemezi hata kama wanaweza kujitegemea wao wenyewe.

Katika mahusiano huwa ni kinyume cha panda girls, wanapenda muda wao mwingi wawe chini ya uangalizi wa mwanaume. Huwa hawapendi waume zao waonekana na wanawake wengine hata kama awe ni rafiki wa kawaida. Wana wivu mkubwa sana katika mahusiano.

8. The Nerd
Ni aina ya wanawake wenye akili, wenye ufahamua na wanaojifunza mambo mbalimbali. Hupenda maisha yao binafsi hawapendi maisha ya kuigiza.

Huwa ni wenye malengo wanayoyatamani kuyafikia, katika mahusiano utapata wakati wao ikiwa watamaliza masomo yao au kufikia malengo yao. Ni wenye ushawishi mkubwa ni wenye marafiki wengi. Hawapendi kusifiwa na kuonekana tofauti na wanawake wengine, hupenda kuonekana wenye ukawaida.

9. The guy's girls
Ni aina ya wasichana au wanawake ambao hupenda zaidi ushirika na wanaume. Hupendelea kufanya mambo ya kiume na wakati mwingine kuonekana katika mwonekano wa uanaume. Huwa ni wenye malengo na mipango mikubwa sana.

Huwa niwenye nguvu ya ushawishi ikiwa atakuwa na jambo lake lazima atahakikisha linafanyika. Huonekana kuwa niwenye ndoto kubwa kupitia mawazo yao. Katika mahusiano ni mara chache kutazama urafiki wake na wanaume katika mambo ya kimapenzi. Anaweza kuwa na mpenzi ambaye wanashiriki naye mara moja na kwa wakati, wanajulikana pia kama Tom-boy.

10.The Fashionista
Ni aina ya wanawake ambao niwabunifu sana na wanamitindo. Huonekana vizuri wakati wote, kama siyo kumpenda basi lazima utamtamani tuu wakati utakapokutana naye. Wanajua bidhaa gani ni toleo jipya.
Mavazi yake yaweza kuwa ni ya bei rahisi lakini ni wanawake wanaojua kupangilia sana. Ni wanawake wenye mizunguko sana, wanapenda kusafiri na hupendelea kuonekana katika kila sherehe.
 
Nilipata kidemu ki Listener lakini hakikuwa na mwonekano mzuri ,ni kakipotezea,alikuwa ni mwanamke ambae haniulizi maswali sjui uko wapi,sjui ulikuwa wap,sjui unaenda wapi,

Siku akiniuliza nikimkumbatia tu maswali yake yote yanayeyuka na anasamehe kila kitu

Sasa baada ya kuachana nae nikadumbukia kwa Panda girl aisee ni familia ndo imeniokoa baada ya kuingilia kati kuokoa jahazi na nasema nimekoma

Hata hivyo niko nampango wa kumtafuta LISTENER wangu nimfanyie kitu fulani kizuri kama kulipa fadhila
 
Nilipata kidemu ki Listener lakini hakikuwa na mwonekano mzuri ,ni kakipotezea,alikuwa ni mwanamke ambae haniulizi maswali sjui uko wapi,sjui ulikuwa wap,sjui unaenda wapi,

Siku akiniuliza nikimkumbatia tu maswali yake yote yanayeyuka na anasamehe kila kitu

Sasa baada ya kuachana nae nikadumbukia kwa Panda girl aisee ni familia ndo imeniokoa baada ya kuingilia kati kuokoa jahazi na nasema nimekoma

Hata hivyo niko nampango wa kumtafuta LISTENER wangu nimfanyie kitu fulani kizuri kama kulipa fadhila
Barikiwa sana ....huyo ndo alikuwa sahihi kwako
 
Ilikuwaje mkuu?
Kwanza alijifanya ananipenda kuliko pitiliza,anagombana na kila mtu eti kwasababu yangu,hataki niwe nawasikiliza hata wazazi wangu,yaan alipenda nimsikilize yeye tu
Alinifanya pia nikawa na matumizi makubwa ya kipesa wakati huo naendesha miradi ya familia
Pia alianzisha tabia za kufanya vitendo vya kujitoa uhai pale anapohis niko na wanawake wengine
 
Kwanza alijifanya ananipenda kuliko pitiliza,anagombana na kila mtu eti kwasababu yangu,hataki niwe nawasikiliza hata wazazi wangu,yaan alipenda nimsikilize yeye tu
Alinifanya pia nikawa na matumizi makubwa ya kipesa wakati huo naendesha miradi ya familia
Pia alianzisha tabia za kufanya vitendo vya kujitoa uhai pale anapohis niko na wanawake wengine
Na hapo unakuwa kama umelogwa, unafata anachokwambia
 
Na hapo unakuwa kama umelogwa, unafata anachokwambia
Kuna wajinga walikuwa wanaamin hivyo wakat sio,mara nying nilkuwa namkazia pale anapotaka kunipeleka kiboya,mara nyingi kalikuwa kanalia mpaka nakahurumia
 
Back
Top Bottom