Aina za majini na kazi zake

Aina za majini na kazi zake

Habari zenu wakuu. Niende kwenye mada husika
Kwa wale wajuzi wanaoelewa juu ya jini mahaba nahitaji kufahamu jini huyu anaingia kwa mtu wa aina au sifa zipi na anasababisha madhara yapi kwa muhusika?
Asanteni.
Mshana Jr nifafanulie hapo
 
Mshana Jr nifafanulie hapo
Jini makhaba huwa kwanza anachagua watu wa kuwaingilia, ni mapenzi na hulka binafsi kama vya mwingine yoyote... Yaani utamanifu wa kawaida wa mwanaume
Mara nyingi hupenda kuingilia mwanamke nyakati za usiku ndotoni... Yani utahisi ni ndoto lakini ukiamka utajikuta tayari kikwelikweli
Madhara yake ni makubwa kwakuwa huwezi kudumu kwenye mahusiano hasa jini likikupenda kabisa., au utakuwa hupendi kuwa na mahusiano na wanadamu na sometimes unakuwa na ukorofi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani Mungu aliyatupa duniani yatutese? Ni vitu vya kufikirika tu, hekaya za Abunuasi.Labda kwa kuwa uchawi haionekani na upo basi kwa kusuasua huenda majini yapo
e

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jini makhaba huwa kwanza anachagua watu wa kuwaingilia, ni mapenzi na hulka binafsi kama vya mwingine yoyote... Yaani utamanifu wa kawaida wa mwanaume
Mara nyingi hupenda kuingilia mwanamke nyakati za usiku ndotoni... Yani utahisi ni ndoto lakini ukiamka utajikuta tayari kikwelikweli
Madhara yake ni makubwa kwakuwa huwezi kudumu kwenye mahusiano hasa jini likikupenda kabisa., au utakuwa hupendi kuwa na mahusiano na wanadamu na sometimes unakuwa na ukorofi

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah! Hili jambo limenigharimu sana aisee. Mungu anisaidie
 
Ila najua njia rahisi ni kusali sana kuomba ulinzi wa Roho Mtakatifu na Mama Bikira Maria ili haya mavitu yakae mbali na binadamu kwani ni uharibifu mtupu mbele ya Mola wetu.
 
Hakuna haja tena ya kutoa tafsiri ya majini kwakuwa tayari tumeshalidajili hili kwenye post iliyopita kwamba majini ni viumbe roho waliofukuzwa toka mbinguni na kutupwa ulimwengu wa giza.

Mada hii ni maalum kwa ajili ya kutambua aina za majini na kazi zake
Kuna wakati katika jamii unaweza kumshangaa mtu au hata kugombana naye kutokana na tabia zake na mambo yake huyu si wa kulaumu sana saa nyingine si yeye bali ni jini, hata hapa JF tunao wengi tuu.

Kimsimgi wapo majini tofauti tofauti zaidi ya 60 lakini kazi zao kwa sehemu kubwa zinaingiliana hivyo nitaweka baadhi tu ambayo kwa kiasi kikubwa ndio hubeba mambo mengi fuatana nami.

1. SUBIANI - hili ni jini linalosababisha ajali na lenye kuzuia hedhi kwa mwanamke, lina penda sana damu hasa hiyo ya hedhi.

View attachment 342303

2.MURAFARI- hili ni jini la kuzuia mafanikio ya kimaisha kielimu na hata kipato, ukitupiwa hili jini utahangaika sana na maisha.

3.LATIFU- jini la mateso ufukara na matumizi ya hovyo unakuwa ni mtumwa wa kupata kupoteza na kutumia bila tija.

4.JAHARI-jini jizi la biashara, unafanya Sana biashara lakini huoni ustawi wala mafanikio yoyote.

View attachment 342305

5.HASINANI- Jini la fujo ulevi wa kila aina bhangi sigara madawa pombe nk

6.JUBE- Jini la utasa, hili unaweza kutupiwa tu na mbaya wako au ukiwa mtoa mimba au mpiga puchu mahiri.

7.RUYATI- ndoto mbaya, ukiacha ndoto maono au ndoto ujumbe , hizi ndoto za kutisha husababishwa na jini ruyati.

8.TAJARUNI-hili ni la utajiri wa masharti ya kutoa kafara la ndugu na kufanya ngono na mzazi au mwanao.

9. WAIDADAT- jini linalomfanya mwanaume aige mambo yote ya kike kuanzia tabia mpaka mavazi.

View attachment 342307

10. ALIBADIRI- Ukitupiwa hili kwa sababu yoyote ile hasa kutenda uovu huponi.

11.ANZURA -kuzuia ndoa hasa kwa wanawake, utakuta binti mzuri kakamilika kila idara lakini anaishia kuposwa tuu.

12.MAIMUNA- jini mfarakano wa kuleta magomvi kwenye ndoa hatimaye kuvunjika.

13 . MAKATA- Jini makata ni noma hili likiingia kwenye familia au ukoo basi vifo vitafululiza mpaka mbaki wachache kabisa.

View attachment 342306

14.TARIK- jini hili hufarakanisha marafiki watu wanaofanya biashara pamoja kwenye vyama nk nk..likishaingia mahali hili lazima kinuke.

15. JINI WIVU KIJICHO NA ROHO YA KWANINI-hili bwana hili popote litakapoona new post ni mtu fulani sikilizia mashambulizi yatakayofuata.

[emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Katika mambo yote hayo hakuna jini lolote linalofaidika na chochote bali kumletea shida mwanadamu ili afarakane na mola wake
Kumbuka kuna majini ya kutupiwa kutumwa na yale yanayofanya kazi yenyewe kwa utashi wao.

==========================
NB: Picha zimewekwa ili kuleta uhalisia zaidi ingwa zinaweza zilihusiane moja kwa moja na Majina ya viumbe hawa.
Mshana asante kwa taarifa hii,ila itakuwa busara kama utamaliza assignment yako to 99,maana nasikia idadi ya koo za majini ni 99.

Halafu Mshana naomba ufafanuzi,hivi kuna siri gani katika namba 9 au 6,maana Dajjal naye namba yake ni 666,na naona makampuni ya simu nayo siku hizi yanatumia sana namba 9 au 6.Kwa mfano,Vodacom,*149*99#,*149*66#.Vodacom hiyo hiyo ukicheki kwa makini utagundua kwamba logo yao ni 6.Airtel wana kifurishi cha Sh.1,999 na hata wao ukicheki logo yao utagundua kwamba ni 9 ya kuzuga.Infact hata kwenye international companies trend hii ipo sana.Kwa nini so much of 9 and 6 and not the other numbers and why now.Karibu Mshana tafadhali nisaidie.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom