Aina saba ya wachangiaji na waanzisha Mada Jukwaa la Siasa

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,702
1: Wafia vyama, hapa hata kama mtu wa mlengo wake katapika atasema katema mate. Wako tayari kusema chochote kwa gharama ya kulinda chama chake.

2: Wafuata watu au wanasiasa maarufu: kuna watu wanawafuata watu hata wahame vyama kumi wako nao. kwa watu hawa sema chochote kuhusu siasa ila usimpe changamoto mwanasiasa wake anaomfuata na kumwamini.

3: Wafuasi na watu wanaoamini katika serikali hii iliyopo madarakani (na mimi nimo).
hawa nao wengine wanavyma wengine hawana lkn hupingwa vikali na kuitwa kila jina na wakosoaji wa serikali hii.

4: Watu wasio na upande wowote, hubadilika kulingana na hoja iliyopo bila kujali inaunga mkono upande gani. wengine kwa kuchagua mfumo huu wameonekana vigeugeu.

5: Wavizia madaraka. Hawa ni watu ambao hawaweki rangi yao hadharani lkn chochote wanachokifanya,hoja wanayoijenga ni ili wasikike na kuonekana wenda siku moja wakaukwaa ugali kwa jina la siasa. hawa ni wengi verified na anonymous na wengine huvizia nafasi hata vyama pinzani kwa misingi ya JF.

6: Walioathiliwa na utawala huu kwa kwa wazi,moja kwa moja au kwa kinyumenyume katika vitumbua vyao. nao sauti zao hupenya kwenye baobonye(keyboard) kama sehemu ya kuonyesha na wao wanapinga kwa sababu tu wameathiliwa sio kwa sababu wanajambo la msingi ktk kupinga kwao mambo yanayoendelea.

7: Wachangiaji waanzisha mada wapenda maendeleo na wasiopenda kujadili mambo hasi muda wote. bali wanapojadili huwa na masuluhisho.
hawa sio wasemaji sana ili kukwepa mashambulizi ya makundi yanayoona kama anachokifanya ni kumpa nafuu asiyempenda.

" Where we dare to talk openly"
 
Hao namba 3.(Ulipo wewe pia). Wanaoamini katika serikali hii ilipo madarakani wana sifa zifuatazo.
1)Kupongeza kwa kila kitu hata wakiambiwa tumejenga viwanda 3000 na wao hawajui japo viwanda 3 physically vilipo.
2)Kutetea na kuunga mkono chochote kitakachofanywa/kutamkwa hata kama kina chembechembe za kuvunja katiba.
3) Kuamini katika takwimu na siyo katika uhalisia.Unakuta MTU anaambiwa uchhmi wetu unakua kwa kupaa hata kama yeye na wote wanaomzunguka wana hali mbaya utasikia anafurahi na kurukaruka.
4)Wapo wa namna mbili kuu katika kundi hili.WANAONUFAIKA NA SAHANI YA MFALME/WANAOTEGEMEA KUNUFAIKA, na WASIO NA ELIMU
 
maoni mazuri...
matumizi bora ya uhuru wa kuchangia hata kama maoni ni potofu
 
Wasifia kila kitu Hawa wengi wako Lumumba kama mtoa mada.

Mfano Rais akisema siongezi mishahara kwa watumishi watamuunga mkono na kusifia akija akisema Nitaongeza mishahara kwa watumishi wataunga mkono tena na kusifia.

Ni kheri uwe mkosoaji Wa kila kitu kuliko kuwa msifiaji Wa kila kitu, maana ipo siku mtu atatembea uchi barabarani bado watamsifia na kusema "hiyo ni fashion mpya ya mjini"
 
naona unaonyesha uwezo finyu wa kutofautisha kuunga mkono serikali na kusifia kila kitu.
 
Watu wenye fikra nyepesi hujadili watu,na watu wenye fikra ya kati hujadili matukio,na wale wenye fikra PEVU hujadili DHANA.Lakini ktk kujadili dhana wale wasomi wapumbavu na wapumbavu wengine hawahusiki ktk kujadili dhana maana hufikiri kwakutumia njaa zao.
 
maoni mazuri...
matumizi bora ya uhuru wa kuchangia hata kama maoni ni potofu
Mkuu eleza upotofu ulioko hapo.Waumini wa serikali iliyomadarakani sifa nilizoziorodhesha ndivyo walivyo.Mfano wewe unavifahamu viwanda vingapi physically, kati ya elfu 3 vilivyotajwa juzi?.
Hata kutumia common sense hakuna!Viwanda elfu tatu vianzishwe ndani ya miaka miwili husitokee mvumo?.Katika ajira hapo Tungepata maafisa manunuzi kwa uchache 3000,Maafisa utumishi kwa uchache 3000,wahasibu 5000 plus,waendesha mitambo kwa uchache 30,000 ,Wakirugenzi watendaji 3000,wahudumu wa ofisi 9000 plus,maafisa masoko 3000 plus na wengine wengi.Unadhani ingekuwa halisi kungekuwa na haja ya kutuorodheshea na kututangazia?.Tungeona tu vijana wanaajiriwa kwa wingi na mambo mengine.Sasa nyie mkiambiwa tu mnapongezaaaaaà na kusema huyu aongezewe miaka.
 
Watu wenye fikra nyepesi hujadili watu,na watu wenye fikra ya kati hujadili matukio,na wale wenye fikra PEVU hujadili DHANA.Lakini ktk kujadili dhana wale wasomi wapumbavu na wapumbavu wengine hawahusiki ktk kujadili dhana maana hufikiri kwakutumia njaa zao.
quote nzuri ya first lady maarufu duniani lkn haifanyikazi kila sehemu na kila wakati.
Deal ya kwanza ya trump ilibidi afunge safari kwenda ujerumani angalau amjue mteja ili katika negotiation aweze kumshawishi afanye nae biashara. angebaki na hoja kama yako angeambulia patupu.
human psychology inasaidia kujua hata hiyo idea unajadili na nani.
quotes sio misahafu ni kama mithali tu zina faida na mapungufu.

sio kila mti unakatwa na panga, mingine chainsaw mkuu.hata quotes zirandane na mazingira
 
Hao namba 3.(Ulipo wewe pia). Wanaoamini katika serikali hii ilipo madarakani wana sifa zifuatazo.
1)Kupongeza kwa kila kitu hata wakiambiwa tumejenga viwanda 3000 na wao hawajui japo viwanda 3 physically vilipo.
2)Kutetea na kuunga mkono chochote kitakachofanywa/kutamkwa hata kama kina chembechembe za kuvunja katiba.
3) Kuamini katika takwimu na siyo katika uhalisia.Unakuta MTU anaambiwa uchhmi wetu unakua kwa kupaa hata kama yeye na wote wanaomzunguka wana hali mbaya utasikia anafurahi na kurukaruka.
4)Wapo wa namna mbili kuu katika kundi hili.WANAONUFAIKA NA SAHANI YA MFALME/WANAOTEGEMEA KUNUFAIKA, na WASIO NA ELIMU
Salute kwako, maana umefafanuka vizuri. Mimi ningesema 'wenye uthubutu wa kuiita chupi kofia kwa kuwa tu baba mkwe kaivaa kichwani'
 
Mkuu eleza upotofu ulioko hapo.Waumini wa serikali iliyomadarakani sifa nilizoziorodhesha ndivyo walivyo.Mfano wewe unavifahamu viwanda vingapi physically, kati ya elfu 3 vilivyotajwa juzi?.
Hata kutumia common sense hakuna!Viwanda elfu tatu vianzishwe ndani ya miaka miwili husitokee mvumo?.Katika ajira hapo Tungepata maafisa manunuzi kwa uchache 3000,Maafisa utumishi kwa uchache 3000,wahasibu 5000 plus,waendesha mitambo kwa uchache 30,000 ,Wakirugenzi watendaji 3000,wahudumu wa ofisi 9000 plus,maafisa masoko 3000 plus na wengine wengi.Unadhani ingekuwa halisi kungekuwa na haja ya kutuorodheshea na kututangazia?.Tungeona tu vijana wanaajiriwa kwa wingi na mambo mengine.Sasa nyie mkiambiwa tu mnapongezaaaaaà na kusema huyu aongezewe miaka.
narudia tena maoni yako mazuri ila potofu au naweza kuyaita maoni kokoro yaani yanataka kujumuisha aina mbalimbali ya waungaji mkono bila umakini wa utofauti wao.
kuunga mkono serikali haimaanishi hakuna chumba cha kukosoa kwa kujenga pale inapobidi. au kutoa ideas mpya.
mfano mimi naunga mkono serikali lakn naamini ktk science and technlogy na kilimo cha kisasa cha kibiashara ingekuwa njia ya haraka ya kutufikisha huku viwanda kuwa matokeo.
lkn pamoja na yote bado vyote hata mwenendo huu naona ni sawa na ukisimamiwa vizuri utaleta mafanikio."kupanga ni kuchagua".
Viwanda ni process huwezi kuona immediate impact. mfano mwaka jana afsa biashara wa wizara anayejiusisha na viwanda vidogo alisema kulikuwa na viwanda 1420 na akataja mazingira na mikoa vilipo ila akasisitiza vingi ni vya kati na vidogo.
chukua hatua tembelea wahusika wakupe taarifa kabla haujapinga.
wenda kwa scope ya hatua tuliyopo impact haijafikia kwenye mawazo yako
 
Huwezi kusifia kama huungi mkono.
kuunga mkono sio kama suala la mtihani wa true or false.
kuunga mkono utawala huu kwangu ni universal set.
ndani kuna subsets ambazo wenda zinaweza zisiwe sawa sana au zinahitaji ukosoaji chanya au maboresho au chochote kile kwa nia ya kujenga.
ni aina ya uchaguzi mwanadamu anaweza kuchagua mkuu.
katikati ya YES na NO kuna parameters nyingi tu mwanadamu anaweza kuchagua bila ushawishi wowote kutoka nje.
 
Back
Top Bottom