Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 53,159
- 72,199
Habari za muda huu wanajukwaa, ni mara nyingine tunakutana katika jukwaa letu hili pendwa kwa ajili ya kujifunza.
Nikienda moja kwa moja kwenye mada, leo katika pitapita zangu huku na huko, nikakutana na hii mada na nimeileta hapa tujifunze..
Zifuatazo ni aina kumi za WANAWAKE wanaopendwa na WANAUME;
A. WENYE MSIMAMO
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, walio makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
B. WAPENDA USAWA
Aina inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50
C. WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa niuwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwasita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani
D. MARAFIKI
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume.Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida naraha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani
E. WAPENDA UWAZI
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo nawapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.
F. WANAOJITEGEMEA
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina ‘naomba vocha’ au wapiga vibomu kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.
G. WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe nakazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi
H. MARIDADI(Warembo)
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini pia ni waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano.
I. WANAORIDHIKA
Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke
J. WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana.“Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.”Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana..
Karibuni kwa majadiliano, kama una nyongeza/chochote unaweza ukaweka
CREDITS TO: Lukemusicfactory and Dodoma Clan