Aina ya Viongozi wa Umma kama Peter Serukamba ni Janga la kitaifa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aina ya Viongozi wa Umma kama Peter Serukamba ni Janga la kitaifa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yericko Nyerere, Feb 14, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,244
  Likes Received: 3,787
  Trophy Points: 280
  Peter Serukamba ni mbunge wa Kigoma Ujiji,na ni mjumbe wa NEC ya CCM, ni krimu ya siasa za Kijani na ni sura ya Ujana ya CCM,

  Wakati taifa na wanamageuzi kwa ujumla wakipambana kukemea ukwasi tata wa Bunge letu chini ya Mama Makinda aka Bibi Kiroboto, Serukamba kupitia mtandao wa kijamii wa twita @serukamba bila haya wala kihoro, apambana waziwazi na wapinga posho kwa kusema "Kama Bunge haliongezi POSHO basi Bunge lifutwe!

  Kwa maneno hayo tu, mimi binafsi namuona ni janga la kitaifa na lisiposhughulikiwa litaliangamiza taifa!
  Kumbuka kila aliye mtz na alipae kodi ya haki basi kodi hiyo hutumiwa ikiwa ni pamoja na kuwalipa posho za kukaa bungeni wabunge na watumishi wengine, hivyo dhana ya Serukamba kuwa wengi wawanaopiga ukelele wa kupinga posha hasa kwake yeye hawamsaidii kwani hawakumchagua na hawatamchagua!
   
 2. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Njaa zinamsumbua kilaza tu
   
 3. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hakuna mbunge wa ccm ambaye hashabikii posho,kwao hawana mpango na mlala hoi kwani wanapaswa kufanya kazi walizotumwa na wananchi wao.Na wala hawakutumwa kwenda kudai posho, hayo ni mawazo binafsi ambayo hayawasaidii wapiga kura.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lakini mkuu wangu yeye ni mwana CCM umesema mwenyewe na ndicho wanachokisimamia kwa wingi zaidi wakijua posho ndizo zitakazo warudisha bungeni ktk kufanyia kampeni. Wao hawafikirii wewe mwananchi isipokuwa maslahi yao wenyewe kurudi mjengoni kwa kutumia Takrima..
   
 5. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Peter sio ndio petro....nadhani mtandao wao unahesabika siku zake za kuchuma
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu Mkandara umesema ukweli mtupu na hasa ukichukulia matokeo tata na nguvu za dola zilizotumika kumtangaza Serukamba kama mbunge wa Kigoma Mjini haishangazi anapoandika maneno kama hayo ya kutetea posho. Wabunge wa aina yake wapo wengi bungeni.
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,244
  Likes Received: 3,787
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuna kilicho nyuma ya pazia hapo? Hebu pembua bila mawaa!
   
 8. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Serukamba ni mtu asiyekuwa na msimamo; ni bodyguard wa Lowassa na ndiko anakopata fedha nyingi za kuhonga ili agenda za Lowassa ziweze kufanikiwa!!
   
 9. King2

  King2 JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Bila kumsahau Ndugai, na makinda
   
 10. M

  Mohamed Ibrahim Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi huu kweli wana jamii tunapoteza muda wa kumjadili huyu mcameroon
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli hakuna anayeridhika ktk suala zima la hela
   
 12. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  wewe unategemea nini kwa mtu ambaye kura kapigiwa na 98% darasa la saba? tena hawana kazi!
   
 13. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,244
  Likes Received: 3,787
  Trophy Points: 280
  Unamaanisha kuwa idadi ya wapiga kura wake 98% ni elimu zao ni darasa la saba?
  Haijalishi kapigiwa kura nanani, jambo la muhimu kama watz wazalendo, tumkatae na tukipaza sauti zetu, wale 98% waliompiga kura wataamka na kumkataa!
  Tufanye hivyo kwa vitendo!
   
 14. C

  Christiano Ronaldo JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata kama mimi si mbunge naweza kuunga mkono suala la wabunge kulipwa vizuri zaidi (si lazima kwa njia ya posho ya vikao). Nianze kwa mambo mawili: Kwanza, kwa jinsi nilivyofuatilia suala hili, si kweli kwamba wabunge wanaoshabikia posho ni wa CCM tu. Asilimia 90 ya wabunge wa Chadema wanataka sana hizo posho, isipokuwa wengi wao wanawaogopa kama chui viongozi wao wakuu wanaopinga posho hizi. Pili, kusema kwamba wabunge wakafanye kazi walizotumwa na wapigakura wao, badala ya kudai posho ni kutojua kwamba wabunge hawana job description maalum ya kazi zao. Wabunge hawa wakishachaguliwa, kila jambo jimboni kwao ni kazi yao - kuanzia ufuatiliaji wa utekelezaji wa ahadi za serikali na za kwao wenyewe, kufuatilia kero za wananchi za aina yoyote ile, kusaidia wananchi kwa shida zao za kijamii (kama michango kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi, ujenzi na misaada ya makanisani na misikitini, misaada ya michezo na burudani) na shida binafsi za wananchi kama magonjwa, elimu ya watoto, michango ya misiba na harusi. Nilivyofuatilia wabunge wote wanaopinga posho hizi (kutoka CCM na upinzani) ni wale wabunge matajiri na wafanyabiashara kama vile Mbowe, Mohamed Dewji, Mkono, Ndensamburo n.k. na pia wabunge wanaopata misaada kwenye NGOs zao kama vile Zitto anayepata hela nyingi toka kwa wafadhili (Ujerumani) na chinichini kutoka kwa viongozi wa mashirika ya Umma wanaomwogopa kama mkt wa POAC, na wengine wenye NGOs kama January n.k. Hawa wana vyanzo vizuri tu vya kuhudumia majimbo yao kwa shida zote za wananchi. Lakini kwa wabunge wanaotegemea malipo ya Bunge tu wana hali mbaya sana. Na bahati mbaya, wananchi na viongozi wa dini mnaolaumu suala la posho ndio wa kwanza kuleta kadi za michango kwa wabunge. Mimi ningependekeza kwamba badala ya posho, wabunge wangelipwa tu mishahara mikubwa kama milioni kumi kwa mwezi. wala sitaweza kuwaonea wivu hata kama mimi mshahara wangu ni kiduchu. Wana majukumu makubwa. Wala simlaumu Serukamba kwa msimamo wake huo.
   
 15. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  MOJA YA HARAKATI ZIDI YA SEREKAMBA NI HII HAPA......... NOW WE ARE GOING PERSONAL TO SEND AM MESSAGE...... HII YA KURUSHA MAWE KWA CHAMA CHOTE HAYAFIKI VIZURI...... LET'S VICTIMIZE .....
  SOMA JIELIMISHE
  Jana naibu spika wa Bunge alitangaza kwamba wabunge hawatolipwa posho mpya [Sh 330,OOO kwa kalio kwa siku ] ni kutokana kwamba Raisi hakuruhusu ongezeko la Posho za wabunge, pia alisema posho hizo azijawahi kulipwa .....[kauli inayopinga na kauli ya makinda na Pinda ] ... hii ni habari Njema kwamba hakuna posho mpya kwa sasa.
  Haya ni matunda ya wananchi/wenyenchi kupiga kelele kupitia vyombo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mitandano ya kijamii [facebook, blog na twitter ] .Kutoka na maamuzi hayo ......kumezuka jambo kwenye mitandao ya kijamii nilikuta mbunge wa UJIJI [ CCM ] Ndg Serukamba akiwa kawati wakati mgumu kwenye mtandao wa twiiter kupitia account yake ya [ @serukamba ]
  Serukamba ni moja ya wabunge mashabiki wa posho..... Huyu ni mbunge aliyefikia hatua ya kusema kama hakuna ongezeko la posho basi bunge livunje [ tusiwe na bunge ] ...ili maneni waongezewe mishahara [kauli kama hiyo ni kejeri kwa manesi maana anajua lazima bunge liwepo hivyo manesi je? ]
  ....... kauli yake nyingi ni >>>>amesaidia sana wananchi na sio kazi yake... hivyo posho ziongezwa kuziba hayo mapengo [kwa nini anafanya shughuli zisizo za mbunge, lakini pia kasaidia kwa malengo yapi? Kwa vigezo vipi? ]...... alienda mbali zaidi na >>>kusema kwamba kama watu wengine wanaweza kuishi bila UBUNGE na yeye anaweza kuishi kwa kufanya kazi nyingine maana amesoma [ hii ni kauli ya kudumu ya baadhi ya wabunge pindi wanapoficha uchwara wao].........lakini leo baada ya kubanwa kwa nini hasiachane na kazi hii ngumu na ya hasara [ ubunge] alikuja juu na kusema watoa hoja wanamchukia tu........ Mbunge huyo akuihishi hapo apia alisema hata kama anapigwa vita kwa kutetea posho lakini mungu atamsaidia na kushinda tena uchaguzi 2015 [ kumbe bado anataka kufanya kazi ya kugawa pesa yake?].....kauli hiyo ni baada ya kampeni maalumu iliyo anzishwa ya .......#KataaSerukamba kutokana na sifa za kutetea faida zake binafsi badala ya jimbo......... wenzetu wa TWITTER wamedhamilia kumpiga vita ili iwe mfano....... kutoka na umuhimu wa hii kampeni leo na mimi nasema ....#KataaSerukamba ...... kama walivyotuumiza bungeni kwa kutuita sisi wananchi ombaomba hivyo wanataka posho zaidi sasa ile kwao, lakini pia kwa kwenda kutetea maslahi binafsi bunge, basi leo na sisi tung'oe mbunge mmoja mmoja asiye faa........... wana UJIJI ni hakika watasikia kio cha watanzania. [ kuna kipindi mototo SARAH lilikuwa jina kuwakilisha mototo wa kike na mateso ya kuendelezwa kijamii .... leo tupige kampeni ..#KataaSerukamba ikiwa na maana tunapinga kunyonywa] ... biashara ya watu kuwa KUPE kwa kisingizio chochote katika jamii ipingwe vita ....... Watanzania atuwezi kufanya kazi kwa bidii kisha tulipe kodi na kumpa mbunge akajitanue kisiasa [ vipi sisi tunaokwenda likizo vijijini na kusaidia ndugu na jamaa na mafariki tukaombe POSHO serikalini pia?] ..... tabia ya kuomba haina kikomo, ni asili ya baadhi ya watu [ hata bar wapo ].... serikali iliwakamata kina matonya kama kuku iweje leo iwape wabunge hela kwa ajili ya omba omba? ..... kwa nini mbunge atete hiyo.......
  Ndugu #KataaSerukamba ni kiwakirishi cha wabunge wa aina yake ..[ #KataaSerukamba ni kiwakilishi kama Sarah na KAYUMBA kwenye harakati za kielimu ...... tuwapige vita na STAMP yetu iwe ....#KataaSerukamba....... kila mtu kwenye WALL naomba Muanzishi hii kampeni..... #KataaSerukamba ili isikike nchi nzima na maeneo ambayo wana wabunge kama yeye bia watapata ujumbe na kuwapiga vita wabunge wasio fanyakazi zao ipasavyo, hali wakisubilia kuwagawia hela............ siku zote kwenye vita tafuta kiongozi wa vita upande wa maadui, kisha lenga kiongozi..... wanajeshi waliobaki watajisalimisha tu.... na wakiendelea na vita watakuwa tayari wamevurugika.......... tulisema sasa ni wakati wa kutenda.....tuanze na ili kila mtu na apige kelele ...#KataaSerukamba.........
  Tusikubali kufuga kupe kwenye jamii yetu, watatumaliza, wanatabia ya kula mpaka wanakufa, tutakufa nao.
   
 16. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kelele kuhusu mafisadi zilipoanza walikuwa wakicheka [ wakimcheka Dr slaa ] lakini leo ufisadi unaitafuta ccm....... hiii ni mwanzo mwisho lazima tung'oe hata mmoja wa hao kupe
   
 17. +255

  +255 JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Mpu..zi sana kutoongezwa posho ndo sababu ya bunge kufutwa, si akatafute kazi nyingine ya kufanya ka ubunge haumlipi..
   
 18. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  unauhakika gani kama hiyo akounti ya twitter ni yake? Anaitumia yeye mwenyewe?
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Posho ni janga la Taifa. Mimi nafahamu kwamba kuna Mbunge Mmoja tu ambaye amezikataa posho za vikao naye ni ZZK wa CDM. Hakuna mbunge mwingine (labda January wa CCM) ambaye amezikataa posho. Watu wanaongea kinafiki tu kwamba posho za vikao hatuzitaki na ni sera yetu kuzikataa lakini hawaonyeshi kwa vitendo. Suala la posho limejaa unafiki mwingi sana. Afadhali hata huyo Serukamba na Shibuda wanaonyesha misimamo yao hadharani kwamba wanazitaka na ziongezwe kuliko wanafiki ambao wanajifanya hawazitaki eti ni sera ya chama lakini wanazila. Mimi ningefurahi sana kama wabunge wote wa CDM wangesusia posho kama Zitto ili kutekeleza hiyo sera yao, lakini wapi linapofika suala la posho wabunge wengi wa CDM wanakuwa wanafiki wakubwa. Jamani kama ni sera ya CDM si utolewe uamuzi wa chama kwamba hakuna kuchukua posho kwa kuwa hiko ni kuwaibia wananchi na atayechukua posho anafutwa chamani. Lakini kwa kuwa wengi ni pro posho, uamuzi kama huo hauwezi kufikiwa. POSHO NI JANGA LA TAIFA NDANI YA CCM NA CDM.
   
 20. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  account ni yake na wabunge wenzake wapo naye..... amekuwa akitumia hiyo account kwa mawasilino na wabunge wenzake....... nenda twitter kafanye uchunguzi kama una wasi zaidi nenda website ya bunge chukua namba ya simu mpigie muulize
   
Loading...