Aina za hasira za Wanawake na vituko vyao

Aina za hasira za Wanawake na vituko vyao

i see me in number 2 and 3, huyu mkuu mbona mutu yake iko kama mimi?

hahahahah sometimes sauti inaisha kabisa and i can not talk at all

but this happens to me very rarely as i have decided to be happy all of my time life no matter what
Nataka nijaribu nijionee kuja huku toto..
 
Hahahahaaa mi hapo nimekutana na woote isipokua ya mtu mpka kuanza kubleed mmhh...ni mpyaaa.
 
Hizo sifa zote zimetua kwa wife wangu peke yake maombi yenu muhimu jamani
 
Habari wakuu,

Kuna aina za hasira za wanawake hasa wanapoudhiwa na wapendwa wao. Ukishaona kakasira muache, hasira zikiisha mambo yatakuwa poa. Muhimu umjue hasira zake zilivyo. Mi wangu ananuna wiki nzima inaweza isha, yupo namba tatu[emoji23][emoji23][emoji23]. Nacheka sana akinuna.. Ila wengine sasa:

1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu!

2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere!

3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra!

4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata!

5. Wako wanawake ambao, akichukia, Atakachokishika usipokimbia anakutandika na anaweza kukuchoma na kisu,, majuto baadaye!

6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia/ ndoa na waume zao!

7. Mwanamke mwingine akikasirika, Mtajuana kitandani panapo usiku, Nakwambia utaungama yoote!

8. Kuna wengine wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka!

9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika!

10. Wengine wakichukia, wanaamua kwenda kulala kimyaaa!!

11. Wanawake wengine wakikasirika, tumbo linakata, na pengine mpaka wanaharisha!

13. Wako ambao wakishikwa na hasira, huingia kwenye maombi na kuugua kusikoweza kutamkwa. Uchungu ukiisha, wananawa uso na kwenda sokoni.

14. Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka saaanaaa.... Hutajua kama amekasirika! Dizaini hii ni hatari sana, maana anaweza kukudhuru kiurahisi.

WEE UKO KUNDI GANI AU MKEO YUKOJE??
Hiyo namba Tisa ndo wife wangu anayo! Hapiki week mbili nzima hapo msichana wa kazi ndo anahudika mambo yote ya jikoni na ushoga na house girl ndo zinazidi
 
Yote baridi, moto ni pale anakupa, kabla maji hayajachemka, anasema toa sitaki.
 
demu wangu akikasirika anakuwa mhongo mhongo sana
 
Back
Top Bottom