mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,706
1: Wafia vyama, hapa hata kama mtu wa mlengo wake katapika atasema katema mate. Wako tayari kusema chochote kwa gharama ya kulinda chama chake.
2: Wafuata watu au wanasiasa maarufu: kuna watu wanawafuata watu hata wahame vyama kumi wako nao. kwa watu hawa sema chochote kuhusu siasa ila usimpe changamoto mwanasiasa wake anaomfuata na kumwamini.
3: Wafuasi na watu wanaoamini katika serikali hii iliyopo madarakani (na mimi nimo).
hawa nao wengine wanavyma wengine hawana lkn hupingwa vikali na kuitwa kila jina na wakosoaji wa serikali hii.
4: Watu wasio na upande wowote, hubadilika kulingana na hoja iliyopo bila kujali inaunga mkono upande gani. wengine kwa kuchagua mfumo huu wameonekana vigeugeu.
5: Wavizia madaraka. Hawa ni watu ambao hawaweki rangi yao hadharani lkn chochote wanachokifanya,hoja wanayoijenga ni ili wasikike na kuonekana wenda siku moja wakaukwaa ugali kwa jina la siasa. hawa ni wengi verified na anonymous na wengine huvizia nafasi hata vyama pinzani kwa misingi ya JF.
6: Walioathiliwa na utawala huu kwa kwa wazi,moja kwa moja au kwa kinyumenyume katika vitumbua vyao. nao sauti zao hupenya kwenye baobonye(keyboard) kama sehemu ya kuonyesha na wao wanapinga kwa sababu tu wameathiliwa sio kwa sababu wanajambo la msingi ktk kupinga kwao mambo yanayoendelea.
7: Wachangiaji waanzisha mada wapenda maendeleo na wasiopenda kujadili mambo hasi muda wote. bali wanapojadili huwa na masuluhisho.
hawa sio wasemaji sana ili kukwepa mashambulizi ya makundi yanayoona kama anachokifanya ni kumpa nafuu asiyempenda.
" Where we dare to talk openly"