Aina za Adhabu Ambazo Hutolewa Mahakamani

Apr 26, 2022
59
94
Utaratibu ni kwamba, mtuhumiwa akishatiwa hatiani, kipengele kinachofuata (after mitigation) ni kupewa adhabu.

Sasa adhabu ziko nyingi; inaweza kuwa kifungo gerezani, kulipa faini, kutaifisha mali/kitu, kuchapwa viboko, kuhukumiwa kifo au kulipa fidia, n.k

Kwa Tanzania, adhabu za makosa mbalimbali zimetajwa kwenye Sheria inayoitwa Kanuni ya Adhabu (Penal Code), 📕 lakini kuna adhabu zingine zinapatikana kwenye sheria zingine mbali mbali. 📚

KUNA AINA KUU MBILI ZA ADHABU

1: Discretionary Sentences. 👌 Unakuta sheria haijaweka wazi adhabu moja ya lazima kwa kosa husika, ila hutegemea na busara za Mahakama.

Hizi ni adhabu ambazo Sheria imeipa Mahakama uwanja mpana wa kutoa adhabu hadi kiwango fulani, mfano adhabu ya kuua bila kukusudia ( manslaughter) Mahakama inaweza kutoa adhabu yoyote, lakini adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha.

2: Mandatory sentences. (Ambapo sheria imeshataja kabisa adhabu moja ya lazima). Mandatory sentences ipo kwenye yale makosa ambayo adhabu yake ni moja tu, imeshatajwa kwenye sheria kwa hiyo Mahakama haiwezi kuamua vinginevyo. Mfano adhabu ya kosa la mauaji ya kukusudia (murder) ni kifo.

Lengo la sheria kulazimisha adhabu iwe moja tu kwenye makosa fulani fulani ni; 👇

- Kuzuia Matumizi mabaya ya uhuru/busara za mahakama kwenye kujiamulia adhabu.

- Kuepusha kutofautiana adhabu kwa watu waliotiwa hatiani kwa makosa yanayofanana.

- Kuwaweka kizuizini wahalifu ambao wamekuwa au wanaonekana tishio kwenye jamii kwa muda mrefu.

- Kuzuia kushamiri kwa baadhi ya maovu katika jamii mfano makosa ya kingono n.k

Je, ikitokea sheria haijataja adhabu ya kosa fulani, Mahakama itafanyaje?

Kama kosa kwenye sheria halijawekewa adhabu yake, Mahakama itatumia “common law” na kumpa mhalifu adhabu ya kifungo au faini kama itakavyoona inafaa, lakini hiyo adhabu isiwe iliyopitiliza. (Kwa wasio na elimu ya sheria, common law ni maamuzi ya Mahakama za nje - England huko - hutumika kukiwa na gap (loophole/lacunae/mapungufu) kwenye Sheria za ndani).

Soma kesi ya Jamhuri v. Emmanuel Timothy [1980] T.L.R 115.

Imeletwa kwako nami Zakaria.
(0754575246 - WhatsApp).
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom