Aina mbili za Wakristo (wasoma Biblia)

Aina mbili za Wakristo (wasoma Biblia)

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
9,761
Reaction score
15,577
Katika kueleza makundi haya mawili ya waamini wa imani ijulikanayo kama Wakristo (maana yake wafuasi wa Yesu) kumekua bado na mzozo mkubwa hadi leo hii kuhusu mambo Muhimu sana kuhusu imani au dini hii.

1. Sheria (Torati)
2. Neema (Kuokolewa kwa imani)

Binafsi nimefatilia sheria sana sheria ambazo Waebrania wanazichukulia kama sheria za Mungu.

Kuhusu neema iliyoletwa na Yesu Kristo.
Waebrania 7:11-12
11 Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?

12 Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike.

TUNAPATA MAKUNDI MAWILI:
1. Wanaotaka sheria zote ziendelee kufatwa.
2. Na wanaosema sheria sio lazima tena. Kwanza ni nyingi na ngumu kuzishika zote.

Wagalatia 2:16
hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.

Sheria (Torati)
Katika Torati (vitabu vitano vya kwanza vya Biblia, yaani Musa), kuna aina mbili za "amri" ambazo mara nyingi hujadiliwa:

Amri Kumi (Decalogue): Hizi ndizo amri kuu zinazojulikana na wengi, ambazo Mungu alimpa Musa kwenye Mlima Sinai. Zimeorodheshwa katika kitabu cha Kutoka 20:1-17 na Kumbukumbu la Torati 5:6-21. Hizi kumi ndio msingi wa maadili na sheria nyingi.

Amri Zote (Mitzvot): Kijadi, Wayahudi wanaamini kwamba Torati ina jumla ya amri 613 (zinazojulikana kama "Mitzvot 613"). Hizi 613 zinajumuisha amri kumi na sheria nyingine nyingi zinazohusu nyanja mbalimbali za maisha, kama vile ibada, sheria za kijamii, chakula, usafi, na kadhalika. Amri hizi 613 zimegawanywa katika amri chanya (mambo ya kufanya) na amri hasi (mambo ya kutokufanya).

Kwa hivyo, jibu fupi ni kwamba kuna Amri Kumi ambazo ni muhimu sana na zinazojulikana sana, lakini kwa ujumla, mila ya Kiyahudi inafundisha kuwa kuna amri 613 katika Torati.

Sheria zilizovyunjwa na wanafunzi wa Yesu.
1. Kufanya kazi siku ya sabato.
2. Kuchangamana na wasio wayahudi.
3.

Hadi Yesu kuondoka bado Petro alikuwa anaaamini kwamba Kujazwa roho mtakatifu ni haki ya wayahudi peke yao, mataifa mengine haiwahusu.

Huitaji Torati kujua Mungu hapendi nini na anapenda nini mfano mzuri,

Isaka na ibrahimu waliishi vipi na kuwa karibu na Mungu kipindi ambacho torati haikuwepo bado ???

Kanisa la leo haliwezi kuhubiri neema (grace) kwani ulaji wao wa sadaka unatokana na sheria iliyotolewa na Musa katika Torati kuhusu matoleo, na ikumbukwe kuwa Mungu aliagiza matoleo kutoka katika Shamba na Mifugo, ambao walitokana na Ardhi ambayo Mungu kawapa.

Sasa wewe Mkristo wa leo unaambiwa toa fungu la Kumi na huku hakuna Ardhi umepewa kama urithi.

Petro atetea sio lazima Kutahiriwa
(Hapa kanisa lilifanya na kikao kupata maamuzi)
Matendo ya Mitume 15:10-11
10 Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua.

11 Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.

Niulize Swali
Kwanini mbaraka wa Isaka kwa mwanaume wa kwanza wa kiume uliweza kuibiwa na mtoto wa pili ambaye ni Yakobo ??

Inawezekana vip mbaraka kuibiwa ?? unaiba nguvu za Mungu ??

Yakobo alikuwa Muongo na Tapeli na alishindana na Ndugu yake tangu tumboni, akamshika kisigino pacha wake ambaye ni kaka yake.
kumvuta kisigino ilikuwa ni ishara.

Bado Mungu anajionesha na Kusema Nimempenda Yakobo bali Esau nimemkataa.

Upo kundi gani.
1. Kuwa mshika sheria, au
2. Kuwa msikivu na mtii.
3. Vyote viwili.

Nimewasikiliza wahubiri wakubwa duniani waalimu na Manabii

Je unawajua wahubiri wakubwa duniani na misimamo yao kuhusus Sheria na Neema ???
1. Billy Graham
2. Myles Munroe

Kwasasa manabii wakubwa dunia na maarufu ninao wajua na waofundisha mambo mazito.
1. Prophet Ubert Angel
2. Prophet Lovy Elias
3. Prophet Passion Java

Hawa wote ni manabii Giants kutoka Afrika, kama baba yake wa kiroho na Musa alikuwa Muafrika, na Musa akaowa Mkushi.

Bila kuwasahau waalimu wazuri.

1. Apostle Miz Mzwakhe Tancredi (South Africa)
2. Paul S. Joshua.
3. Prophet David Rauf

Huwezi kuongeza Nguvu au viwango vyako vya kiroho, Bila kumuelewa Mungu kwa usahihi zaidi.🙏🏾
 
Musa hakuwa muafrika ... Kushi inayoongelewa ilikuwa Iraq..Asili ya wayahudi wote ni Iraq..Na Baba Yao Ibrahim alikuwa muarami(Aramean) ...

Kuhusu Sheria ni kwamba hatuwezi kuitekeleza Sheria Kwa nguvu binafsi za miili yetu...Tumepewa nguvu na msaada WA roho mtakatifu atusaidie kuitimiza Sheria...Maaña yake holly sprit anadeal na chanzo cha Ile dhambi iliowekewa sheria
 
Yesu hajawai vunja sheria yoyote ya Baba yake na kusema kuwa Yesu alivunja sheria ni kumshuhudia uwongo.
yeye mwenyewe anasema"

John 15:10 states, "If you keep my commandments, you will abide in my love, just as I have kept my Father's commandments and abide in his love"

Yeye mwenyewe anajishuhudia kuwa ni mtunza sheria Mzuri.
Amri kumi za MUNGU ni za milele.Zimekuwepo toka Eden na zita kuwepo hadi kwenye ulimwengu mpya.

So,kusema" Yesu alivunja sheria"ni sawa na kusema Yesu ni M-dhambi maana dhambi ni kuvunja sheria.

1 John 3:4. It declares, "Everyone who sins is breaking God's law, for sin is a breaking of the
 
Tuambie hizi pumba zimefundishwa wapi ?
 
huijui sheria vizuri bado,

Kumbuka mahusiano na Mungu hayajengwi kwa kufata sheria.

Mungu akikupa maelekezo kuwa fanya jambo fulani, liwe nje au ndani ya sheria ni lazima kutekeleza.

Mfano sheria inasema Usiuwe.

Lakini si Myahudi si Muislam wote wapo tayari kuuwa kwaajili ya dini zao
 
Kwanza tumalizane na Madai ya Yesu kuwa mdhambi ama kutokuaa mdhambi ndiyo tuje swala la mimi kuijua Sheria ama kutoijua.
Ulisema"Yesu alivunja sheria" na mimi nikasema "Yesu hakuwai vunja sheria na nikakupa andiko akijishuhudia yeye mwenyewe kuwa mtunza sheria".

wayahudi walimpima Yesu kupitia Dogma za Dini yao na Sio Sheria na ndiyo maana Yesu anawambia Wayahudi Mark 7:8
You have let go of the commands of God and are holding on to human traditions".

anawashtumu Wayahudi kwa kuacha sheria za Mungu na kufuata dogma zao.

Sabato ni siku ya Mungu wa Wayahudi,hakuna pahari huyo Mungu wao aliwazuia watu wasiponywe siku ya Sabato ila dogma zao zinazuia.

Ufu 14:12 SUV
Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.

watakarifu ni wale washikao sheria na Iman ya kristo.

tusijadili Bible kwenye Mrengo wa kidhehebu.
 
Shida umekuja kasi ya ngiri bila umakini ?

Sijasema Yesu kavunja Sheria.
Nimesema wanafunzi wake. acha ubumunda basi.
 
Mkuu tafuta pia kuna makundi haya, Hii pia inaleta utata sana - Kuna Continuanism na Cessiotionism.

Japo continuanism ina make sence.
 
Kakimbilia misri?? Misri ndio alipokimbia baada ya kuua akaenda midiani?? Wewe unaijua midiani iko wapi???

Uwe unauliza au kupitia vyanzo sahihi Ili usije ukarudia kuandika vichekesho Kama hivi
umeshinda boss
 
Musa siyo mwafrika .ni mwebrania mahindi ndo maana aliwatetea waebrania wenzake
 
Katika kueleza makundi haya mawili ya waamini wa imani ijulikanayo kama Wakristo (maana yake wafuasi wa Yesu) kumekua bado na mzozo mkubwa hadi leo hii kuhusu mambo Muhimu sana kuhusu imani au dini hii.

1. Sheria (Torati)
2. Neema (Kuokolewa kwa imani)

Binafsi nimefatilia sheria sana sheria ambazo Waebrania wanazichukulia kama sheria za Mungu.

Kuhusu neema iliyoletwa na Yesu Kristo.
Waebrania 7:11-12
11 Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?

12 Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike.

TUNAPATA MAKUNDI MAWILI:
1. Wanaotaka sheria zote ziendelee kufatwa.
2. Na wanaosema sheria sio lazima tena. Kwanza ni nyingi na ngumu kuzishika zote.

Wagalatia 2:16
hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.

Sheria (Torati)
Katika Torati (vitabu vitano vya kwanza vya Biblia, yaani Musa), kuna aina mbili za "amri" ambazo mara nyingi hujadiliwa:

Amri Kumi (Decalogue): Hizi ndizo amri kuu zinazojulikana na wengi, ambazo Mungu alimpa Musa kwenye Mlima Sinai. Zimeorodheshwa katika kitabu cha Kutoka 20:1-17 na Kumbukumbu la Torati 5:6-21. Hizi kumi ndio msingi wa maadili na sheria nyingi.

Amri Zote (Mitzvot): Kijadi, Wayahudi wanaamini kwamba Torati ina jumla ya amri 613 (zinazojulikana kama "Mitzvot 613"). Hizi 613 zinajumuisha amri kumi na sheria nyingine nyingi zinazohusu nyanja mbalimbali za maisha, kama vile ibada, sheria za kijamii, chakula, usafi, na kadhalika. Amri hizi 613 zimegawanywa katika amri chanya (mambo ya kufanya) na amri hasi (mambo ya kutokufanya).

Kwa hivyo, jibu fupi ni kwamba kuna Amri Kumi ambazo ni muhimu sana na zinazojulikana sana, lakini kwa ujumla, mila ya Kiyahudi inafundisha kuwa kuna amri 613 katika Torati.

Sheria zilizovyunjwa na wanafunzi wa Yesu.
1. Kufanya kazi siku ya sabato.
2. Kuchangamana na wasio wayahudi.
3.

Hadi Yesu kuondoka bado Petro alikuwa anaaamini kwamba Kujazwa roho mtakatifu ni haki ya wayahudi peke yao, mataifa mengine haiwahusu.

Huitaji Torati kujua Mungu hapendi nini na anapenda nini mfano mzuri,

Isaka na ibrahimu waliishi vipi na kuwa karibu na Mungu kipindi ambacho tarati haikuwepo bado ???

Kanisa la leo haliwezi kuhubiri neema (grace) kwani ulaji wao wa sadaka unatokana na sheria iliyotolewa na Musa katika Torati kuhusu matoleo, na ikumbukwe kuwa Mungu aliagiza matoleo kutoka katika Shamba na Mifugo, ambao walitokana na Ardhi ambayo Mungu kawapa.

Sasa wewe Mkristo wa leo unaambiwa toa fungu la Kumi na huku hakuna Ardhi umepewa kama urithi.

Petro atetea sio lazima Kutahiriwa
(Hapa kanisa lilifanya na kikao kupata maamuzi)
Matendo ya Mitume 15:10-11
10 Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua.

11 Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.

Niulize Swali
Kwanini mbaraka wa Isaka kwa mwanaume wa kwanza wa kiume uliweza kuibiwa na mtoto wa pili ambaye ni Yakobo ??

Inawezekana vip mbaraka kuibiwa ?? unaiba nguvu za Mungu ??

Yakobo alikuwa Muongo na Tapeli na alishindana na Ndugu yake tangu tumboni, akamshika kisigino pacha wake ambaye ni kaka yake.
kumvuta kisigino ilikuwa ni ishara.

Bado Mungu anajionesha na Kusema Nimempenda Yakobo bali Esau nimemkataa.

Upo kundi gani.
1. Kuwa mshika sheria, au
2. Kuwa msikivu na mtii.
3. Vyote viwili.

Nimewasikiliza wahubiri wakubwa duniani waalimu na Manabii

Je unawajua wahubiri wakubwa duniani na misimamo yao kuhusus Sheria na Neema ???
1. Billy Graham
2. Myles Munroe

Kwasasa manabii wakubwa dunia na maarufu ninao wajua na waofundisha mambo mazito.
1. Prophet Ubert Angel
2. Prophet Lovy Elias
3. Prophet Passion Java

Hawa wote ni manabii Giants kutoka Afrika, kama baba yake wa kiroho na Musa alikuwa Muafrika, na Musa akaowa Mkushi.

Bila kuwasahau waalimu wazuri.

1. Apostle Miz Mzwakhe Tancredi (South Africa)
2. Paul S. Joshua.
3. Prophet David Rauf

Huwezi kuongeza Nguvu au viwango vyako vya kiroho, Bila kumuelewa Mungu kwa usahihi zaidi.🙏🏾
Hatuhesabiwi haki kwa njia ya Sheria bali kwa neema.Yani Ile neema ndiyo inayokuwezesha kuishika na kuiishi Sheria .mfano : huwezi kushinda dhambi yoyote bila Neema kukuwezesha kushinda hiyo dhambi.Neema inakupa uelewa wa ndani wa kwa Nini usitende dhambi!!Neema inakupa nguvu ya ushindi wa dhambi!! Neema ni aiana ya uungu itendayo kazi ndani ya Mtu!! Yani ,Neema ikiwa ndani yako huoni ugumu wa kuishika sharia.Neema ni Yesu mwenyewe.ukiwa na Yesu ndani yako huwezi kutenda dhambi!!Mfano Mimi kabla ya kupata hii neema nilikuwa mzinzi sana lakini tangia nilipopata neema hii mwaka 2001 mpaka naoa 2007 sijawahi hata kumwambia msichana kwamba nampenda! Mpaka Leo sijawahi zini Wala kutoka nje ya ndoa!! Why? Kwa sababu Ile neema imenifunulia ubaya wa dhambi na imeniwezesha kushinda Ile dhambi! Sheria au amri kwamba usizini niliijua lakini kujua kwa Sheria Ile hakukunifanya nisizini!! Neema inatukataza kutenda dhambi Yani inatuwezesha kuzishika zile amri au Sheria bila ugumu wowote.

Kazi ya neema :

Tito 2:11-12
[11]Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men,
[12]nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly, in this present world;
 
Hatuhesabiwi haki kwa njia ya Sheria bali kwa neema.Yani Ile neema ndiyo inayokuwezesha kuishika na kuiishi Sheria .mfano : huwezi kushinda dhambi yoyote bila Neema kukuwezesha kushinda hiyo dhambi.Neema inakupa uelewa wa ndani wa kwa Nini usitende dhambi!!Neema inakupa nguvu ya ushindi wa dhambi!! Neema ni aiana ya uungu itendayo kazi ndani ya Mtu!! Yani ,Neema ikiwa ndani yako huoni ugumu wa kuishika sharia.Neema ni Yesu mwenyewe.ukiwa na Yesu ndani yako huwezi kutenda dhambi!!Mfano Mimi kabla ya kupata hii neema nilikuwa mzinzi sana lakini tangia nilipopata neema hii mwaka 2001 mpaka naoa 2007 sijawahi hata kumwambia msichana kwamba nampenda! Mpaka Leo sijawahi zini Wala kutoka nje ya ndoa!! Why? Kwa sababu Ile neema imenifunulia ubaya wa dhambi na imeniwezesha kushinda Ile dhambi! Sheria au amri kwamba usizini niliijua lakini kujua kwa Sheria Ile hakukunifanya nisizini!! Neema inatukataza kutenda dhambi Yani inatuwezesha kuzishika zile amri au Sheria bila ugumu wowote.
Yesu aliacha sheria ya kuowa mke mmoja, lakini zamani kidogo ndoa za wake wengi zililuhusiwa, au taraka zamani ilikua ruksa

Unafikir Mungu wa agano la kale na Mungu kipindi cha Agano jipya kabadilika Hekima na Akili zake ????

Mathayo 19:8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.

Unabisha sheria haikuwa na Mapungufu ???
 
Katika kueleza makundi haya mawili ya waamini wa imani ijulikanayo kama Wakristo (maana yake wafuasi wa Yesu) kumekua bado na mzozo mkubwa hadi leo hii kuhusu mambo Muhimu sana kuhusu imani au dini hii.

1. Sheria (Torati)
2. Neema (Kuokolewa kwa imani)

Binafsi nimefatilia sheria sana sheria ambazo Waebrania wanazichukulia kama sheria za Mungu.

Kuhusu neema iliyoletwa na Yesu Kristo.
Waebrania 7:11-12
11 Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?

12 Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike.

TUNAPATA MAKUNDI MAWILI:
1. Wanaotaka sheria zote ziendelee kufatwa.
2. Na wanaosema sheria sio lazima tena. Kwanza ni nyingi na ngumu kuzishika zote.

Wagalatia 2:16
hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.

Sheria (Torati)
Katika Torati (vitabu vitano vya kwanza vya Biblia, yaani Musa), kuna aina mbili za "amri" ambazo mara nyingi hujadiliwa:

Amri Kumi (Decalogue): Hizi ndizo amri kuu zinazojulikana na wengi, ambazo Mungu alimpa Musa kwenye Mlima Sinai. Zimeorodheshwa katika kitabu cha Kutoka 20:1-17 na Kumbukumbu la Torati 5:6-21. Hizi kumi ndio msingi wa maadili na sheria nyingi.

Amri Zote (Mitzvot): Kijadi, Wayahudi wanaamini kwamba Torati ina jumla ya amri 613 (zinazojulikana kama "Mitzvot 613"). Hizi 613 zinajumuisha amri kumi na sheria nyingine nyingi zinazohusu nyanja mbalimbali za maisha, kama vile ibada, sheria za kijamii, chakula, usafi, na kadhalika. Amri hizi 613 zimegawanywa katika amri chanya (mambo ya kufanya) na amri hasi (mambo ya kutokufanya).

Kwa hivyo, jibu fupi ni kwamba kuna Amri Kumi ambazo ni muhimu sana na zinazojulikana sana, lakini kwa ujumla, mila ya Kiyahudi inafundisha kuwa kuna amri 613 katika Torati.

Sheria zilizovyunjwa na wanafunzi wa Yesu.
1. Kufanya kazi siku ya sabato.
2. Kuchangamana na wasio wayahudi.
3.

Hadi Yesu kuondoka bado Petro alikuwa anaaamini kwamba Kujazwa roho mtakatifu ni haki ya wayahudi peke yao, mataifa mengine haiwahusu.

Huitaji Torati kujua Mungu hapendi nini na anapenda nini mfano mzuri,

Isaka na ibrahimu waliishi vipi na kuwa karibu na Mungu kipindi ambacho tarati haikuwepo bado ???

Kanisa la leo haliwezi kuhubiri neema (grace) kwani ulaji wao wa sadaka unatokana na sheria iliyotolewa na Musa katika Torati kuhusu matoleo, na ikumbukwe kuwa Mungu aliagiza matoleo kutoka katika Shamba na Mifugo, ambao walitokana na Ardhi ambayo Mungu kawapa.

Sasa wewe Mkristo wa leo unaambiwa toa fungu la Kumi na huku hakuna Ardhi umepewa kama urithi.

Petro atetea sio lazima Kutahiriwa
(Hapa kanisa lilifanya na kikao kupata maamuzi)
Matendo ya Mitume 15:10-11
10 Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua.

11 Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.

Niulize Swali
Kwanini mbaraka wa Isaka kwa mwanaume wa kwanza wa kiume uliweza kuibiwa na mtoto wa pili ambaye ni Yakobo ??

Inawezekana vip mbaraka kuibiwa ?? unaiba nguvu za Mungu ??

Yakobo alikuwa Muongo na Tapeli na alishindana na Ndugu yake tangu tumboni, akamshika kisigino pacha wake ambaye ni kaka yake.
kumvuta kisigino ilikuwa ni ishara.

Bado Mungu anajionesha na Kusema Nimempenda Yakobo bali Esau nimemkataa.

Upo kundi gani.
1. Kuwa mshika sheria, au
2. Kuwa msikivu na mtii.
3. Vyote viwili.

Nimewasikiliza wahubiri wakubwa duniani waalimu na Manabii

Je unawajua wahubiri wakubwa duniani na misimamo yao kuhusus Sheria na Neema ???
1. Billy Graham
2. Myles Munroe

Kwasasa manabii wakubwa dunia na maarufu ninao wajua na waofundisha mambo mazito.
1. Prophet Ubert Angel
2. Prophet Lovy Elias
3. Prophet Passion Java

Hawa wote ni manabii Giants kutoka Afrika, kama baba yake wa kiroho na Musa alikuwa Muafrika, na Musa akaowa Mkushi.

Bila kuwasahau waalimu wazuri.

1. Apostle Miz Mzwakhe Tancredi (South Africa)
2. Paul S. Joshua.
3. Prophet David Rauf

Huwezi kuongeza Nguvu au viwango vyako vya kiroho, Bila kumuelewa Mungu kwa usahihi zaidi.🙏🏾
sammarize tukuelewe upo upande gan ww mtoa mada na hao manabii wako !....nakula ugali dagaa hapa .
 
Kwanza tumalizane na Madai ya Yesu kuwa mdhambi ama kutokuaa mdhambi ndiyo tuje swala la mimi kuijua Sheria ama kutoijua.
Ulisema"Yesu alivunja sheria" na mimi nikasema "Yesu hakuwai vunja sheria na nikakupa andiko akijishuhudia yeye mwenyewe kuwa mtunza sheria".

wayahudi walimpima Yesu kupitia Dogma za Dini yao na Sio Sheria na ndiyo maana Yesu anawambia Wayahudi Mark 7:8
You have let go of the commands of God and are holding on to human traditions".

anawashtumu Wayahudi kwa kuacha sheria za Mungu na kufuata dogma zao.

Sabato ni siku ya Mungu wa Wayahudi,hakuna pahari huyo Mungu wao aliwazuia watu wasiponywe siku ya Sabato ila dogma zao zinazuia.

Ufu 14:12 SUV
Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.

watakarifu ni wale washikao sheria na Iman ya kristo.

tusijadili Bible kwenye Mrengo wa kidhehebu.
Yn 5:17 SUV
[17] Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.

Yesu alisema maneno kama hayo huoni kuwa alikuwa kinyume na Sheria...

Sheria inasema "Usifanye kazi yoyote" Lakini Yesu akawaambia Yeye na Baba yake wanafanya kazi hata siku ya Sabato.

Lakini mkuu moja ya sheria ali-quote Yesu inasema hivi;
Mathayo 15:4 BHN
[4] Mungu amesema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na ‘Anayemtukana baba yake au mama yake, lazima auawe.’

Je sheria hiyo unaifuata au kuna namna umeirekebisha?

Sheria zingine ni hizi, je unazifuata pia au kuna namna umezirekebisha

Kutoka 22:18-19 BHN
[18] “Usimwache mwanamke mchawi aishi. [19] “Anayezini na mnyama lazima auawe.
 
Ufu 14:12 SUV
Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.

watakarifu ni wale washikao sheria na Iman ya kristo.
Ndiyo watakatifu ni wale washikao sheria na Imani ya Kristo.
Lakini lazima ujue Sheria ya Kristo ni ipi? Sheria ziko za aina mbili
1. Sheria ya Roho iletayo Uzima.
2. Sheria ya Dhambi iletayo mauti.

Rum 8:2 SUV
[2] Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Torati ndiyo iletayo dhambi na matunda yake ni mauti (Torati ndiyo Sheria ya Dhambi na Mauti).
Andiko hilo katika ufunuo limesema Amri/Sheria za Mungu na imani ya kristo, Amri za Mungu alizomaanisha hapo hapo siyo Amri kumi au TORATI.
 
sammarize tukuelewe upo upande gan ww mtoa mada na hao manabii wako !....nakula ugali dagaa hapa .
Bila shaka atakuwa upande wa neema.
Kumbuka kuna sheria 613, hizo hakuna mwenye uwezo wa kuzishika ila kwa neema ya Yesu tunapata kuokolewa na siyo kwa matendo ya sheria.
 
sasa kama tunaokolewa kwa neema peke yake basi hakuna atakayeenda jehanamu.....utanipeleka jehanamu kwakigezo kipi? .......na utatumia nini kuhukumu.....? wote tunasepa pepon kula mabkra
 
Rum 3:23-26​

kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu.

Maoni yangu.

Anayejua akina nani wataenda na akina nani hawaendi Mbinguni ni Mungu mwenyewe.

Sisi jukumu letu ni kumuamini Mungu na Yesu Kristo huku tukitenda yaliyo mema na kuishi kwa mapenzi na mwongozo wa Roho Mtakatifu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom