Aina za hasira za Wanawake na vituko vyao

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,172
Reaction score
64,535
Habari wakuu,

Kuna aina za hasira za wanawake hasa wanapoudhiwa na wapendwa wao. Ukishaona kakasira muache, hasira zikiisha mambo yatakuwa poa. Muhimu umjue hasira zake zilivyo. Mi wangu ananuna wiki nzima inaweza isha, yupo namba tatu[emoji23][emoji23][emoji23]. Nacheka sana akinuna.. Ila wengine sasa:

1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu!

2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere!

3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra!

4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata!

5. Wako wanawake ambao, akichukia, Atakachokishika usipokimbia anakutandika na anaweza kukuchoma na kisu,, majuto baadaye!

6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia/ ndoa na waume zao!

7. Mwanamke mwingine akikasirika, Mtajuana kitandani panapo usiku, Nakwambia utaungama yoote!

8. Kuna wengine wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka!

9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika!

10. Wengine wakichukia, wanaamua kwenda kulala kimyaaa!!

11. Wanawake wengine wakikasirika, tumbo linakata, na pengine mpaka wanaharisha!

13. Wako ambao wakishikwa na hasira, huingia kwenye maombi na kuugua kusikoweza kutamkwa. Uchungu ukiisha, wananawa uso na kwenda sokoni.

14. Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka saaanaaa.... Hutajua kama amekasirika! Dizaini hii ni hatari sana, maana anaweza kukudhuru kiurahisi.

WEE UKO KUNDI GANI AU MKEO YUKOJE??
 
Habari wakuu,

Kuna aina za hasira za wanawake hasa wanapudhiwa na wapendwa wao. Ukishaona kakasira muache, hasira zikiisha mambo yatakuwa poa. Muhimu umjue hasira zake ziluvyo. Mi wangu ananuna wiki wiki nzima yupo namba tatu[emoji23][emoji23][emoji23]. Nacheka sana akinuna.. Ila wengine sasa:

1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu!

2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere!

3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra!

4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata!

5. Wako wanawake ambao, akichukia, Atakachokishika usipokimbia anakutandika na anaweza kukuchoma na kisu,, majuto baadaye!

6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia/ ndoa na waume zao!

7. Mwanamke mwingine akikasirika, Mtajuana kitandani panapo usiku, Nakwambia utaungama yoote!

8. Kuna wengine wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka!

9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika!

10. Wengine wakichukia, wanaamua kwenda kulala kimyaaa!!

11. Wanawake wengine wakikasirika, tumbo linakata, na pengine mpaka wanaharisha!

13. Wako ambao wakishikwa na hasira, huingia kwenye maombi na kuugua kusikoweza kutamkwa. Uchungu ukiisha, wananawa uso na kwenda sokoni.

14. Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka saaanaaa.... Hutajua kama amekasirika! Dizaini hii ni hatari sana, maana anaweza kukudhuru kiurahisi.

WEE UKO KUNDI GANI AU MKEO YUKOJE??
15: Wakikasirika wanawaita wenzi wao vibamia...
16. Wakikasirika wanawaita wanaume "wanaume wa Dar" (wanawake wa aina hii wako wengi sana hapa JF)
 
Habari wakuu,

Kuna aina za hasira za wanawake hasa wanapudhiwa na wapendwa wao. Ukishaona kakasira muache, hasira zikiisha mambo yatakuwa poa. Muhimu umjue hasira zake ziluvyo. Mi wangu ananuna wiki wiki nzima yupo namba tatu[emoji23][emoji23][emoji23]. Nacheka sana akinuna.. Ila wengine

3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra!
Madame S

hapo red babe nimecheka vibaya daah
 
Ndo hasira za wifi hizo!![emoji85] [emoji85] [emoji85]
Ila nyie wanawake....
Siku nimejua tupo tofauti saana ni kipindi naanza kukua.

Nilikaa na mshkaji alikuwa na Mwanamke wake. Sasa huyo mwanamke anakaa mji tofautu na sisi. Akija kututembelea anakuta nimelala.

Anakasirika hatari.. Daby hakutaka nije. Daby hanipendi...Sasa mimi nikusubiri nisilale nikusalimie tu? kwa mwanamke hili ni kubwa saana ila wanaume waala.
 
Back
Top Bottom